Wazazi wake wanagoma, nifanyeje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazazi wake wanagoma, nifanyeje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Magoo, Jul 7, 2012.

 1. M

  Magoo JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 438
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Nimekuwa na mahusiano na huyu binti kwa miaka 2 sasa nafsi yangu imeridhika naye na tulipanga baada ya yeye kumaliza masomo tuanze mipango ya ndoa, sasa kamaliza masomo yake....aliwaeleza wazazi wake kuhusu mimi na kwamba tunaitaji kupeleka posa kabla ya mipango mingine ya harusi cha kushangaza baba yake aligoma kwamba binti yake ni mdogo (22yrs) kiukweli sina amani coz tunaishi mikoa tofauti na hata kuonana inakuwa kazi sasa kwa sababu yuko home kwao ni ngumu sana kutoka naona kama naweza mkosa kama hali hii ikiendelea kwa muda mrefu. Yeye yuko tayari na ameridhia tatizo ni mzazi wake na ndiye anapaswa kumsikiliza, imefikia hatua nafikiria kumpa mimba ila kwa upande mwingine naona si sahihi. Naomba msaada wenu wa kimawazo kwa sababu hili swala linaitaji ridhaa ya wazazi ili kujenga uhusiano bora na familia yao
   
 2. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Ngoja nikakuitie Kaunga nikimkosa namwita gfsonwin...............mimi siko vizuri kimoyo kwa leo
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,442
  Likes Received: 81,491
  Trophy Points: 280
  Kama bado anasoma basi hili la kumpa mimba halijakaa vizuri, lakini kama kamaliza masomo yake na yeye karidhia kupata ujauzito basi kazi kwenu wapendanao...lakini hilo la udogo ni kweli ni bado mdogo ila unaweza kukuta watu wawili wenye umri kama huo mmoja akawa tayari kwa maisha ya ndoa na mwingine akahitaji miaka mingine michache.
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  hapo ni mimba tu, akina baba huwa wana wivu mkali kweli kwa binti zao.
   
 5. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 796
  Trophy Points: 280
  BAK said it all!
   
 6. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mpe mimba
   
 7. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Kweni ndoa ni lazima kwenye mazingira kama haya? Amchukue tu aishi naye mzazi mwenyewe atapata akili na kuamua kumuoza kabisa!!! Miaka 22 siyo mdogo aisee!
   
 8. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,219
  Trophy Points: 280
  hiyo ya mimba ndo solution, piga mimba hapo, baba mkwe atakutafuta mwenyewe
   
 9. M

  Mbozib JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Piga magoti muombe Mungu wako halafu uende tena kwa wakwe Mungu atakuwa amewagusa
   
 10. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #10
  Jul 8, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,738
  Trophy Points: 280
  Hapo ni kitu cha uvimbe tu hakuna jinsi.

  Mi mwenyewe................................:.................................................
   
 11. Voice of Wisdom

  Voice of Wisdom JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 541
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  kwa nini ufikirie kumpa mimba ndo suluhisho? Je hapo ndo mawazo yako yamefikia mwisho. Je umeshajaribu kutumia njia mbadala(mshenga kwenda kuzungumza na mzazi wa huyo binti?) kumpa mimba maana yake unataka wazazi wamwozeshe bint yao kwa shinikizo na si ridhaa yao, je unafikiri hata wakikubali utapata zile baraka kama mume? Wazazi watakuona mhuni kwani hakuna mzazi aliyeko tayari kuona mwanae anakuwa na mahusiaono ya kimapenzi nje ya ndoa(japo uhalisia wanajua wanafanya hvyo ila hawapo tayari kusikia au kuthibitishiwa). Fikiria watakuchukulia vp japo watakuruhusu umwoe. Wasikilize hao waze tafuta mshenga anegotiate nao.
   
 12. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #12
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,135
  Likes Received: 378
  Trophy Points: 180
  kamaliza masomo ktk level gan kaka?manake km ni chuo kikuu nadhani huyo ni mtu mzima kabsa,na wazazi wake wanatakiwa waheshimu mawazo yake.
   
 13. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #13
  Jul 9, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Kamaliza chuo au secondary?
   
 14. M

  Magoo JF-Expert Member

  #14
  Jul 10, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 438
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kamaliza Diploma ya ualimu
   
 15. M

  Magoo JF-Expert Member

  #15
  Jul 10, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 438
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Ahaaa 2meshafunga mara kibao laikini mzee haelewi kitu anasema after 2/3yrs ndo atasikiliza swala lake
   
 16. M

  Magoo JF-Expert Member

  #16
  Jul 10, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 438
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Thanks mkuu ila sitaki kumkosa coz wengi wakikaa muda mrefu hawakawii kubadilika na kusikia kuna m2 kamjaza
   
 17. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #17
  Jul 10, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Fanya subira na uendeshe mambo taratibu maadam uko kwenye jambo la kheri muamini mungu.
   
 18. sam2000

  sam2000 JF-Expert Member

  #18
  Jul 11, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 450
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Its better you unaambiwa umri bado, mwenzio naaambiwa lazima nitoke dini yao and huyu ni mtu nimekuwa nae for six damn years!!!
   
Loading...