Wazazi wawasaidie watoto wao wa kike kupata wachumba (mume)

Maleven

JF-Expert Member
Sep 8, 2019
624
2,772
Nadhan moja majukumu ya wazazi yanayoendelea kupotea ni wazazi kuwatafutia watotot wao wachumba wa kuoa au kuwaoa, binafsi nadhan utaratibu huu urudishwe tena upewe nguvu zaidi hasa kwa watoto wa kike.

Mtu yoyote anaefanya kazi katika ofisi alioko msichana kuanzia miaka 24 na kuendelea na hajaolewa atakwambia au anajua ni jinsi gani msichana huyo yuko desperate, amesoma, ana kazi, na pengine amepanga nyumba, lakini ikifika usiku kitanda kinakua kikubwa maana hawezi kukabiliana na lonliness, anatamani awepo mtu pembeni yake.

Hali hii inawatesa sana na inafanya wahangaike huku wakiweka mitego mbali mbali wengine huangukia hata kwa waume za watu. Singungumzii wale wadada wachache walioamua kutumia miili yao vibaya, nazungumzia wadada wa kawaida wanaojiheshimu ila maumbile yanakua wameshawazidi nguvu.

Ni muda sasa wazazi wachukue jukumu la kuwatafutia watoto wao wenza wa kuishi nao na kuunganisha familia, pia wanapowasomesha wasiwaambie wasome ile wawe na hela ili wanaume wasiwasumbue ila wawasomeshe ili waje kuwasaidia wanaume zao katika majukumu ya kifamilia pale mwanaume anapokwama
 
Duh! Hii Hali ya kuwaongelea kina Dada juu ya swala la Ndoa sijui kwann limeshika Kasi sana Ila mi nnavyoelewa isingekua social perspective kuchangia kwa kiasi kikubwa kumbana mwanamke na ndoa au watoto sidhani Kama wangekua wanahangaika hata na Sisi wanaume.. Wanaume baadhi tuache insecurities, hautaweza kupendwa na wadada wote.. sio kila utakae mtongoza Ni lazima akukubalie.. mnawaonea tu Mabinti zetu zaeni wa kwenu muone uchungu..
Ulimwengu mpya utaanza na mwanamke.. lakini zaidi unaanzishwa na Jinsi Mwanaume atakavyombadili Mwanamke.. Ni sawa na kusafisha dodoki ili likusafishe mwilini.. tukiwajenga vizuri na kuishi nao kwa upendo Hawa watu sio wabaya kiivyo..
 
Hali mbayaaa
20200926_225655.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa kuona hii insecurities za baadhi ya wanaume wasiojiamini na kuja kulia Lia humu kisa wamekataliwa
 
Yaani mambo yamekua hovyo sana, hadi hufikia wengine kuingia kwenye mahusiano bila kujijua Dini zao

Na ukute wanapeana mpaka Mimba hawajuani Dini zao

Yaani vijana wanachukulia rahisi rahisi sana haya mahusiano.
 
Back
Top Bottom