Wazazi na tabia ya upendeleo katika malezi

Steven mushi mushi

JF-Expert Member
Jul 25, 2016
533
739
Hii hali nimeishuhudia katika familia nyingi. Unakuta katika familia kuna mtoto ambaye anapendwa kuliko wengine na kufanyiwa kila kitu anchotaka na hata akikosea huwa haadhibiwa na katika hiyo familia unakuta pia wapo watoto wengine lakini yeye ndo anafanyiwa upendeleo na kudekezwa kuliko wenzake.

Lakini kwa upande mmoja au nyingine hii hali inaweza ikaleta hali ya chuki na utabaka miongoni mwa watoto kutokana na hii tabia ya wazazi kupendelea baadhi ya watoto na kutoshuhulikia wengine.

Ki ukweli hii tabia siyo nzuri hata kidogo katika malezi ya watoto na wewe kama mzazi unapaswa kuwalea wanao katika malezi sawa bila upendeleo na kama ni mda wa kufanya kazi basi hakikisha watoto wote wanafanya kazi na kama ni mda wa kupumzika basi wote wapumzike na sio unakuta mwingine yeye hafanyi kazi ilihali wenzake wanafanya kazi.

Vilevile katika suala zima la zawadi hakikisha pia hili unalifanya kwa usawa kwa watoto wote na sio flani unampendelea na kuwapunja wengine hiyo siyo sawa katika malezi kwa sababu wakati mwingine unaweza ukasababisha chuki na migogoro miongoni mwa watoto na wakati mwingine kupelekea hata watoto kuanza kubaguana na kutokuishi kwa upendo na furaha kama watoto wa familia moja kutokana na sababu sisizo za msingi kutoka kwa wazazi za kulea watoto kwa upendeleo.

Kwa hiyo wewe kama mzazi hakikisha unawalea watoto wako katinga misingi ya haki na usawa pasipo upendeleo wa aina yoyote na hii itakusaidia kuleta upendo na umoja katika familia yako na kuepusha chuki na manung'uniko yasiyo na msingi miongoni mwa watoto wenu na hii italeta usawa katika familia.
 
Haya mambo yalikuwa zamani kiongozi, siku hizi kila familia kuna Mtoto mmoja sana sana wawili, na unakuta Mtoto mwenyewe anapendwa/wanapendwa balaaa! Na majina yao utasikia sijui junia sijui Ian, mara Michelle sijui
 
Alafuuu wamesahau yale majina yetu ya akina shemdoe,shemndolwa, shekifu...... Utazani hawajatokea kule magunga au mlalo au soni pamoja na vuga
 
Haya mambo yalikuwa zamani kiongozi, siku hizi kila familia kuna Mtoto mmoja sana sana wawili, na unakuta Mtoto mwenyewe anapendwa/wanapendwa balaaa! Na majina yao utasikia sijui junia sijui Ian, mara Michelle sijui
mkuu wewe niombee kwa mungu baba niwe hai nikioa watoto wote majina ya bibi na babu zao yanawahusu hakuna cha ian wala michele nataka watoto kumi na nane mama tofauti
 
Back
Top Bottom