Wazee wa DSM na JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazee wa DSM na JK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MkimbizwaMbio, Nov 19, 2011.

 1. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #1
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nikijiuliza,
  Kwa nini kila mara JK anapokuwa na dukuduku hukimbilia kuongea na wazee wa jiji la Dar es Salaam.
  Hivi hawa wazee ndio Habari Maelezo ya JK???
  Kuna nini hapa. Mbona sijasikia akiongea na Vijana wa DSM walio wengi kuliko hao wazee.

  Mwenye kujua siri kati ya JK na Wazee wa DSM atujuze.
   
 2. N

  NURFUS Member

  #2
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kiukweili hata mimi najiuliza kila siku pale mkuu wetu anapokuwa na dukuduku linalohusu mstakabali wa nchi hii iliyo huru na amani ya mdomoni huamua kuongea na wazee wa dar, hivi ndio kusema hao wazee ndio wenye busara sana zenye kuwakilisha watanzania wote au ndio yeye anaona wanafaa kwa hoja anazokuwa nazo?? Na kwanini hao wazee huja na uniforms za chama tawala tu na sio wazee kwa ujumla yao. Me nafikri next time aseme tu kwa uwazi kuwa ataongea na wazee wa ssm na sio wa dar ambao nafikiri anafikiri hao wazee huwakilisha wazee wa tanzania nzima.
   
 3. Makucha

  Makucha JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sioni tatizo ila busara Jk kuongea na wazee anapokuwa na dukuduku, hata Mwl. alifanya hivyo na anapoongea na wazee na sisi tunasikia. Ila tungependa aongee na vijana na makundi mengine kwa pamoja pia ili na wao watakapokuwa wazee wawe wana uzoefu wa kutosha kumshauri rais atakapoongea na wazee siku zijazo.
   
 4. Brine

  Brine JF-Expert Member

  #4
  Nov 19, 2011
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 376
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  kwa sababu bado wanafikira za kizamani na hawawezi kumchallenge
   
 5. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #5
  Nov 19, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Jana nilishangaa kidogo pale mkuu wa nchi rais JK,pamoja na mapungufu mengine alipoamua kuliongelea suala nyeti la katiba ya nchi yetu,ambalo ni lete sote kwa wazee wa CCM pekee?Hii ina maana ni mali ya wana CCM tu?
   
 6. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #6
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,607
  Likes Received: 4,710
  Trophy Points: 280
  Yeye anamuiga Mwalimu, hana sababu zaidi ya hiyo, siyo mbunifu.
   
 7. M

  Maliyamoto Member

  #7
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa nimeamini kwamba hata kipindi cha Uongozi wa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere, "makahaba walikuwepo na inawezekana waliokubuhu kuliko tulinao kwa sasa.." Kama utapata fursa ya kusikia style ya bibi zetu walizokuwa wakitumia kumshangilia M/Kiti wa CCM MH. Jk, tutakubaliana wote juu ya hili..

  Aibu gani hii jamani....?
   
 8. k

  kivike Tito I Member

  #8
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nimeamin ukizeeka uwezo wa kufikiri unarud nyuma,sitak kabisa kukumbuka aibu ya jana,nahis walikuwa wanashangilia wasichokijua
   
 9. Aaronium

  Aaronium Senior Member

  #9
  Nov 19, 2011
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Well, shida ipo kubwa sana! kuna wazee kila mkoa hapa Tanganyika, angetumia busara akazungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari kama inavyokuwa mara zote kufikisha ujumbe wa kitaifa kwa taifa ambalo yeye ni mkuu, sasa hata akizungumza na vijana kwa mfano, wanawake, wanaume peke yao tena wale wa CCM ambao wanpewa pilau na kusinzia, hebu ieleweke kwamba mheshimiwa anapungua uwezo wake wa kujatambua kwamba pale alipoapa kuwa ni rais wa Tanganyika alikoma kuwa bilateral, washauri wake pia wamelala usingizi wa pono! Ongea na wananchi wako mzee KK, siyo wapiga kura wako, uchaguzi uliisha na ulikubali na kuapa kuiongoza nchi bila ubaguzi, sasa iwaje unawaambia Wazee, tena wa CCM tena wa Mkoa ofcourse JK mkuu Nyerere alitumia hilo jukwaa kwa sababu hakukuwa na vyama vingi naye alikosea kwa sababu alisahau kwamba wazee wapo nchi nzima hii!
   
