Wazee wa CCM (Shinyanga) wamshukia Dk Slaa

Wazee wa CCM (Shinyanga) wamshukia Dk Slaa

Nashindwa kuelewa hawa wazee walikuwa wanasema nini na kukemea nini?
  1. Wanampongeza Kikwete kwa kukemea upandaji holela wa bei: Ikiwa Kikwete atakemea kama wapinzani wanavyofanya (ambao hawana serikali), nani atadhibiti. Au vyombo vya dola ni kukamata na kupiga mabomu maandamano ya wapinzani tu? Alitakiwa atuambie hatua gani za wanachukua.
  2. Wanasema serikali haina budi kuchukua hatua za makusudi ili bei za vyakula na bidhaa nyingine muhimu nchini zishuke: Sasa CDM wanasema nini na wao wanasema nini? Au na hayo yalikuwa maandamano ya CDM chini ya mwavuli wa wazee wa CCM?
  3. Tena wanasema, "Tunahitaji kuwa na umeme wa uhakika kwa kuwa ndiyo msingi wa uchumi wetu,”: Kwanza hiyo pia ndio ajenda mojawapo ya maandamano ya CDM. Mbili, Tutatapataje umeme wa uhakika na serikali yao ndio inawakumbatia Dowans? Wazee mmeliwa na CCM yenu.
Kweli CCM wamechanganyikiwa. Wanataka kuonekana wako loyal kwa chama na wakati huohuo wanalalama.
VIVA CDM! VIVA Harakati za ukombozi! VIVA Maandamano ya Ukombozi.
Yaani kwa kweli umenichekesha ahsante kwa ujumbe mzuri kweli wana CCM hawaelewi hata waunge mkono kitu gani cha mwenyekiti wao jamani kuchanganyikiwa huku mapema namna hii huko mbele baada ya mzunguko wa nchi nzima si ndio itakuwa ngoma
 
Wazee walimshangilia Mwinyi kwa kuanzisha kuchangia elimu ya juu, sasa wanashindwa kusomesha watoto wao. Hawa wazee balaa sana kuwamo humu nchini!
 
Ningeshangaa kama lingekuwa tamko la vijana wa mkoa wa Shinyanga, lakini kama ni wazee hilo halininyimi usingizi, kwani ninavyojua mimi walioiadhibu CCM mkoani Shinyanga ni vijana na si wazee.Watu muhimu kwa sasa ni vijana na ndiyo DECIDING FACTOR kwa hatma ya Tanzania.

Wazee kwiishineeeeeeeee kanzi.Wazee kwa sasa hawana tija maana hao ndiyo wanachelewesha mabadiliko ya kweli, However, kwa mkoa wa Shinyanga Wazee hawakiungi mkono Chama Cha Majambazi(ccm).

Huu ni uongo wa Taahira Mgeja
 
Yaani kwa kweli umenichekesha ahsante kwa ujumbe mzuri kweli wana CCM hawaelewi hata waunge mkono kitu gani cha mwenyekiti wao jamani kuchanganyikiwa huku mapema namna hii huko mbele baada ya mzunguko wa nchi nzima si ndio itakuwa ngoma

Asante Mkuu! Hiyo ndiyo shida ya kulelewa kwenye zidumu fikra za mwenyekiti
 
Huyu Slaa ni kasisi aliyeasi kama alivyo Ibirisi.

Hivyo lazima watu wawe makini nae sana huyo. Ahsante wazee kuliona hilo.

Haya ni majungu tu ya spin doctors wa ccm waliokalia key board na kubuni hilo baraza la wazee wa ccm hapo shinyanga!

Inashsngaza kuwa hakuna hata mjumbe mmoja wa hilo baraza aliyetambulishwa kwa jina kama ndio msemaji wao; huu wote ni uzushi wa propaganda za ccm kwani wazee wa Shinyanga hawawezi kuunga mkono serikali isiyowajali wao na wananchi wenzao!
 
Huyu Slaa ni kasisi aliyeasi kama alivyo Ibirisi.

Hivyo lazima watu wawe makini nae sana huyo. Ahsante wazee kuliona hilo.

kama huelewi habari za kanisa ni bora ukae kimya, kuliko kuonyesha ujinga wako" ukiitaji zaidi ufafanuzi ucogope niulize nikueleze kidogo kuhusu laisaition in the catholic church.
 
