Karibu sana. Huenda ukapata ukinzani kutoka kwake zaidi lakini msimamo wako ndio utakaomponya na yeye. Na baadae utaona akifurahia alichokua anapinga. Jitahidi kama ulikua unampa kitu labda kila mwezi uendelee kumpa ili asijeanza kulalamika.
Unapaswa uwe na msimamo wa kusimamia mawazo yako mema bila kuyumbishwa na baada ya muda watakufahamu hivyo na watakuheshimu hivyo. Ila ukiyumba tu kidogo tegemea kuyumbishwa kila mara. Mama zetu ni wema sana lakini SIO kila ushauri wao niwa kuzingatia. Wao pia ni wanadamu na kuna wakati mwingine ushauri wao huwa ni sio mzuri au kulipa visasi vyao au wa kuwaoneshea wenzao n.k n.k
Tuwaheshimu sana na kuwapenda wazazi wetu ila tupime pia ushauri wao kwa HAKI. Pale tunapoona hawajashauri vzr ni wajibu wetu kuwafundisha kwa VITENDO ama kuongea nao lkn kwa hekima saana.