Enock gabriel
JF-Expert Member
- Apr 26, 2021
- 348
- 312
Kama wazazi hawakuombi, ikiwa wewe ni mwanaume, usijaribu kuhonga hiyo pesa. Weka akiba kidogokidogo siku moja wasapraise kwa zawadi ambayo hawawezi kuikataa.Mimi ni mwanachuo, ninatoka familia ya kawaida sana. Ninapata mkopo, wazazi wangu wanaishi maisha ya kawaida sana. Kinachonisikitisha ni kuwaona wenzangu wakiombwa matumizi na wazazi wao, wakati mimi wazazi wangu mpaka uwatumie wewe, tena kwa kuwalazimisha wapokee, ni wana maisha ya kawaida ila hawajawahi niomba hata 100, jamani nishaurini, na mama ndio kabisa yaani!
KUHUSU WAO KUTOKUKUOMBAMimi ni mwanachuo, ninatoka familia ya kawaida sana. Ninapata mkopo, wazazi wangu wanaishi maisha ya kawaida sana. Kinachonisikitisha ni kuwaona wenzangu wakiombwa matumizi na wazazi wao, wakati mimi wazazi wangu mpaka uwatumie wewe, tena kwa kuwalazimisha wapokee, ni wana maisha ya kawaida ila hawajawahi niomba hata 100, jamani nishaurini, na mama ndio kabisa yaani!
Wazazi wanamuogopaje mtoto kisa ukali bro?Wewe sio lazima uombwe, wewe mwenyewe angalia ni vitu gani ungependa wazazi wako wawe navyo kwa wakati huu, vitu ambavyo unaweza kuwasaidia au pia unaweza kukaa nao kitako na kuwauliza ni kitu gani wanachohitaji kwa muda huo.
Kwa maana nyingine wafanye wawe huru kufunguka kwako, yawezekana wewe ulipokuwa mdogo labda ulikuwa na tabia ya ukali sana na wazazi bado wanakuogopa --- kama ni hivyo jaribu kujenga urafiki, ucheshi na upole kwao ili wajenge confidence wakiwa na wewe.
Ahsante kaka!Deni kubwa ninaliona kwako unalo ndugu yangu,wazazi wako bado hawaoni kama umefika hatua ya kuombwa
Unachotakiwa kufanya kwasasa ni soma kwa bidiii sana, jitahidi kila uwezavyo ukue kiuchumi ni kweli upo chuo
Wazazi hawakuombi kitu ila si kwamba hawana shida wanatamani kukuona hicho kidogo kinaongezeka sasa wewe
Kitu pekee unatakiwa fanya sasa hivi ni kuwaza namna yakuongeza hicho kidogo ulichokua unataka watumia wazazi
Kama huna ubongo wa biashara,basi save hizo hela zao kama ulikua unataka kila wiki uwatumie 50,000,kwakua hujawatumia
Hifadhi hiyo 50,000 mahali na utambue kuwa si Yako ni ya wazazi wako,ukipata tena amount unataka watumia,ihifadhi kule ulipoiweka ile nyingine.
Nenda kwa mtirirko huo ukimaliza Chuo tumia hela za wazazi wako (zile ulizokua ukiweka) kuanzisha kitu chako kisimamie kwabidiii usizembeee.
nakuhakikishia zawadi pekee utakayoweza wapa wazazi wako wakaipokea kwa mikono miwili huku wakitabasamu kwenye nyuso zao ni "mafanikio yako kiuchumi" hebu wape hiyo zawadi wazazi wako.
unaona umetoka familia ya aina gani,wazazi wako hawataki kuwa mzigo kwako wanataka usiwe kama wao kuna mengi behind the scen huyajui wana ji sacrifice kwa sababu yako,Hawataki nawewe uje upate mateso hayo utakapokua unawahudumia watoto wako.
Wanakupenda sana,wanakuwazia mema jitahidi kuchangamsha hiyo akili,elewa una deni kubwa kubwa kubwa mbele yako Kimbizana na Muda mafanikio yako uyapate angali wazazi wako wapo HAI waonje Zawadi waliyotamani ipata kwako.
Natamani unielewe au nikupe hii kichwa yangu uelewe nini namaanisha na nataka uwe vipi,naamini umenielewa japo kidogo.
Wazazi wanamuogopaje mtoto kisa ukali bro?
Daaah! Tufarijiane tu kaka.Mkuu Wazazi wangu walikuwa hivyo Yani hata Mia hawakuombi hata Kama wamelala na njaa.
Kwetu me ndo first born, baada ya kupata Kazi nikajichanga kurekebisha nyumba ya home and everything Yani nlifanya full renovations.
Sasa baba sijui akajua nalipwa millions Maana marekebisho yalikuwa ya gharama kidogo.
Saivi show naiona baba kila saa ananambia kuhusu kumlipia mdogo wangu ada sijui hostel na sio Kama Hana hela. Yani nikiona sim ya mdingi najua tu story za hela Hadi sometimes nakausha.
Tho mama Hadi Leo haniombi, Yani akiomba ujue shida imemshika kweli na hapo ataomba radhi kwa kukuomba.
Ma first born tunashida
Mzazi mwenye akili hawezi kumuomba hela mtoto anayefahamu kabisa kwamba anasoma na si mfanyakazi; Ungekuwa unasoma na kufanya kazi hapo pengine wangekuomba; Maana mkopo sio kwa ajili ya wewe kujikimu kwenye masomo na sio; Kama hawalipi ada nadhani hiyo ni support Tosha sana kwao.Jamani nishaurini na mama ndio kabisa yaani!