Wazanzibari wawe shupavu wavunje muungano kama wana hoja na ubavu

mpayukaji

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
940
349
Ukisikia wazanzibari wanavyolalamika kukandamizwa na serikali ya muungano, unapata kinyaa na ngoa. Malalamiko ya wazanzibari yamegeuka ndwele tena isiyotibika. Kwanini wanashindwa kuamua moja kusuka au kunyoa wakaona ukweli mchungu? Je tatizo la wazanzibari ni muungano, viongozi wao au wao wenyewe? Je ni kwanini wazanzibari wanakuwa mabingwa wa maneno badala ya matendo? Onyo, wakati wakipanga kusuka hata kunyoa wafikirie watakapowaweka watu wao wangi waliozaliwa bara ambao wanaweza kuwa wengi kuliko hata hao waliosalia huko visiwani. Pia waangalie ukweli kuwa akina Seif na Jusa wanaowahamasisha kutalikiana na bara wengi wao wanaishi bara muda mrefu kuliko Zanzibar. Anyaway, wakimalizana na hawa ni wabara wataanza hawa ni wapemba nasi ni wazanzibari. Hawa ni mazalia ya waarabu nasi mazalia ya watumwa toka bara.
 
Wanaodai wanaonewa na wale wanaobeba wenzao wepi ni rahisi kujinasuwa? Nafikiri Watanganyika kwa uwingi na nguvu zao ndio wenye nafasi kubwa ya kujituwa mzigo. Labda tuseme kuwa mzigo huo una tija kuliko zaidi maumivu.
 
Does this mean muungano ukivunjwa watanganyika kwao na wazanzibar kwao? Mana hata huku Zenji uchinchukume nafkiri wameshazidi wenyeji!
 
Back
Top Bottom