Bawabu wa pili
Senior Member
- Nov 14, 2025
- 147
- 432
Wazazi na Walezi wa Manispaa ya Mtwara–Mikindani mkoani Mtwara, wameiomba Serikali kuendeleza programu maalum ya kuwaweka kambi Wanafunzi wenye ufaulu wa mdogo ili kuongeza kiwango cha ufaulu.Ombi hilo limetolewa mara baada ya matokeo ya mtihani wa MOCK wa kidato cha nne ngazi ya Mkoa kuonyesha kuwa wanafunzi 107 wamepata daraja 0, hali iliyomfanya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Mwalimu Hassan Nyange, kuwaweka kambi wanafunzi hao kutoka Shule 9 za manispaa.
Akizungumza kwa niaba ya Wazazi wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza na kuwaaga wanafunzi waliokuwa kambini, Mwenyekiti wa Wazazi wa kambi hiyo, Joel William, ameiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kuifanya programu hiyo kuwa ya nchi nzima ili kuinua ufaulu wa Wanafunzi
Afisa Elimu wa Mkoa wa Mtwara, amesema historia ya ufaulu wa kidato cha nne mwaka 2024 ndiyo iliyoleta wazo la kuwaweka kambini wanafunzi 103, ambapo wanafunzi 61 walipata daraja 0, huku ufaulu wa daraja la 1 hadi la 4 ukiwa asilimia 97 katika Manispaa ya Mtwara–Mikindani.
Naye Afisa Tarafa wa Mtwara Mjini, Titho Cholobi, amesema kambi hiyo iliyoanzishwa na Mwalimu Nyange ilikuwa mpango wa dharura wenye lengo la kuokoa ufaulu, na amemuomba Mkurugenzi kuanzisha misingi madhubuti ili mfumo huo uendelee hata kama muanzilishi hayupo, na kila mtumishi aweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara–Mikindani, Mwalimu Hassan Nyange, amesema kupitia wanafunzi hao wanataka kuthibitisha kwa Wazazi na wadau kuwa hakuna Mwanafunzi asiyeweza kufaulu, bali tatizo ni ukosefu wa usimamizi na ufuatiliaji kutoka kwa baadhi ya Wazazi Ameitaka jamii kufuatilia mienendo ya Watoto kwani hatamvumilia Mzazi ambaye mtoto wake atakutwa na ujauzito.
Kutokana na changamoto ya upatikanaji wa fedha za kuendesha kambi hiyo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Mtwara, Wakili Richard Mwalingo, ameshauri uongozi wa manispaa kuangalia namna ya kutumia sehemu ya mfuko wa elimu katika uendeshajiAfisa Elimu Kata ya Mitengo Shakira Mkwazu amewaomba Wazazi na walezi kutochoka kuwaunga mkono Wanafunzi, ameomba viongozi wa juu kutafakari namna ya kuendeleza kambi hiyo kwa mwaka ujao.