Wazee wa Simba wamechoka

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,307
12,604
Timu zetu za VPL zimejaa vijana wengi wanaocheza kwenye viwanja vibovu sana. Vijana hawa wanapambana ili kupata nafasi ya kucheza Simba na Yanga na pengine Azam na nje ya nchi.

Simba kuna hela vijana wanafahamu hivyo lakini kinachowashangaza ni kuwaona wazee wengi kama Bocco, Ajibu, Onyango, Kagere, Mkude, Wawa, na Nyoni wako Simba pamoja na uzee wao.

Wazee kama hawa hawawezi kuchezeshwa mfululizo kila mechi kwenye viwanja vibovu dhidi ya timu zilizojaa vijana na askali wengi. Kama wazee watapata majeraha (sprain) kidogo tu kupona kwake ni shuhuli kubwa. Wazee hawa huwezi kuwategemea wacheze back to back ligi na mashindano ya champions kwa wakati mmoja.

usichangae simba ikawa mbovu sana round ya pili, la sivyo ianze sasa kuwapa nafasi vijana wacheze mara kwa mara
 
Wazee kama hawa hawawezi kuchezeshwa mfululizo kila mechi kwenye viwanja vibovu dhidi ya timu zilizojaa vijana na askali wengi. Kama wazee watapata majeraha (sprain) kidogo tu kupona kwake ni shuhuli kubwa
Kwa hiyo unashauri timu ziwe zinasajili vijana wanaojua kucheza viwanja vibovu, sio?
 
Kwa hiyo unashauri timu ziwe zinasajili vijana wanaojua kucheza viwanja vibovu, sio?
kwa manufaa ya wazee wetu viwanja viwekewe dimba la nyasi bandia ili kuwanusuru wazee. Vijana hata wakicheza kwenye uwanja wenye visiki vya mikarambati sio shida sana, kupona kwao sio shida
 
Vijana hata wakicheza kwenye uwanja wenye visiki vya mikarambati sio shida sana, kupona kwao sio shida
kijana Juma Mahadhi amekaa nje zaidi ya msimu mzima akiwa hajapona, msimu wa usajili Yanga wakaamua kumsajili na majeraha yake wakamuacha mzee Ngassa aliekuwa fit. Hadi leo hajapona. kijana Paul Godfrey 'Boxer' amekaa nje zaidi ya nusu msimu, akajaribu kurudi akatonesha tena, amecheza mechi moja tu msimu mzima, Yanga walimsajili wakamuacha mzee Juma Abdul aliyekuwa fit kabisa. Bado natafakari hoja yako kwamba wazee wanachelewa kupona kuliko vijana
 
Timu zetu za VPL zimejaa vijana wengi wanaocheza kwenye viwanja vibovu sana. Vijana hawa wanapambana ili kupata nafasi ya kucheza Simba na Yanga na pengine Azam na nje ya nchi.

Simba kuna hela vijana wanafahamu hivyo lakini kinachowashangaza ni kuwaona wazee wengi kama Bocco, Ajibu, Onyango, Kagere, Mkude, Wawa, na Nyoni wako Simba pamoja na uzee wao.

Wazee kama hawa hawawezi kuchezeshwa mfululizo kila mechi kwenye viwanja vibovu dhidi ya timu zilizojaa vijana na askali wengi. Kama wazee watapata majeraha (sprain) kidogo tu kupona kwake ni shuhuli kubwa. Wazee hawa huwezi kuwategemea wacheze back to back ligi na mashindano ya champions kwa wakati mmoja.

usichangae simba ikawa mbovu sana round ya pili, la sivyo ianze sasa kuwapa nafasi vijana wacheze mara kwa mara
Watahonga tu.
 
Watanzania bila kuacha upumbavu wa usimba na uyanga....mtaendelea kuwa mbumbumbu katika mashindano ya kimataifa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom