Wazazi wangu wanaishi maisha ya kawaida lakini hawaniombi chochote

Wewe sio lazima uombwe, wewe mwenyewe angalia ni vitu gani ungependa wazazi wako wawe navyo kwa wakati huu, vitu ambavyo unaweza kuwasaidia au pia unaweza kukaa nao kitako na kuwauliza ni kitu gani wanachohitaji kwa muda huo.

Kwa maana nyingine wafanye wawe huru kufunguka kwako, yawezekana wewe ulipokuwa mdogo labda ulikuwa na tabia ya ukali sana na wazazi bado wanakuogopa 🤣🤣--- kama ni hivyo jaribu kujenga urafiki, ucheshi na upole kwao ili wajenge confidence wakiwa na wewe.
 
Mimi ni mwanachuo, ninatoka familia ya kawaida sana. Ninapata mkopo, wazazi wangu wanaishi maisha ya kawaida sana. Kinachonisikitisha ni kuwaona wenzangu wakiombwa matumizi na wazazi wao, wakati mimi wazazi wangu mpaka uwatumie wewe, tena kwa kuwalazimisha wapokee, ni wana maisha ya kawaida ila hawajawahi niomba hata 100, jamani nishaurini, na mama ndio kabisa yaani!
Kama wazazi hawakuombi, ikiwa wewe ni mwanaume, usijaribu kuhonga hiyo pesa. Weka akiba kidogokidogo siku moja wasapraise kwa zawadi ambayo hawawezi kuikataa.
 
Deni kubwa ninaliona kwako unalo ndugu yangu,wazazi wako bado hawaoni kama umefika hatua ya kuombwa

Unachotakiwa kufanya kwasasa ni soma kwa bidiii sana, jitahidi kila uwezavyo ukue kiuchumi ni kweli upo chuo

Wazazi hawakuombi kitu ila si kwamba hawana shida wanatamani kukuona hicho kidogo kinaongezeka sasa wewe

Kitu pekee unatakiwa fanya sasa hivi ni kuwaza namna yakuongeza hicho kidogo ulichokua unataka watumia wazazi

Kama huna ubongo wa biashara,basi save hizo hela zao kama ulikua unataka kila wiki uwatumie 50,000,kwakua hujawatumia

Hifadhi hiyo 50,000 mahali na utambue kuwa si Yako ni ya wazazi wako,ukipata tena amount unataka watumia,ihifadhi kule ulipoiweka ile nyingine.

Nenda kwa mtirirko huo ukimaliza Chuo tumia hela za wazazi wako (zile ulizokua ukiweka) kuanzisha kitu chako kisimamie kwabidiii usizembeee.

nakuhakikishia zawadi pekee utakayoweza wapa wazazi wako wakaipokea kwa mikono miwili huku wakitabasamu kwenye nyuso zao ni "mafanikio yako kiuchumi" hebu wape hiyo zawadi wazazi wako.

unaona umetoka familia ya aina gani,wazazi wako hawataki kuwa mzigo kwako wanataka usiwe kama wao kuna mengi behind the scen huyajui wana ji sacrifice kwa sababu yako,Hawataki nawewe uje upate mateso hayo utakapokua unawahudumia watoto wako.

Wanakupenda sana,wanakuwazia mema jitahidi kuchangamsha hiyo akili,elewa una deni kubwa kubwa kubwa mbele yako Kimbizana na Muda mafanikio yako uyapate angali wazazi wako wapo HAI waonje Zawadi waliyotamani ipata kwako.

Natamani unielewe au nikupe hii kichwa yangu uelewe nini namaanisha na nataka uwe vipi,naamini umenielewa japo kidogo.
 
Mimi ni mwanachuo, ninatoka familia ya kawaida sana. Ninapata mkopo, wazazi wangu wanaishi maisha ya kawaida sana. Kinachonisikitisha ni kuwaona wenzangu wakiombwa matumizi na wazazi wao, wakati mimi wazazi wangu mpaka uwatumie wewe, tena kwa kuwalazimisha wapokee, ni wana maisha ya kawaida ila hawajawahi niomba hata 100, jamani nishaurini, na mama ndio kabisa yaani!
KUHUSU WAO KUTOKUKUOMBA
Kuna mambo mawili

1.pengine wanao uelewa kwamba bado haujafikia stage ya kuombwa na ni kweli hivyo wanakuacha.

Katika stage hii watoto wengi chuoni wakipata mkopo hawaaambii wazazi wao,wazazi hushangaa tu mbona kimya mtoto haombi pesa yeyote,nao wazazi wengine kwa kuogopa kuombwa hawaulizi wananyuti tuu kimyaa 😀😀.

2.pwngine wazazi wako huweka nao mazoea tokea utotoni mwenu mkawa mnashare vitu mbali mbai kama marafiki ,badala yake wakawa hawataki mzaha na wewe mama mama na baba baba hakuna kuchekeana.

Familia zingine huishi na wazazi wao kama marafiki,hii inasaidia mzazi akipata shida asione tabu kuomba kwa mtoto.

KUHUSU NINI UFANYE
Kwanza tambua wazazi wako dhiki wanayo,usije sema hawajapata shida ndo mana hawakuombi,shida wanazo lakini pengine wanapitia hatua hizo hapobili juu.

Hivyo cha kufanya usiweke akiba pesa yote maadamu hawakuombi,kama ulipanga uwape 70000 watumie 30K na 40K iweke.

Kumbuka kuwa kuwanyima wazazi wako sasa hivi ukawapa kidogo sio dhambi ikiwa tu una lengo la kujenga future yako,kwani future yako ndio future ya wazazi wako.

Hivyo ukifanikiwa katika future yako,basi na wazazi wako wefanikiwa pia,hivyo sio dhambi ukawapa kidogo na kingine ukasave for your future.

Jitahidi ukimaliza chuo uwe na jambo la kufanya,sio unamaliza chuo unaanza kialia kutafuta ajira wakati uliweza kusave na kuanzisha kabiashara kadogo.

Sisi ni vijana tunakua bado hivyo tuwekeze katika kutafuta kuliko kuwekeza katika kula bata.
 
Angalia nyumbani kuna shida gani kama labda bati zimechoka rekebisha,kama kuna ukuta unanyufa tengeneza vizuri au wanunulie hata mifugo apo nyumbani kama kuku,mbuzi ,wazazi ni "baraka"
 
Hapo ni wewe tuu kujiongeza...

Hongera kwa kupata wazazi wa namna hiyo,Kwa sabbu kuna viwazazi kero + visirani balaa
 
Kuna baadhi yawatu hata iweje hawawezi kuomba wanajiamini wanaweza kupambania maisha yao jipange ili siku wakishindwa kujitafutia uwe msaada
 
Wewe sio lazima uombwe, wewe mwenyewe angalia ni vitu gani ungependa wazazi wako wawe navyo kwa wakati huu, vitu ambavyo unaweza kuwasaidia au pia unaweza kukaa nao kitako na kuwauliza ni kitu gani wanachohitaji kwa muda huo.

Kwa maana nyingine wafanye wawe huru kufunguka kwako, yawezekana wewe ulipokuwa mdogo labda ulikuwa na tabia ya ukali sana na wazazi bado wanakuogopa --- kama ni hivyo jaribu kujenga urafiki, ucheshi na upole kwao ili wajenge confidence wakiwa na wewe.
Wazazi wanamuogopaje mtoto kisa ukali bro?
 
Deni kubwa ninaliona kwako unalo ndugu yangu,wazazi wako bado hawaoni kama umefika hatua ya kuombwa

Unachotakiwa kufanya kwasasa ni soma kwa bidiii sana, jitahidi kila uwezavyo ukue kiuchumi ni kweli upo chuo

Wazazi hawakuombi kitu ila si kwamba hawana shida wanatamani kukuona hicho kidogo kinaongezeka sasa wewe

Kitu pekee unatakiwa fanya sasa hivi ni kuwaza namna yakuongeza hicho kidogo ulichokua unataka watumia wazazi

Kama huna ubongo wa biashara,basi save hizo hela zao kama ulikua unataka kila wiki uwatumie 50,000,kwakua hujawatumia

Hifadhi hiyo 50,000 mahali na utambue kuwa si Yako ni ya wazazi wako,ukipata tena amount unataka watumia,ihifadhi kule ulipoiweka ile nyingine.

