Wazazi wangenichagulia mke...

Mhhhh! Utadhani ulikuwepo jana nilipokuwa namshauri rafiki yangu aliyechaguliwa mchumba na mama yake. Mama kachagua binti wa kihindi jamaa naye ni mhindi ila anahusudisha sana watasha. Basi kauli yangu ya kumshawishi ili tu akutane na huyo bidada ili kuanza kufahamiana kwa karibu ni sawa kabisa na hayo maneno yako kwenye rangi.

Kuna kitu huwa wengi kuwa tunajidanganya... Eti "Mapenzi ni ya watu wawili" huwa sijui vigezo vya imani hii ni ipi.

Ndoa mnaoana wewe na huyo mwenza wako pamoja na familia nzima. Familia ina nafasi kubwa sana katika furaha, imani na amani ya ndoa tegemeana na circumstances zenyewe.

Faida ya kukubali mama kukuchagulia mke hi hizi:-


  1. Utaepuka sana kuwekwa kati na wanawake hao muhimu kuliko wote katika maisha yako... Mara mkeo mkiwa chumbani baada ya faragha - kuanza kulalama juu ya mamako huyo. Au ukienda kwa mama kulalamika juu ya mkeo.
  2. Heshima ya mkeo juu ya mamako kuwa juu kwa kutambua kuwa yupo responsible kwa yeye kuwa pale... Wanawake wengi hekima na busara imewashinda saana juu ya kufanya mashindano na mamamkwe... Husahau kabisa kuwa huyo mi mzaa chema, na kuwa nafasi ya kuwa mwanamke anaye tawala maisha ya mtoto wake ni kitu ambacho yeye (mamamkwe) kama mwanadamu lazima imuume. Hivyo huenda ndani ya ndoa huku kaajianda kabisa kuwa kuna vita dhidi ya mamamkwe juu ya mtoto wake.
  3. Uwezekano wa kupata mke mwema... Sababu hadi mamako a suggest ina maana kamuangalia binti, kaangalia familia pamoja na tabia zao za namna ya kuishi na watu.
 
Back
Top Bottom