Wazazi tuwaunge mkono watoto wetu na walimu kqwenye mgomo...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazazi tuwaunge mkono watoto wetu na walimu kqwenye mgomo...!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BabaDesi, Jul 30, 2012.

 1. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2012
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mgomo wa Walimu umeanza rasmi leo. Taarifa zinasema kuwa kuna baadhi ya shule nchini ambazo wanafunzi wameingia barabarani kuandamana kudai HAKI yao ya Kupata Elimu.
  Ni kitu cha ajabu sana kama watoto wetu wanaweza kuwa na akili na UJASIRI wa kutetea kile wanachhona ni HAKI yao wakati sisi Wazazi wao tunaangalia tu kama vile Mgomo huo hautuhusu wala kutuathiri kwa namna yoyote ile.
  Ni LAZIMA tuwaunge Mkono Walimu wetu na Watoto wetu kwenye Mgomo kwa sababu Serikali hii SI-SIKIVU inaweza ikaacha Mgomo huu uendelee kwa sababu Watoto wao hawasomi kwenye shule za Serikali ambazo Walimu wake ndio Wanaogoma.

  SHIME!! TUwaunge Mkono Walimu wetu na Watoto wetu Kugoma ili Mgomo huu ushughulikiwe Haraka Iwezekanavyo na Serikali hii SI-SIKIVU.

  Tufanyeje? Kwanaza tunaweza kuwaunga mkonon watoto wetu kwa kuingia barabarani na kuitaka Serikali hii kumaliza Mgomo huu haraka Iwezekanavyo na kuacha vitisho vya kitoto vya Watawala kutembelea Shule kuangalia Walimu waliogoma Wakati wanajua kabisa mgomo huu upo Kihalali!

  Tunaweza tukaanzisha pia medani yetu ya TAHRIR pale VIwanja vya Mnazi Mmoja na tukae pale hadi Mgomo huu ushughulikiwe na Serikali na Watoto wetu warudi madarasani na kupata HAKI yao ya kupewa Elimu. Inahitajika UJASIRI tu. Kama Watoto wetu wanaweza Kwa nini sisi Wazazi wao Tushindwe???

  Lakini Wote kwa Pamoja tunaweza kuungana na Wafanyakazi na kuamua kuwa Kama Serikali hii SI-SIKIVU itashindwa kumaliza Bai Wazazi wote waamue kwamba hawatakubali kuhesabiwa siku ya Sensa. Kwa nini Watoto wetu wahesabiwe wakati hawapewi HAKI yaoa ya msingi ya Kupata ELIMU????

  Watanzania Tuamkeni na TUwaunge mkono walimu na watoto wetu kupata HAKI zao za Msingi. Hatuna cha Kupoteza zaidi ya Minyoyoro ya WOGA iliyotufunga...!!!
   
 2. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #2
  Jul 30, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  naunga mkono hoja.%
   
 3. G

  Godwishes JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 577
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Tunduma kumechimbika.Nataman wanaf.wote Tz wangekuwa kama wa Tunduma.Thumbs up !wanaf.WAZAZ Na Walimu.
   
Loading...