Monday, 14 March 2011 06:38

Na Anthony Komanya, Shinyanga
BARAZA la Wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shinyanga Mjini, limemshukia Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibroad Slaa kwa kwa madia kuwa anaudanganya umma wa Watanzania. Pia, limesema hatua yake ya kumzushia kifo mbele ya mkutano wa hadhara Mkuu wa mkoa Shinyanga, Dk. Yohana Balele, ilikuwa na lengo la kuwachanganya na kuwadhoofisha wananchi.
dk.%20willibrod%20slaa.jpg

Baraza hilo la wazee limesema siasa za kuwazushia vifo viongozi wanaohehishimika mbele ya jamii, zimepitwa na wakati na kwamba, ni sawa na siasa za majitaka.
“Tunalaani uzushi wa Dk. Slaa wa kudai kuwa Dk. Balele amefariki wakati siyo kweli, Chadema na viongozi wake wafanye siasa safi na waache siasa chafu,” lilisema tamko la wazee hao.
Mbali na kumshukia Dk. Slaa, Baraza hilo pia limempongeza rais Jakaya Kikwete kwa kukemea upandaji holela wa bei za vyakula nchini.
Aidha, limeunga mkono uamuzi wa serikali wa kufuta kodi ya sukari inayotoka nje ya nchi ili kuhakikisha bei inashuka na kutoa nafuu kwa watumiaji.
Pongezi hizo zilitolewa juzi ikiwa ni sehemu ya tamko la kuwapongeza wagombea wa CCM mkoani hapa, waliopata ushindi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Baraza la wazee hao lilisema serikali haina budi kuchukua hatua za makusudi ili bei za vyakula na bidhaa nyingine muhimu nchini zishuke.
Lilisema kushuka kwa bidhaa hizo kutatoa ahueni kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa na uzalishaji mali, tofauti na ilivyo sasa ambapo maisha yameonekana kupanda na kuwafanya watu kutumia muda mwingi kutafuta njia mbadala za kuishi.
Pia, limeshauri serikali kumaliza tatizo la mgawo wa umeme unaoendelea katika maeneo mbalimbali nchini.
“Tunahitaji kuwa na umeme wa uhakika kwa kuwa ndiyo msingi wa uchumi wetu,” walisema wazee hao.

hawa wazee wako sawa kabisaaaaa
 
Kwetu AMANI ni muhimu kuliko lolote lile. Chukulia mfano mdogo tu wa Gongola mboto wakati wa mabomu unaona watu walivyotaharuki.

Sote tuombe Amani itawale nchini na tuzishinde nguvu za shetani kutaka kumwaga damu nchini.

kweli ccm ni ccm" mifano yote ya amani duniani unaangukia gongola mbote. Ps ule ni uzembe na msitututie hasira, kuuwa muuwe ninyi kwa malengo yenu, halaf nasumbua wananchi kupeka misaada na nyie hakuna chochote mlilofanya zaidi ya kuuza sura 2.
 
Kama mtu yupo lakini hana faida yoyote ni sawa na mfu, ata mimi nasema Balele kafa! kama hajafa mbona Wazee ndio wanamsemea? mbona halishindwa kuleta haki katika chaguzi za Mkoa wa Shinyanga?

kama yupo watwambie kafanya nini kama mkuu wa mkoa tokea mwaka jana? au yupo tu Ofisini kunywa chai! huyu si kama mfu tu! yaani mfu kisiasa.
 
Monday, 14 March 2011 06:38

Na Anthony Komanya, Shinyanga
BARAZA la Wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shinyanga Mjini, limemshukia Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibroad Slaa kwa kwa madia kuwa anaudanganya umma wa Watanzania. Pia, limesema hatua yake ya kumzushia kifo mbele ya mkutano wa hadhara Mkuu wa mkoa Shinyanga, Dk. Yohana Balele, ilikuwa na lengo la kuwachanganya na kuwadhoofisha wananchi.
dk.%20willibrod%20slaa.jpg

Baraza hilo la wazee limesema siasa za kuwazushia vifo viongozi wanaohehishimika mbele ya jamii, zimepitwa na wakati na kwamba, ni sawa na siasa za majitaka.
Tunalaani uzushi wa Dk. Slaa wa kudai kuwa Dk. Balele amefariki wakati siyo kweli, Chadema na viongozi wake wafanye siasa safi na waache siasa chafu, lilisema tamko la wazee hao.
Mbali na kumshukia Dk. Slaa, Baraza hilo pia limempongeza rais Jakaya Kikwete kwa kukemea upandaji holela wa bei za vyakula nchini.
Aidha, limeunga mkono uamuzi wa serikali wa kufuta kodi ya sukari inayotoka nje ya nchi ili kuhakikisha bei inashuka na kutoa nafuu kwa watumiaji.
Pongezi hizo zilitolewa juzi ikiwa ni sehemu ya tamko la kuwapongeza wagombea wa CCM mkoani hapa, waliopata ushindi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Baraza la wazee hao lilisema serikali haina budi kuchukua hatua za makusudi ili bei za vyakula na bidhaa nyingine muhimu nchini zishuke.
Lilisema kushuka kwa bidhaa hizo kutatoa ahueni kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa na uzalishaji mali, tofauti na ilivyo sasa ambapo maisha yameonekana kupanda na kuwafanya watu kutumia muda mwingi kutafuta njia mbadala za kuishi.
Pia, limeshauri serikali kumaliza tatizo la mgawo wa umeme unaoendelea katika maeneo mbalimbali nchini.
Tunahitaji kuwa na umeme wa uhakika kwa kuwa ndiyo msingi wa uchumi wetu, walisema wazee hao.
Nasikitika kuamini kama haw wazee wa shinyanga wanahekima.kwa waliosikia taarifa ama warudie clip aliyozungumza Dr Slaa wazingekuja na kauli kama hiyo kwani hazina hekima hata chembe.labda tu niseme hata mimi nilipokea taarifa toka kwa mtu wa karibu sana na familia juu ya kifo hicho..sasa nani mwenye makosa.
 
