Raynavero
JF-Expert Member
- Apr 29, 2014
- 38,375
- 56,096
Habari wana mmu.Ni mara ya kwanza kuposti hapa. Dada yangu anafundisha shule moja ya msingi ya hapa DAR.Jana shuleni kwao, wamewafuma wanafunzi kumi wa darasa la tano chooni wakilawitiana.Walipowahoji wameanza lini wakadai toka darasa la tatu.Na miongoni mwao kuna mwanafunzi ni muathrika na shule inafahamu. Walimu wakaafikiana waadhibiwe na waitwe wazazi wao,mkuu wa shule akaamrisha waadhibiwe tu wazazi na walezi wasiitwe,ana hofu habari zitawafikia vyombo vya habari,shule itapata kashfa. Nimeumia kama mzazi. Ombi langu kwa wazazi hasa wenye watoto wa kiume,tujitahidini kuchunguza watoto wetu hata kama tuko busy vipi.Tukumbuke kizazi cha sasa kimeharibika mno na tumuombe sana mungu alinde vizazi vyetu.