WAZAZI: Mwanangu anamchukia mdogo wake

WAZAZI: Mwanangu anamchukia mdogo wake

Nina mtoto wa kike wa umri wa miaka 4 ambae tangu utoto wake amekuwa karibu na mimi sana ,nkitaka kwenda kazini inabidi nimvizie nitoroke na nikirudi nyumbani lazima nibuni mbinu za kutoroka kwenda baa akila kabla sijala anakula kidogo,nikirudi hata kama ni saa saba basi ataamka na kula na mimi ,na usiku hulala kanikumbatia ,hata nikiamka kwenda chooni ataamka na kunisindikiza akiamini natoroka . Aidha yuko na ukaribu wa wastani sana na mama yake kwa uchunguzi wangu mama yake anamkono wa kimachame kwao anapiga sana mtoto hata kwa kosa la kutema mate kwenye sofa mimi kanizoea hadi balaa.

Sasa mwezi uloisha nikajaaliwa mtoto wa pili kwa mwanamke huyu wa kiume ,siku mwanangu wa kike alipomuona hospitali naskia alipiga kelele '' Eeeeh wameninunulia mdogo wangu '' akawa mala amlete hiki mara kile na hata mdoli wake pendwa uitwao emii (lilikuwa jina la rafiki yake jirani alieondoka) alimuachia mtoto hospitali .

Sasa mziki ukaanza alipoanza kushuhudia attention yetu ilivyohamia kwa mtoto mpya siku moja aligoma kulala akiwa sebuleni baada ya kumbembeleza akiwa amejikunyata alilia sana na kusema '' dadiii naomba mumrudishe huyu mtoto kwao mlikomnunua mimi simpendi'' looh nafsi iliumia sana ,niligundua niliacha mbachao ,baya zaidi hata wanafamilia wengine wanaonekana wamehusika katika kumtenga .

Basi nikaja na mbinu matata ya kujifanya sitambui uwepo wa mwanangu mpya kikweli anafurahia sana nakatoa out,kuogelea ,nakapeleka mwenyewe shule na kitandani mama busy na kichanga mimi na ka daughter kangu .tatizo ni akilia tu mtoto anasema ''kelele rudi kwenu..'' ukiimpa zawadi anaficha eti mtoto ataiba ,hivi zipo mbinu zozote za kisaikolojia au nisubiri tu akue mambo yatajiset ,Maana tulipofikia hairuhusiwi kumiacha mtoto na dada yake .
Mimi sio mtaalamu wa hayo mambo japo ningependa kukushauri mambo machache yanaweza kuwa na msaada kidogo

1. Jitahidi sana kuwanunulia zawadi wote wawili unapopata nafasi ya kufanya hivyo. Unaweza kumpa Kwanza dada unamwambia yeye ampe mdogo ake

2. Mueleze huyo mtoto mkubwa huyo ni mdogo wako unatakiwa kumpenda ( tunaita kumnenea mtoto ). Hata watoto washanga wahenga wanashauri kufanya hivi kwa ndugu wa karibu ili wasiwaogope. Itaanza kumkaa akilini kwamba ni mdogo ake na anatakiwa kumpenda

3. Mpe majukumu huyo mtoto mkubwa ya kumsaidia mdogo ake. Hapa namaanisha kumtuma vitu vyake vidogo vidogo taratibu itamjenga kiakili na kifikra.

4. Mkemee akiongea maneno mabaya ( kumkemea kirafiki sio kumpiga au kumkaripia)

Mimi nimemaliza kwa uelewa wangu mdogo
 
Umemaliza sina haja ya kuongeza pia apandikize neno la Mungu ndani mwao.
 
