Wazee wa CCM (Shinyanga) wamshukia Dk Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazee wa CCM (Shinyanga) wamshukia Dk Slaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 14, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  14 March 2011

  BARAZA la Wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shinyanga Mjini, limemshukia Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibroad Slaa kwa madai kuwa anaudanganya umma wa Watanzania.

  Pia, limesema hatua yake ya kumzushia kifo mbele ya mkutano wa hadhara Mkuu wa mkoa Shinyanga, Dk. Yohana Balele, ilikuwa na lengo la kuwachanganya na kuwadhoofisha wananchi.

  Baraza hilo la wazee limesema siasa za kuwazushia vifo viongozi wanaohehishimika mbele ya jamii, zimepitwa na wakati na kwamba, ni sawa na siasa za majitaka.


  "Tunalaani uzushi wa Dk. Slaa wa kudai kuwa Dk. Balele amefariki wakati siyo kweli, Chadema na viongozi wake wafanye siasa safi na waache siasa chafu," lilisema tamko la wazee hao.

  Mbali na kumshukia Dk. Slaa, Baraza hilo pia limempongeza rais Jakaya Kikwete kwa kukemea upandaji holela wa bei za vyakula nchini.

  Aidha, limeunga mkono uamuzi wa serikali wa kufuta kodi ya sukari inayotoka nje ya nchi ili kuhakikisha bei inashuka na kutoa nafuu kwa watumiaji.

  Pongezi hizo zilitolewa juzi ikiwa ni sehemu ya tamko la kuwapongeza wagombea wa CCM mkoani hapa, waliopata ushindi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

  Baraza la wazee hao lilisema serikali haina budi kuchukua hatua za makusudi ili bei za vyakula na bidhaa nyingine muhimu nchini zishuke.

  Lilisema kushuka kwa bidhaa hizo kutatoa ahueni kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa na uzalishaji mali, tofauti na ilivyo sasa ambapo maisha yameonekana kupanda na kuwafanya watu kutumia muda mwingi kutafuta njia mbadala za kuishi.

  Pia, limeshauri serikali kumaliza tatizo la mgawo wa umeme unaoendelea katika maeneo mbalimbali nchini.

  "Tunahitaji kuwa na umeme wa uhakika kwa kuwa ndiyo msingi wa uchumi wetu," walisema wazee hao.
   
 2. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Nashindwa kuelewa hawa wazee walikuwa wanasema nini na kukemea nini?
  1. Wanampongeza Kikwete kwa kukemea upandaji holela wa bei: Ikiwa Kikwete atakemea kama wapinzani wanavyofanya (ambao hawana serikali), nani atadhibiti. Au vyombo vya dola ni kukamata na kupiga mabomu maandamano ya wapinzani tu? Alitakiwa atuambie hatua gani za wanachukua.
  2. Wanasema serikali haina budi kuchukua hatua za makusudi ili bei za vyakula na bidhaa nyingine muhimu nchini zishuke: Sasa CDM wanasema nini na wao wanasema nini? Au na hayo yalikuwa maandamano ya CDM chini ya mwavuli wa wazee wa CCM?
  3. Tena wanasema, "Tunahitaji kuwa na umeme wa uhakika kwa kuwa ndiyo msingi wa uchumi wetu,": Kwanza hiyo pia ndio ajenda mojawapo ya maandamano ya CDM. Mbili, Tutatapataje umeme wa uhakika na serikali yao ndio inawakumbatia Dowans? Wazee mmeliwa na CCM yenu.
  Kweli CCM wamechanganyikiwa. Wanataka kuonekana wako loyal kwa chama na wakati huohuo wanalalama.
  VIVA CDM! VIVA Harakati za ukombozi! VIVA Maandamano ya Ukombozi.
   
 3. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huyu Slaa ni kasisi aliyeasi kama alivyo Ibirisi.

  Hivyo lazima watu wawe makini nae sana huyo. Ahsante wazee kuliona hilo.
   
 4. J

  Joblube JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Upumbavu mtu huzaliwa nao kama huu
   
 5. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tena ananguvu kubwa za kishetani huyo.

  Ashindwe na alegee.

  Hongera wazee wa Shinyanga. Wabeja saana
   
 6. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  ningependa kupata profiles za hao wanaojiita wazee wa shinyanga kabla ya ku-comment kitu cho chote!
   
 7. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Acha kuandika kwa font kubwa na kugandamiza..kizuri chajiuza..
   
 8. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Wameshapata madai yao ya kustaafu? waache walale hao hawana ticha kwa taifa letu!
   
 9. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,839
  Likes Received: 11,957
  Trophy Points: 280
  Hata nyani wana wazee wao kwa hiyo sishangai nasikia Wassira pia alikuwepo.
   
 10. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #10
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Chuki Binafsi hazina nafasi, wewe nakushauri usichukuliwe na sera za udini, acha, nafikiri watoto wako pia wanasoma shule hizi ambazo hazina madawati, vitabu,chaki,walimu, vyoo bora na hata majengo bora ya kusomea.
   
 11. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #11
  Mar 14, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,046
  Likes Received: 13,259
  Trophy Points: 280

  madai ya kustaafu! kwani waliwahi kuajiliwa wapi? wote ni vizee vya kijiweni vilivyopewa buku tano tano kwenda kuongea upupu.
   
 12. L

  Liberal man Member

  #12
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata Gadhafi ana wafuasi wake, kwa hiyo sishangai hawa wazee ccm wanajua sana ku-brain wash
   
 13. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #13
  Mar 14, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,839
  Likes Received: 11,957
  Trophy Points: 280
  Hawa hapa bdo wanasubiri mafao

  [​IMG]
   
 14. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #14
  Mar 14, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  hawa wazee muda wao umepita, hawana jipya.
   
 15. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #15
  Mar 14, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwetu AMANI ni muhimu kuliko lolote lile. Chukulia mfano mdogo tu wa Gongola mboto wakati wa mabomu unaona watu walivyotaharuki.

  Sote tuombe Amani itawale nchini na tuzishinde nguvu za shetani kutaka kumwaga damu nchini.
   
 16. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #16
  Mar 14, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Toka lini Mgeja akawa .....Wazee wa Shinyanga? kuweni waangalifu na propaganda za CCM
   
 17. msafiri.razaro

  msafiri.razaro JF-Expert Member

  #17
  Mar 14, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 616
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Hizi Ndio busara za wazee wa kwetu kweli?
   
 18. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #18
  Mar 14, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,046
  Likes Received: 13,259
  Trophy Points: 280

  Unaposema kwetu unamuwakilisha nani? Kwa taarifa yako Tanzania kuna utulivu tu hakuna amani, watu wenye njaa na waliokata tamaa unapowaeleza habari ya amani unachekesha sana. na watu kama nyinyi lazima ujuwe tu ipo siku utakufa tu, na utakwenda kujibu mbele ya muumba wako, hii kazi ya kichangudoa unayoifanya hapa kuusaliti umma.
   
 19. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #19
  Mar 14, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  hayo nenda kaongelee msiikitini!
   
 20. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #20
  Mar 14, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Mbogo31,
  Thanks, mweleweshe pole pole atakapojua ukweli na kuongoka atakuwa mkali kwa maovu kuliko sisi.
   
Loading...