Muungano: Ahmed Rajab na hoja laini na za kibabaishaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muungano: Ahmed Rajab na hoja laini na za kibabaishaji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nguruvi3, Oct 28, 2012.

 1. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #1
  Oct 28, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  (A)NOVEMBA 5 Wazanzibari wataadhimisha kutimu miaka miwili tangu iundwe Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

  Kabla ya hapo Wazanzibari walikuwa wamegawanyika vibaya sana.

  (1) Kwa hakika, mzozano huo si wa jana wala juzi. Ulianza kuchomoza mwaka 1957 pale siasa zilipokuwa zinachacha na watawala wa kikoloni wa Kingereza walipoanzisha mfumo wa siasa za vyama vingi.

  (2) Mikwaruzano na mifarakano ya kisiasa iliendelea na kusababisha Mapinduzi ya mwaka 1964.

  (3) Baada ya Mapinduzi hayo haikuchukua muda Zanzibar ikapoteza mamlaka yake kamili ilipoungana na Tanganyika mwezi wa Aprili mwaka huo wa 1964.

  (4) Wakati huo Mapinduzi yalikuwa ya moto lakini yalikuwa bado machanga na hayakutimia hata umri wa Siku Mia Moja. Ndiyo maana kuna wenye kuhoji kwamba Mapinduzi hayo yalinyimwa fursa ya kujiimarisha na kujizatiti ili yaweze kuyatanzua matatizo ya muda mrefu ya kisiasa, kiuchumi na kijamii yaliyokuwa yakiwakabili Wazanzibari.

  (5) Moja ya mambo yenye kusikitisha katika historia ya karibuni ya Zanzibar ni kwamba Mapinduzi ya nchi hiyo, ambayo katika siku zake za awali yalitangaza kanuni za kupigiwa mfano za kutaka kuleta usawa na maendeleo kwa Wazanzibari wote, yaliachiwa yapoteze dira na yapotoke.

  (6) Serikali ya Muungano, kwa upande wake, iliyakodolea macho tu Mapinduzi na vitimbi vya upotovu vya viongozi wake. Wakati wote huo Serikali ya Muungano haikuchukua hatua yoyote na wala haikuonyesha dalili ya kutaka kufanya chochote kile kuizuia hali ya uonevu na ya utawala mbovu isizidi kuwa mbaya.

  (7) Matokeo yake ni kwamba Mapinduzi yalikwenda kombo na yakapotea njia. Hii ndiyo sababu kwa nini hadi hii leo, katika kipindi cha takriban nusu karne, malengo Mapinduzi ya kuleta usawa na maendeleo hayakuweza kutimizwa.

  (8) Ni jambo lililo wazi kwamba Wazanzibari wamepata hasara kubwa kutokana na mgawanyiko na mfarakano wao. Kwa kweli hali hiyo ya kutokuwako suluhu ya kisiasa ndiyo iliyochangia pakubwa kuifanya Zanzibar iwe kama ilivyo hii leo.

  (9) Hali ya mambo hii leo Zanzibar ni tofauti sana na ilivyokuwa zamani. Hii leo Zanzibar ina serikali iliyoviingiza ndani yake vyama vyote vikuu nchini humo yaani Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF). Matokeo yake ni kupatikana umoja miongoni mwa Wazanzibari na pia utulivu wa hali ya kisiasa. Yote hayo mawili ni mambo adhimu na yanabidi yaendelezwe, yakuzwe na yaimarishwe ili Wazanzibari waweze kutimiza malengo yao.

  (10) Wazanzibari wanatambua umuhimu wa kuhakikisha kwamba amani na hali ya utulivu inaendelea kudumu ili waweze kufanikisha juhudi zao za kupigania pawepo na mfumo mpya wa ushirikiano kati ya Zanzibar na Tanganyika wakati wa mchakato wa sasa wa kuitunga upya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

  Hawatoweza kamwe kuyapata matlaba yao bila ya kuwa watu wamoja waliosimama pamoja na wenye kuamini kwamba kuwa watiifu kwa nchi yao na kuyapigania maslahi ya nchi yao ni jambo la wajibu na lililo muhimu na adhimu kushinda utiifu kwa chama chochote cha kisiasa au itikadi yoyote ya kisiasa.

