Wazee mpo hii yenu

Wazee mpo hii yenu

stelita

Member
Joined
Nov 26, 2014
Posts
9
Reaction score
1
Kuna Mbongo kaniomba nimsaidie kupost hii maana yeye akaunti inagoma kufunguka kasahau nenosiri....nawaomba chonde usitume PM kwangu kwani haitosaidia wala sitazijibu badala yake wewe tangaza nia hapa kwenye post atakupm yeye mwenyewe akipenda.

NAMNUKUU....
Mimi sifa zangu ni kama ifuatavyo:
Umri:- miaka 45
Hali ya ndoa: niliachika kwa talaka
Watoto: Ninao watano wote wapo shuleni.
Kipato changu ni bora mkono uende kinywani kwa kazi ya kuajiriwa.
Jinsia ni mwanamke
Elimu ni ya chuo-baada ya sekondari
Dini ni mkristo.
Afya njema kabisa na nimejitunza vizuri.

Ninatafuta mume mtarajiwa kwa sifa hizi au zinazoendana:

Mwanaume mtalaka,mfiwa au mchelewaji tu.
Miaka 48 hadi 58 ndo uwe umri wake.
Mwenye elimu ya juu au awe na upeo na mtazamo chanya.

mwenye afya njema.

Mwenye shughuli halali za kujikimu kimaisha.

Mkristo mcha Mungu wa kweli au mwislamu wa rasharasha asiwe na msimamo mkali.

Pombe sigara hapana

Mwenye heshima katika jamii yaani anayeheshimika.

Anayehitaji mke.

Mtanzania nibora zaidi japo mwafrika yeyote anaweza akafaa.

mawasiliano ni 123456789@gmail.com au hapa kwa stelita. asanteni.
MWISHO WA KUNUKUU....


Ama kweli watu hawakati tamaa umphu!!

nakuombea upate mama wewe 123456789!
 
Last edited by a moderator:
Mbona hueleweki,umesema akaunti imegoma kufunguka,amesahau neno la siri akakuomba umpostie,alafu unasema usitumiwe pm maana hutojibu ila atampm mtu atakae tangaza nia mwenyewe,je atakua amekumbuka neno la siri?kama ndio hvyo kwa nini asingepost mwenyewe?.

Kua wazi kama unataka mume na sio kusingizia kua umeombwa.
 
Mbona hueleweki,umesema akaunti imegoma kufunguka,amesahau neno la siri akakuomba umpostie,alafu unasema usitumiwe pm maana hutojibu ila atampm mtu atakae tangaza nia mwenyewe,je atakua amekumbuka neno la siri?kama ndio hvyo kwa nini asingepost mwenyewe?.

Kua wazi kama unataka mume na sio kusingizia kua umeombwa.

Ama kweli kichwa ndio mtu, mwili kiwiliwili tu.
 
jamani wale wachache waliomtumia email anashukuru. tayari anawasiliana na mmoja wao wakipatana itakuwa imetosha....
 
Back
Top Bottom