Chuki Binafsi hazina nafasi, wewe nakushauri usichukuliwe na sera za udini, acha, nafikiri watoto wako pia wanasoma shule hizi ambazo hazina madawati, vitabu,chaki,walimu, vyoo bora na hata majengo bora ya kusomea.

Wanae wako arabuni huko kwani wanajua shida? achana na huyu dini imemkolea mdomoni!
 
BARAZA la Wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shinyanga Mjini, limemshukia Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibroad Slaa kwa madai kuwa anaudanganya umma wa Watanzania. Pia, limesema hatua yake ya kumzushia kifo mbele ya mkutano wa hadhara Mkuu wa mkoa Shinyanga, Dk. Yohana Balele, ilikuwa na lengo la kuwachanganya na kuwadhoofisha wananchi.

Baraza hilo la wazee limesema siasa za kuwazushia vifo viongozi wanaohehishimika mbele ya jamii, zimepitwa na wakati na kwamba, ni sawa na siasa za majitaka.

"Tunalaani uzushi wa Dk. Slaa wa kudai kuwa Dk. Balele amefariki wakati siyo kweli, Chadema na viongozi wake wafanye siasa safi na waache siasa chafu," lilisema tamko la wazee hao.

Mbali na kumshukia Dk. Slaa, Baraza hilo pia limempongeza rais Jakaya Kikwete kwa kukemea upandaji holela wa bei za vyakula nchini.

Aidha, limeunga mkono uamuzi wa serikali wa kufuta kodi ya sukari inayotoka nje ya nchi ili kuhakikisha bei inashuka na kutoa nafuu kwa watumiaji.

Pongezi hizo zilitolewa juzi ikiwa ni sehemu ya tamko la kuwapongeza wagombea wa CCM mkoani hapa, waliopata ushindi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Baraza la wazee hao lilisema serikali haina budi kuchukua hatua za makusudi ili bei za vyakula na bidhaa nyingine muhimu nchini zishuke.

Lilisema kushuka kwa bidhaa hizo kutatoa ahueni kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa na uzalishaji mali, tofauti na ilivyo sasa ambapo maisha yameonekana kupanda na kuwafanya watu kutumia muda mwingi kutafuta njia mbadala za kuishi.
Pia, limeshauri serikali kumaliza tatizo la mgawo wa umeme unaoendelea katika maeneo mbalimbali nchini.

"Tunahitaji kuwa na umeme wa uhakika kwa kuwa ndiyo msingi wa uchumi wetu," walisema wazee hao.
 
Hivi ni kweli PHD holder alimzushia kifo Brig.gen.(Rtd)Balele?
 
Inabidi slaa anyoshe maelezo kuhusu suala la uzushi wa kifo cha R.C Balele na kuiondoa serikali kwa mtindo wa Tunisia,Misri n.k hii ni muhimu ili kulinda reputation ya chama.
 
Nadhani wanapigania Mslahi yao kama CCM ikiondoka Madarakani sasa hivi wazee wengi wa chama hawatanufaika wao na familia zao; iliandikwa magazetini kuwa huyu Balele ni mgojwa na alikuwa anatibiwa Mwanza ambako Mkewe anaishi.

Hizi zinaonekana ni fitina za kibinafsi

Kuondoka kwenye uongozi wa kidini sio sababu kuwa utakuwa ibilisi
 
Huyu Slaa ni kasisi aliyeasi kama alivyo Ibirisi.

Hivyo lazima watu wawe makini nae sana huyo. Ahsante wazee kuliona hilo.

Wewe mtu ni Mdini sana. Halafu hata kiswahili hujui...Hii kuita watu ibilisi ni dhihaka kubwa. Hata kama hukubaliani na mtu suluhisho sio matusi na dhihaka. Tatizo lenu mna midomo michafu sana, ila nyie mkiguswa tu hamkawii kutangaza jihad.
 
Nadhani wanapigania Mslahi yao kama CCM ikiondoka Madarakani sasa hivi wazee wengi wa chama hawatanufaika wao na familia zao; iliandikwa magazetini kuwa huyu Balele ni mgojwa na alikuwa anatibiwa Mwanza ambako Mkewe anaishi.

Hizi zinaonekana ni fitina za kibinafsi

Kuondoka kwenye uongozi wa kidini sio sababu kuwa utakuwa ibilisi

kwa nini isiwe lazima,mtu anazushia watu wamekufa we unamchukuliaje?
 
Mropokaji ni mropokaji tu finisha hakuna vile utasema tuamini vingine ,eti maandamano yameshusha sukari,mambo gani tunadanganyana ashushe ciment iwe afu tano nitamkubali
 
Back
Top Bottom