  (11) Kuhusu suala hili, Wazanzibari wanaelewa vilivyo kwamba ikiwa hali ya amani itachafuliwa basi hali ya ndani ya nchi haitokuwa tulivu wala imara na itaitia nchi yao jina baya ulimwenguni. Kwa hakika, hali hiyo itakwenda kinyume na maslahi ya Zanzibar kwani baadhi ya watu wataanza kuwa na shaka ikiwa Zanzibar yenye mamlaka yake kamili itaweza kuhifadhi amani na hali ya utulivu na wakati huohuo kuwapatia Wazanzibari maendeleo ya kiuchumi na ya kijamii.

  (12) Kwa hivyo, katika kuuadhimisha mwaka wa pili wa uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni muhimu Wazanzibari wa itikadi tofauti za kisiasa wahakikishe tena kwamba wamejitolea kuyatetea Maridhiano pamoja na umoja wao wa pamoja. Hizo ndizo nguzo mbili zitazowawezesha kutimiza lengo lao la kuwa na Muungano wa aina mpya na Tanganyika.

  Huu si wakati wake lakini nina hakika iko siku hao wenye kuleta chokochoko ama watafichuliwa na Wazanzibari wenzao au watajifichua wenyewe kwa njama zao. Itafika siku umma utachoka na chokochoko zenye lengo la kuubabaisha na kuutoa kwenye mstari wa kupigania pawepo mashirikiano mapya na Tanganyika.

  (13) Kuna safu mbili za wenye kuleta chokochoko hizo. Ya kwanza ni ile ya wahafidhina wa CCM/Zanzibar ambo tangu mwanzo walijitokeza wazi kuyapinga maridhiano. Hawa bado wanaendelea na vitimbi vyao.

  Safu ya pili ni ya wale wanaojaribu kuihujumu Serikali ya Umoja wa Kitaifa bila ya kutanabahi kwamba nao pia wanaangukia kulekule kwa wahafidhina wa CCM. Wanachofanya hawa ni kuwatia mitegoni vijana wenye jazba nyingi lakini wasio na uweledi wa kisiasa.

  Uchambuzi wangu:
  Mara nyingi tumesema kuwa hoja za Ahmed Rajab haziwezi kusimama zenyewe bila kutaja Muungano wa Tanzania au Tanganyika kama inavyosomeka katika (3)(6)(10)(12).

  Mwandishi anajua kuwa ili kuleta hasira na kuamsha hisia za Wazanzibar hata kwa matatizo yao ni lazima aitaje Tanganyika(1)
  Kichwa cha habari (A) kinaashiria kuwa habari hii ni juu ya serikali ya muungano visiwani. Hoja hii inapoteza maana kwa makusudi au kwa bahati mbaya kwasababu hakuna kwa kuishirikisha Tanganyika katika jambo lisiloihusu kama nilivyoonyesha hapo juu.

  Wakati anaeleza matatizo yaliyoanza Zanzibar mwaka 1957(1) Ahmed ameitupia lawama serikali ya muungano (6) miaka 7 tangu kuanza kwa choko choko na kuilamu kutochukua hatua.

  Hoja yake inapingana na nyingine (11) ambayo anataka Zanzibar yenye mamlaka kamili.
  Kwanini basi alaumu muungano kwa kutoingilia kati mambo ya Zanzibar huku akitaka ZNZ iwe na mamlaka kamili!

  Ahmed anaonyesha kuwa mikwaruzano ya kisiasa ndicho chanzo cha mapinduzi (2) na wala si uonevu wa tabaka la waarabu dhidi ya watu wengine.Anasema mapinduzi yamepoteza dira na yamepotoka(5) akimaanisha kuwa yalitarajiwa kuleta usawa. Je, ni kundi gain linaloona linaonewa hadi Ahmed kusema mapinduzi hayana maana tena?

  Wakati akisema mapinduzi yalilenga kuondoa ubaguzi na unyanyasaji, Ahmed huyo huyo anasema mapinduzi yamesababisha uonevu na utawala mbovu(6).

  Huu ni ushahidi mwingine kuwa Ahmed na kundi lake hawaamini katika mapinduzi.

  Ahmed anasifu umoja wa kitaifa ulioletwa na CCM/CUF (9). Wakati huo huo analaumu wahafidhina wa CCM (13). Huu ni ushahidi kuwa Ahmed ni CUF na anawaona wenzake wa CCM anaowasifia kwa unafiki kuwa ndicho chanzo cha mgawanyiko. Kwanini aamini kuwa CCM ndio wenye wahafidhina na wala siyo CUF.