 10. PROF. ENG

  PROF. ENG Senior Member

  #10
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM = Chama Cha Mazee!!.
   
 11. p

  plawala JF-Expert Member

  #11
  Nov 19, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na hawakuenda bure,walipewa posho kidogo,na kupewa maelekezo kwamba kila akiongea JK anagalau washangilie
   
 12. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #12
  Nov 19, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  JK ni mtu wa kudesa wala hajishughulishi kufikiri. Eti kwa sababu aliona Nyerere akifanya hivyo basi anafikiri hiyo ni dogma anacopy paste tu bila kujua kua muda na majira yamebadilika tangu Nyerere aondoke madarakani
   
 13. m

  mwinukai JF-Expert Member

  #13
  Nov 19, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 1,448
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  huyu jamaa nakumbuka aliwahi kushangiliwa sana mwaka jana wakati akisema HATAKI KURA ZA WALIMU,anyway anakwenda kwa watu wanaozungumza fikra moja.
   
 14. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #14
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135

  Masahihisho: wale sio wazee wa DSM bali ni wazee wa CCM wa mkoa wa dar es salaam ndio maana walikuwa wakisalimiana kwa salamu ya ccm oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
   
 15. Litvinienko

  Litvinienko JF-Expert Member

  #15
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kichwa cha JK kina kasoro za kuzaliwa.
   
 16. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #16
  Nov 19, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Jana nilitaka kupost thread kama hii ila kwa mtazamo tofauti kidogo. Kwakuwa umeileta, nitaongezea maana hatutofautiani sana. Nina maswali machache yakuongezea

  Hivi wanawapataje hao wazee? Tunapowaita wazee wa Dar, tunawapataje? Dar yenye wakazi karibu 5mil, hao ndio wazee wa Dsm? Nini kigezo cha kuwaalika kwenye mkutano wa rais? Nani anawaalika?

  Hao wazee ni kweli wanawakilisha wakazi wa dar? Are they truly representing or the true color for dsm elders. Au wanaaiaisha wenzao?

  Kwa hoja alizokuwa nazo rais, ilikuwa sahihi kuzungumza na wazee? Ilikuwa sahihi kweli kuzungumza na taifa kupitia "wazee wa dsm" kwa hoja alizokuwa nazo. Ujumbe umefika kwa njia sahihi? Yaani, rais amefanikiwa kuufikisha ujumbe wake kwa njia ya kuzungumza na wazee wale?

  Utaratibu wa rais kuzungumza na taifa kupitia kundi moja tu la jamii kwa kila anapotaka kuzungumza ni sahihi? Kuna wakati anatakiwa kuzungumza na makundi mengine pia anapolihutubia taifa kulingana na hoja alizonazo?

  Vipi kuhusu wazee wa maeneo mengine ya nchi? Au ni wazee wa Ddm na Dsm tu? Hao wazee wamaeneo mengine wanajisikiaje?

  Naomba kuwasilisha.

  ..
   
 17. nzitunga

  nzitunga Senior Member

  #17
  Nov 19, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Posti hii ingesomeka "WAZEE WA CCM DAR NA JK"
  Kwa sababu wale walikuwa ni wazee wa CCM, na alikwenda kuchat nao tu
   
 18. KANYIMBI

  KANYIMBI JF-Expert Member

  #18
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 311
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Bora aliongea na makada wazee wa chama cha jembe na nyundo, maana vijana wa kizazi kipya hamkawii kuzomea wakubwa. ndio sababu hamkualikwa
   
 19. P

  Paul J Senior Member

  #19
  Nov 19, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Usanii mtupu! Wazee wenyewe uliwaona? Kimsingi aliuthibitishia umma wa watanzania kuwa ccm imeteka mchakato mzima wa katiba na ndo maana ujumbe kaufikisha kwa kupitia makada wazee wa ccm!Mada aliyoiongelea pale: Uchumi na Katiba si la wazee wa dsm ni swala la kitaifa.
   
 20. msweken

  msweken Senior Member

  #20
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 191
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Kama kweli JK anawapenda wazee awaweke chini wazee wa iliyokua jumuia ya East Afrika, kisha atoe upupu wake mbele yao.
   
Loading...