Juzi nimepanda hili hili Nganga la kwenye picha, dereva akasema hili scandal lilimkosa kwa bahati mbaya tu, cause na yeye alikuwa anataka afanye over-taking bahati tu akasita wenzake wote wakapita, kumbe kuna jamaa ana camera.
Aliishia kula ujiko na sifa kibao kumbe ndio wale wale
Ndo maana FALCON na TAQWA wanazitumia sana.
Happy nation ya mbeya -dar iangaliwe kwakweli,inaenda c mchezo asee.
Mkuu hizo basi hao wamanga wanazipenda sababu zinatembea sana kwenye tambalale na ndio maana hata ligi ya lusaka Nakonde wazambia wanaziogopa sana hizo basi zinatembea balaa na wakati huo zinakuwa zimetoka zimbabwe ujue mkuu na pia zimbabwe nako wanaziogopa ni nyepesi ktk mwendo.ila milimani haziwezi mfano za Dar-Burundi zinapata tabu sana milimani
nilipanda taqwa mwezi wa 11mwaka jana toka mbeya kwenda dar aisee hizo spidi ni kali balaaaa Mungu mwenyewe ni mwema,nimeapa kutopanda hizo gari tena
Mkuu hupendi gari inayofunguka?
Ile sauti ya Manka kwanza halichoki New Force Zimekuja zimechoka yenyewe ipo tuu.Ukitaka ujue hiyo gari inakimbia nenda nayo mbeya yaani Kitonga saa sita na nusu saa saba ushafika.Mkuu hiyo ni Happy nation SAUTI YA MANKA usipende kulipanda hilo bus linakimbia sana lina engine ya lori 124 gear 8 horsepower 360.hilo basi panda km unataka kuwahi ila kiusalama sio zuri linakimbia sana