  Na kama wapo kwanini atuaminishe kuwa serikali imeleta utulivu kwa mashirikiano ya vyama viwili (9).

  Katika yote hayo hoja kubwa ya Ahmed kuhusu makala yake (A) si kuzungumzia umoja wa Wazanzibar. Anachosema ni kuwa umoja wa WZNZ anataka ulete amani na utulivu (9), na baada ya hapo anafichua siri ya makala yake kwa kusema lengo la umoja ZNZ ni kukabiliana na Tanganyika (11)(12)(13)

  Hoja hii ni ushahidi kuwa adui wa Wazanzibar ni Tanganyika wala siyo mifarakano (2) na mapinduzi (3).

  Ili kuendelea kuubabaisha umma wa Wazanzibar, baada ya kuacha hoja ya serikali 3, mkataba wa Uswiss na sasa mkataba, mwandishi Ahmed ameibuka na tenzi mpya anayoiita mashirikiano mapya na Tanganyika(12)

  Hili la mashirikiano amelianza baada ya hoja yake ya mkataba kunyumbuliwa, kufinyangwa na kupuuzwa na kudharaulika kwa kukosa mashiko hasa na Watanganyika ambao wana weledi wa hali ya juu.

  Na katika kuhakikisha kuwa muungano unahitajika kwa Zanzibar Ahmed anataka kuwapumbaza Watanganyika kama anavyowafanyia wenzake visiwani kwa kutumia nahau, ngano na mashairi huku akificha ukweli kuwa Zanzibar inaiihitaji Tanganyika itake isitake.Ukweli huu hawaambii nduguze akidhani anaweza kutuduwaza nasi.

  Kwa vile anataka mamlaka kamili (3)(11) kwanini basi atake Mashirikiano na Tanganyika ile ile inayoleta mitafaruku Zanzibar? Kwa mara nyingine tunaona jinsi umoja wa Wazanzibar unavyoitegemea Tanganyika kiuchumi, kisiasa na kijamii.

  Vinginevyo Ahmed anayeitaka Zanzibar huru hana sababu zozote za msingi za kutuwashawishi Watanganyika kuwa mashirikiano mapya yatatusaidia zaidi ya kuisadia Zanzibar.

  Ahmed, mwisho wa mkataba, serikali 3, mashirikiano mapya ni Chumbe.Ukishavuka bahari kuu unaacha Uzanzibar Chumbe unatanguliza Utanzania, lau kama hamtaki hewala endendeni salama mkawasalimie waarabu.

  Makala ya Ahmed imenukuliwa kutoka katika gazeti la Raia Mwema. Tunawashukuru Raia Mwema
   
 2. takashi

  takashi JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2012
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 909
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #3
  Oct 28, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Takashi, Ahmed amwekea hoja nimezijibu moja baada ya nyingine.

  Sasa wewe unadhima ya kujibu hoja na si matusi. Matusi ni silaha dhaifu sana na ya mwisho kwa mwenye weledi kuitumia.
  Endapo kinachosemwasi kweli, jibu hoja na onyesha. Au la kimya nacho ni sehemu ya busara
   
 4. brasy coco

  brasy coco JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2012
  Joined: Apr 25, 2012
  Messages: 1,296
  Likes Received: 588
  Trophy Points: 280
  huyu Ahmed hana cha kuandika hana hoja si yeye tu wapo wengi wanaotafuta umaarufu kuoptia Tanganyika yani anaona asipotaja muungano wa tanganyika na zanzibar basi hatosikika huu ni ujinga sana
   
 5. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #5
  Oct 28, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Kama ukisomsoma vizuri yeye anataka wazanzibar wawe kitu kimoja ili kukabiliana na Tanganyika.
  Hoja zake zote amebadili isipokuwa moja tu, amegoma kutamka neno vunja muungano kama alivyoshindwa Maalim Seif, Jusa n.k.

  Ukimsoma vizuri huyu haamini katika mapinduzi kama Jusa, MaaliM,Mansour na akina Farouk Karim.
  Watake wasitake wanaiihitaji Tanganyika
   
 6. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #6
  Oct 28, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Badala ya kuangalia mpasuko wao wanataka kuingia kwenye ligi na Tanganyika, mimi nitaendelea kuangalia huu mfurukuto mwishowe ni nini maana wako all over the place
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ahmedi Rajab haishi vituko! Kimsingi anahimiza wazanzibari wote waungane ili kupambana na Tanganyika. Pamoja na kuzunguka-zunguka sana lakini anaonekana kusema kuwa chanzo cha mgawanyiko ni Tanganyika (muungano katika context ya Zanzibar ni Tanganyika). Kwa maana hiyo basi, matatizo ya Zanzibar including kugawanyika kwa wanzibari ni Tanganyika.


