NALIA NGWENA
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 10,377
- 12,935
NALIA NGWENA na ubishi wangu huu nimepiga sana vibao lakini kila nyimbo mpya bwana mdogo wangu anapita nazo /anazihifadhi akilini. Ni mtoto wa miaka minne nimekuwa nikishangazwa sana namna gani akihifadhi nyimbo kichwani mbaya zaidi huwa napata aibu ninapokua na wageni unakuta anaimba mashairi ya hamasa za ngono/matusi.
Kuna nyimbo moja nafikiri ni ubeti wa Mboso Khan Kuna kakipande anasema "Mjusi kafiri asafishe mtaro" mwanangu huo ubeti alikuwa anaimba wote. Na Kuna nyimbo nyingine nafikiri ni ya Harmonize Kuna ubeti anaimba "inama nipache Rungu". Yote Tisa kumi nyimbo ya umeyatimba ushairi wa Mboso anaweza akaimba asubuhi mpaka jioni hata hajali wala nini tena mbele ya wageni.
Nilipiga vibao lakini niliona vibao siyo suluhisho maana kuna muda huwa ananiambia "baba mbona kwenye TV huwa wanaimba"!? Husema kuwa namuonea. Kiukweli nyimbo za wasanii wetu wanatumia maneno machafu sana/matusi mpaka wewe MTU mzima hata kusikia mbele ya wakubwa wako unaona aibu.
Wakuu nyinyi mnatumia njia gani kumdhibiti mtoto wako asiimbe nyimbo zenye maudhui ya matusi/maneno machafu? Nasoma comments.