Au katoto hako si kako kweli.. Jaribu kuwa makini labda umeuziwa mbuzi kwenye gunia..
Anyway uzi wako huu unatamanisha sana mzazi kuwa na ukaribu na watoto wake hata watoa mimba wanaumia sana waonapo mapenz ya dhati
mhh sasa mfano sio wangu ,tatizo liko wapi mkuu ? Mi nimeadress wazazi we na konki mnatafuta nini humu
 
Kila unakifanya maishani kina matokeo hasi au chanya maishani ,jitaidi unakuwa na mtoto usizidishe mapenzi mpaka mwingine akajua kuwa mm sipendwi.kuna mzee mmoja alikuwa kama ww yy alizidisha mahaba kwa mmoja pia alikuwa mkali sana kwa wengine sasa wale ambao hakuwa penda waliajiliwa America na huyu aliempenda alikuwa kawaida tu kimaisha.sasa hawa wa America kidogo tu mama kaitwa America kwa wanawe mpaka ikafikia hatua America ikawa kama home 🏠.baba wivu ukaanza mbona mm siitwi mara vile kisa alilofanya ni kubagua watoto nao wanambagua,majuto ni mjukuu.
Hao watoto ningewazira yaani mtoto nimlee mimi afu annunie kisa nampenda nduguye hao wangetafuta baba yao huko ulaya fasta
 
Asante bro Najitahidi sana ,mfano nimeondoa stock yote ya pombe nyumbani ,sivuti sigara mbele yake na sirudi kabla sijala big g,Mamake humpeleka kanisa kila jumapili na nilimpeleka kujiunga sunday school wamesema awe anaenda kushinda tu ila at 5 ndo ataanza rasmi

Pamoja ndugu
 
Huu uzi umenikumbusha mwanangu, napenda sana maisha ya familia na watoto, naamini siku moja kushoto ataketi mke pembeni mtoto.
 
Usijali mkuu ni kawaida tu mfano hai ni kwangu

Mimi na mdogo wangu anae nifata tumepishana kwa miaka mingi sana

Alivyo zaliwa nilikuwa simpendi nikimuona nachukia ata kumgusa nilikuwa sitaki

Ila kwa sasa nampenda kuliko maelezo kumpiga siwezi akizingua namsemesha ila sio kumpiga nampenda sana

Usijali walee vizuri wanao haswa katika maadili ya dini

Mungu akukuzie salama
 
Akikua ataacha...hata mimi ilikuwa kama wew
But baada ya mda alianza mpenda mdogo wake
Nina mtoto wa kike wa umri wa miaka 4 ambae tangu utoto wake amekuwa karibu na mimi sana ,nkitaka kwenda kazini inabidi nimvizie nitoroke na nikirudi nyumbani lazima nibuni mbinu za kutoroka kwenda baa akila kabla sijala anakula kidogo,nikirudi hata kama ni saa saba basi ataamka na kula na mimi ,na usiku hulala kanikumbatia ,hata nikiamka kwenda chooni ataamka na kunisindikiza akiamini natoroka . Aidha yuko na ukaribu wa wastani sana na mama yake kwa uchunguzi wangu mama yake anamkono wa kimachame kwao anapiga sana mtoto hata kwa kosa la kutema mate kwenye sofa mimi kanizoea hadi balaa.

Sasa mwezi uloisha nikajaaliwa mtoto wa pili kwa mwanamke huyu wa kiume ,siku mwanangu wa kike alipomuona hospitali naskia alipiga kelele '' Eeeeh wameninunulia mdogo wangu '' akawa mala amlete hiki mara kile na hata mdoli wake pendwa uitwao emii (lilikuwa jina la rafiki yake jirani alieondoka) alimuachia mtoto hospitali .

Sasa mziki ukaanza alipoanza kushuhudia attention yetu ilivyohamia kwa mtoto mpya siku moja aligoma kulala akiwa sebuleni baada ya kumbembeleza akiwa amejikunyata alilia sana na kusema '' dadiii naomba mumrudishe huyu mtoto kwao mlikomnunua mimi simpendi'' looh nafsi iliumia sana ,niligundua niliacha mbachao ,baya zaidi hata wanafamilia wengine wanaonekana wamehusika katika kumtenga .

