Raimundo
JF-Expert Member
- May 23, 2009
- 13,415
- 12,628
Mtoto anaishi jinsi utakavyo mzazi...ukitaka awe mkorofi atajijengea hiyo hali na ukitaka awe mpole ni sawa pia. Mtoto anacheza na akili za wazazi ili kujua yupi mkali na yupi mpole kwa kufanya kosa dogo lisilohitaji adhabu ila akawapima kujua mtarespond vp...Mfano mtoto anaweza kusonya/kuonyesha kiburi au kulia bila sababu kisha anawapima nyie wazazi kujua misimamo yenu kwa kosa analofanya...Hapa mzazi unatakiwa uonyeshe kutopendezwa na alichokifanya na kumwonya kwa upendo wa hali ya juu, kama atarudia tena onyesha hali ya ukali tofauti na mara ya kwanza na mwisho akirudia tena ktk siku au muda huo huo basi unamwadhibu kwa kumkumbusha kosa lake na jinsi ulivyomwonya na hakusikia...hata kama mtoto hawezi kuzungumza ila anaelewa yote unayomwambia. Usimwadhibu mtoto zaidi ya mara 1 kwa siku kwani itamjengea usugu na hapo utapoteza zaidi. Ni mhm mzazi kuonyesha kumpenda mtoto kwa matendo na maneno yako kwani watoto tangu wachanga wanapata hisia za upendo wa mzazi hivyo kama humuonyeshi mapenzi ya dhati ataanza kujenga uadui na kukuchukulia wewe ni mtu hatari kwa ustawi wa maisha yake.
Usikubali hata siku moja mtoto akawa ndie mlezi wa familia, hapa namaanisha ana uwezo wa kulia hadi apewe soda/pipi au chochote kwani hili litamfanya mtoto kushindwa kutambua nafasi ya mzazi katika kufanya maamuzi na mwisho kuwa baba/mama asiye na maadili hapo baadae. Kuna familia moja nilienda mzazi anamsifia mtoto kwa kujua kucheza kiduku na kila mgeni akifika mtoto anashabikia kila linaloongewa na kuwa mstari wa mbele kushauri hata kipikwe chakula gani na kero zaidi habanduki hapo mlipo japo kuna HG....Ukiona hivi mzazi jitafakari mara mbili na uombe ushauri kwa wazazi wenzio hata kama umeshalea watoto 10 ila ujuzi wako hauna tija.
Mwisho japo tunawapenda sana watoto wetu ila malezi bora ndio kipimo pekee cha upendo tulio nao kwa watoto wetu. Tuwalee watoto kama watoto na sio watoto kama roho/mioyo yetu.
Nime - like (kitufe cha like sikioni kwenye PC yangu).