Nenda kwa mtirirko huo ukimaliza Chuo tumia hela za wazazi wako (zile ulizokua ukiweka) kuanzisha kitu chako kisimamie kwabidiii usizembeee.

nakuhakikishia zawadi pekee utakayoweza wapa wazazi wako wakaipokea kwa mikono miwili huku wakitabasamu kwenye nyuso zao ni "mafanikio yako kiuchumi" hebu wape hiyo zawadi wazazi wako.

unaona umetoka familia ya aina gani,wazazi wako hawataki kuwa mzigo kwako wanataka usiwe kama wao kuna mengi behind the scen huyajui wana ji sacrifice kwa sababu yako,Hawataki nawewe uje upate mateso hayo utakapokua unawahudumia watoto wako.

Wanakupenda sana,wanakuwazia mema jitahidi kuchangamsha hiyo akili,elewa una deni kubwa kubwa kubwa mbele yako Kimbizana na Muda mafanikio yako uyapate angali wazazi wako wapo HAI waonje Zawadi waliyotamani ipata kwako.

Natamani unielewe au nikupe hii kichwa yangu uelewe nini namaanisha na nataka uwe vipi,naamini umenielewa japo kidogo.
Ahsante kaka!
 
Jiongeze wewe, wanataka ujiandalie maisha, mshukuru Mungu, wazazi waelewa, wanataka ukomae utoke kimaisha.
Wanaridhika na walichonacho hawana tamaa, wape wanachohitaji siyo pesa, kama ukienda nyumbani, ukifika hakikisha paketi za sukari, mafuta ya kula, sabuni, mkaa, gesi unanunua mara moja moja.

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Wazazi wanamuogopaje mtoto kisa ukali bro?

Ipo hiyo, kuna baadhi ya watoto huwa wakaidi, Watundu, Watukutu, wakorofi, jeuri nk, na wanapokuwa watu wazima bado wazazi wanakumbuka watoto wao walivyokuwa utotoni kwasababu wao ndio waliowazaa, kwa jinsi hiyo wazazi wengine huwachukua/treat kwa tahadhari kubwa, itakuwa ni bahati njema kama mtu atambue kuwa yeye alipokuwa mtoto alikuwa na tabia hizo na ajaribu kujionyesha mbele ya wazazi kwamba katika utuu uzima hayupo tena hivyo na ndio maana nikasema kama alikuwa hivyo utotoni basi huu ndio muda muafaka wa kuwaonyesha wazazi kwamba upo tofauti na ulivyokuwa zama za utoto/udogo na upo kwa ajili yao, na sio lazima wazazi wakulilie shida bali wewe mwenyewe unaweza kuangalia na kuona ni kitu gani wazazi wanahitaji kwa muda ule basi uwahudumie na hapo unawazoesha kuomba msaada pindi wanapopata shida.
 
Mkuu Wazazi wangu walikuwa hivyo Yani hata Mia hawakuombi hata Kama wamelala na njaa.

Kwetu me ndo first born, baada ya kupata Kazi nikajichanga kurekebisha nyumba ya home and everything Yani nlifanya full renovations.

Sasa baba sijui akajua nalipwa millions Maana marekebisho yalikuwa ya gharama kidogo.
Saivi show naiona baba kila saa ananambia kuhusu kumlipia mdogo wangu ada sijui hostel na sio Kama Hana hela. Yani nikiona sim ya mdingi najua tu story za hela Hadi sometimes nakausha.

Tho mama Hadi Leo haniombi, Yani akiomba ujue shida imemshika kweli na hapo ataomba radhi kwa kukuomba.

Ma first born tunashida
 
Daaah! Tufarijiane tu kaka.
 
Jamani nishaurini na mama ndio kabisa yaani!
Mzazi mwenye akili hawezi kumuomba hela mtoto anayefahamu kabisa kwamba anasoma na si mfanyakazi; Ungekuwa unasoma na kufanya kazi hapo pengine wangekuomba; Maana mkopo sio kwa ajili ya wewe kujikimu kwenye masomo na sio; Kama hawalipi ada nadhani hiyo ni support Tosha sana kwao.
 
Back
Top Bottom