Lisa
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 1,549
- 1,075
Habari zenu wana MMU
Kutokana na maisha tunayoishi na watoto wetu, inatakiwa kupunguza ukali kidogo kwao maana wanakuwa wakiishi kwa wasiwasi pale wafanyapo kosa, au kuharibu kitu ndani ya nyumba, sikatai kuwa kumfundisha mtoto si vibaya lakini tupunguze kidogo ukali.
Nina maana gani mtoto akikosea kidogo, mzazi unamchapa au kumfokea kiasi ambacho anakuwa na wasiwasi, inafika sehemu, unamnunulia kitu cha kuchezea anakuwa anaogopa kukichezea maana akiharibu atachapwa, so unakuta amekiweka ukimuuliza kwa nn huchezei anakwambia naogopa nikiharibu dady atanichapa, hii inaweza kupelekea mtoto kutoweza kuwaza zaidi , na unakuwa unamkatisha fikra zake, za kuweza kuwaza zaidi.
jana nilipata aibu ya mwaka, alikuja mgeni home, dada akamkaribisha juice, bahati mbaya mgeni akavunja glass, basi mtoto wangu wa pili , ni mvulana akaanza kumwambia mgeni " enheeeeeeeeee leooooooooooo, ngoja baba arudi utakoma umevunja glass, shauri lako. akaanza kumwita dada yake, "Dadaaaaa njoo uone Uncle kavunja glass si ungemwekea kwenye kikombe cha plastiki hapo tungefuta tu wala wasingejua kama umemwaga juice"Basi bwana mgeni akakaa, tukafika home, ile tunaingia tu, mtoto akaaanza kumwambia mgeni, muombe kabisa msamaha, nikabaki nashangaa, nikamuuliza kuna nini akadaikia kavunja glass, mimi namwambia aombe kabisa msamaha ili baba asimchape"
niliona aibu, ikanibidi nijichekeshe na kuanza kumuelimisha kuwa wakubwa hawachapwi, lakini hapo alishakwenda chumbani kuchukua mkanda ili amletee baba yake.
SO PLEASE WAZAZI WENZANGU TUPUNGUZE UKALI KWA WATOTO WETU.