The only
JF-Expert Member
- May 19, 2011
- 11,131
- 14,636
Nina mtoto wa kike wa umri wa miaka 4 ambae tangu utoto wake amekuwa karibu na mimi sana ,nkitaka kwenda kazini inabidi nimvizie nitoroke na nikirudi nyumbani lazima nibuni mbinu za kutoroka kwenda baa akila kabla sijala anakula kidogo,nikirudi hata kama ni saa saba basi ataamka na kula na mimi ,na usiku hulala kanikumbatia ,hata nikiamka kwenda chooni ataamka na kunisindikiza akiamini natoroka . Aidha yuko na ukaribu wa wastani sana na mama yake kwa uchunguzi wangu mama yake anamkono wa kimachame kwao anapiga sana mtoto hata kwa kosa la kutema mate kwenye sofa mimi kanizoea hadi balaa.
Sasa mwezi uloisha nikajaaliwa mtoto wa pili kwa mwanamke huyu wa kiume ,siku mwanangu wa kike alipomuona hospitali naskia alipiga kelele '' Eeeeh wameninunulia mdogo wangu '' akawa mala amlete hiki mara kile na hata mdoli wake pendwa uitwao emii (lilikuwa jina la rafiki yake jirani alieondoka) alimuachia mtoto hospitali .
Sasa mziki ukaanza alipoanza kushuhudia attention yetu ilivyohamia kwa mtoto mpya siku moja aligoma kulala akiwa sebuleni baada ya kumbembeleza akiwa amejikunyata alilia sana na kusema '' dadiii naomba mumrudishe huyu mtoto kwao mlikomnunua mimi simpendi'' looh nafsi iliumia sana ,niligundua niliacha mbachao ,baya zaidi hata wanafamilia wengine wanaonekana wamehusika katika kumtenga .
Basi nikaja na mbinu matata ya kujifanya sitambui uwepo wa mwanangu mpya kikweli anafurahia sana nakatoa out,kuogelea ,nakapeleka mwenyewe shule na kitandani mama busy na kichanga mimi na ka daughter kangu .tatizo ni akilia tu mtoto anasema ''kelele rudi kwenu..'' ukiimpa zawadi anaficha eti mtoto ataiba ,hivi zipo mbinu zozote za kisaikolojia au nisubiri tu akue mambo yatajiset ,Maana tulipofikia hairuhusiwi kumiacha mtoto na dada yake .