Wazazi hupandikiza maradhi kwa watoto wao bila kujua

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,351
33,187
Folic.jpg

WAHENGA wetu walitufundisha msemo unaosema; "Kila kizuri hakikosi kasoro". Ndiyo kusema kila jambo lina pande mbili, faida na hasara. Kwa watu wenye akili timamu wanachokifanya ni kujua hasara ni zipi na faida ni zipi. Vile vile, wanajitahidi kujua ni namna gani wataweza kupunguza hasara juu ya jambo fulani.


Katika makala hii nakusudia kuwazindua wazazi na jamii kwa ujumla namna wanavyopandikiza maradhi kwa watoto wao bila ya wazazi hao kujua, jambo ambalo linatokana na hasara ya teknolojia ya vyakula.

Teknolojia ya vyakula ina hasara na faida. Kwa upande wa faida, teknolojia hii inatuwezesha kutengeneza vyakula

ambavyo vinaweza kukaa kwa muda mrefu kabla ya kuharibika ikilinganishwa na vyakula vibichi. Kwa mfano maziwa ya ng'ombe ambayo mabichi (fresh) yanaharibika haraka zaidi kuliko yale yaliyotengenezwa na kuwa katika sura ya unga.


Mfano unaoonesha hasara ya teknolojia ya vyakula ni vyakula vinavyotengenezwa viwandani (au majumbani) ambavyo vinasukari nyingi. Vyakula hivyo ni kama vile pili (pelembende), Big G, biskuti, sukari gulu, gubiti, kashata, keki na kadhalika.


Sukari (ambayo inapatikana kwa wingi katika vyakula vilivyoviorodhesha hapo juu) inaweza kusababisha maradhi mbalimbali mwilini. Sukari inachangia kuoza kwa meno (hasa kwa watoto) inaleta kitambi (na unene), inasababisha kisukari. Pia sukari (nyingi) mwilini inasababisha ugonjwa wa moyo, matatizo ya ini, magonjwa ya ngozi, magonjwa ya tumbo yanayoathiri usagaji wa chakula na magonjwa ya aina nyingine.


Ndiyo kusema wazazi wanaowapa watoto wao vyakula kama pipi, Big G, biskuti, sukari gulu, kashata, gubiti, halua na mfano wa hivyo, wanapandikiza maradhi kwa watoto wao bila wao wenyewe (wazazi) kujua. Kwa maneno mepesi ambayo hata mwenye kiwango cha elimu ya ngumbalu atanielewa ninasema kuwa, wazazi msiwape watoto wenu

vyakula vyenye sukari nyingi kama vile pipi, biskuti, halua, Big G, sukari gulu, gubiti na kama hivyo.

Sambamba na hilo, wazazi wakumbuke kuwa kinga ni bora kuliko tiba.
Kwa hiyo, ni vizuri ukachukua tahadhari kwa kutokumpa mtoto wako vyakula vyenye sukari nyingi
 
Back
Top Bottom