Basi nikaja na mbinu matata ya kujifanya sitambui uwepo wa mwanangu mpya kikweli anafurahia sana nakatoa out,kuogelea ,nakapeleka mwenyewe shule na kitandani mama busy na kichanga mimi na ka daughter kangu .tatizo ni akilia tu mtoto anasema ''kelele rudi kwenu..'' ukiimpa zawadi anaficha eti mtoto ataiba ,hivi zipo mbinu zozote za kisaikolojia au nisubiri tu akue mambo yatajiset ,Maana tulipofikia hairuhusiwi kumiacha mtoto na dada yake .
 
Eti kelele rudi kwenu[emoji1787] chunguza vizuri kati yao mmoja sio mtoto wako
 
Mkuu 'wivu' ni kitu kilichomo ndani ya kiumbe hai chochote achilia mbali miti, hata katika Biblia inasema msiabudu miungu wengine maana Mungu wetu ana wivu. Wivu ni hali ya kuona thamani ambayo ulikuwa unaipata inaelekezwa kwa mtu mwingine na kwako inapungua au inatoweka kabisa. Katika hali hii hata mtoto anakuwa amefurahia ule ukaribu na wazazi sasa anapokuja mwingine lazima care iende kwa mtoto mpya. Wewe kama baba jaribu kubalance upendo huo, mshirikiahe mwanao wa kwanza katika malezi ya huyo mdogo. Yaani kama unambeba uwe nae pia. Mwambie huyu ni mdogo wako na uwe unajaribu kumpa baadhi ya majukumu ya mtoto kwa huyo wa kwanza kama kumbeba, kumbembeleza akilia yaani mtoto akilia mwambie tumbembeleze mtoto anyamaze wote, yaani mshirikishe katika malezi ya mdogo wake ili wakue kwa upendo, wazungu wanafanya hivyo ila kibongobongo hao watakuwa wanadundana kila siku. Anachohitaji mkubwa ni ukaribu wako, hivyo kuwa karibu nae kwa kumlea mdogo pamoja,
 
Kwakweli inanipa faraja sana, ila mwanzoni nilikuwa naogopa hata kumuacha mtoto peke yake.
Mwenyewe akitoka shule anaanza kumsimulia vya shule basi mdogo wake akicheka yy anajua kameleewa basi nae anafurahi kumbe mwenzake anajichekea zake tu malaika wake
Wewe unajuaje hajaelewa? Tafiti zinaonesha watoto wadogo sana wana uwezo mzuri tu wa kufuatilia mambo, ingawa hawana ule utashi bado.
 
Mkuu pamoja na michango mizuri ikiwa ni pamoja na pongezi kedekede kuna jambo nilikuwa tushirikishane kuhusu saikolojia ya mtoto. Katika umri huo age ya miaka 4 ni kipindi ambacho mtoto anaanza kumifunza kujitegemea. Hii ni pamoja na kwenda shule za wali anaachw bila kushinda na wazazi wake na kucheza na watoto wengine. Akiwa nyumbani the same hatua za toilet training, table manner anakuwa ashazipitia. Sasa any way mkuu kulala na mtoto wa age ya miaka minne najaribu kuileta picha haiji. At age of 4 moto ashaanza kuwekewa ratiba ya muda wa kula kucheza na hata kulala pia. Mtoto anakupenda ndio na kawaida mtoto hukimbilia zaidi pale anapoona kuna attention kubwa kwake. Hapa pia mtoto anafundishwa do and don't! Uhuru kwa mtoto ni mzuri lakini uhuru usionekane kama upendo wa kumdekeza sana mtoto namaanisha spoiling! Kuacha kula vizuri mpaka akusubiri hata ukichelewa fyekelea mbali hapo si sawa na mbaya zaidi epuka kulala na yeye watoto ndo umri wanahadithiana jinsi wazazi wao walivyo. Baba yangu ana hiki na hiki na kile huwezi jua ukiwa umevaa pajama anakuchumgulia ukibadili nguo pia. Ni hayo tu!
 
Kwa kweli umechambua kisayansi bila kuweka mahaba niue nadhani sasa inabidi nianze kufuata ushauli wako kulala na housegirl kunamhusu na marufuku kunisubiri ,uko sahihi mkuu umeongea kama mzazi ,asante
 
Back
Top Bottom