  Sasa, Bwana Ahmed anaweza kusema ni kwanini Zanzibar inataka kuwa na mkataba na Tanganyika? Kama mkataba huu wa miaka 48 sasa, umeleta mgawanyiko na 'dhiki' kwa wanzanzibari, kwanini watake mkataba mwingine? Kwanini Bwana Ahmed asihimize wazanzibari wote wadai uhuru kamili na kuachana na huyu 'mchonganishi' Tanganyika? Bwana Ahmed hataki kupumua?

  LET ZANZIBAR GO!
   
 8. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #8
  Oct 28, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Anachotaka ni umoja wa kupambana na Tanganyika, wakati huo huo hataki kuiacha Tanganyika.

  Ahmed anawadanganya WZN akijua fika nini kitatokea baada ya wao kuondoka. Hakuna mahali ameweza kuandika neno vunja muungano. Kwasasa hivi Mtanganyika tembea kifua mbele maana hakuna, narudia hakuna MZN mwenye akili timamu atakayethubutu, aliyethubutu kusema VUNJA MUUNGANO. Si Maalim Seif wala awaye.

  Zanzibar inihitaji Tanganyika itake isitake. Kasema Nasor Moyo, Jusa, Seif na Ahmed sidhani kama kuna kidudu mtu mwingine anayekataa ukweli huu. Wanachotakiwa sasa ni kuwa na nidhamu na adabu.
  Ujeuri mwisho Chumbe maana hakuna mwenye ubavu, abavu anao Tanganyika, period!
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,622
  Trophy Points: 280
  Mkuu Nguruvi3, kwa maoni yangu, tunapojadili issues za muungano, tuwe sensetive zaidi na upande wa pili!. Hizi kauli za "mwisho Chumbe" sio kauli zenye "good faith".

  Zanzibar ni mke, akichukia huhitaji kubembelezwa na sio kukaripiwa!. Achofanya Ahamed Rajab, ndicho kinachofanywa na baadhi ya vitimbakwiri vya muungano, kwa kumchagiza mke wetu Zanzibar kutaka kuanza kufanya visa, vitimbi na viroja ili apewe talaka!. Kwa vile mume Tanganyika, bado anampenda mkewe Zanzibar, anapaswa kumbembeleza na kumuenga enga uli atulie tuli kwenye ndoa!.
  P.
   
 10. F

  FJM JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Pasco, unaitwa koloni lakini bado unaleta mambo ya kuwa sensitive? Una shida gani na kauli ya "mwisho Chumbe?. Tuna changamoto lukuki, elimu mbovu, huduma za afya mgogoro na hatuwezi kila siku ni kelele za ukoloni. Lazima tuzibe kelele ili tupate muda wa kufanya mambo yanayoeleweka. Kama Zanzibar wanaona muungano unawanyonya muda umefika wakaachan nao.

  2nd Paragraph yako sijaipenda hata kidogo.
   
 11. F

  FJM JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Bunge la muungano linaanza siku si nyingi. Tuone nani anataka kupumua!
   
 12. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #12
  Oct 28, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Pasco kwani huyu mwanamke asiyeisha vituko nani anamchagiza? ye kazi kutwa akizunguka kudai talaka ya mkataba? Mume Tanganyika kamfanya nini zaidi ya kumwangalia akifunga mtaa kuita matarumbeta ya kumsuta mumewe, shurti anacheza mwenyewe anatoa vijineno na kujijibu mwenyewe mume amtazama ati hasa mume kwa busara anamwambia mfano chukua kilicho chako uende salama. Hapo sasa ndio utaona uhayawani wa huyu mwanamke.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. F

  FJM JF-Expert Member

  #13
  Oct 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Talaka ya mkataba...hehehehe... Hello Hollywood!
   
 14. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #14
  Oct 28, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Seriously FJM ukicheka na nyani utavuna mabua, platform ndio hiyo Bunge ndio linaanza hilo sasa basi tuwasikie wakiwasilisha madai ya kisheria ukizingatia kwasasa wao ni "wamoja" (kichekesho hicho) Alijisemea Nape, Bwana fulani sahivi kaufyata na ndevu ananyoa haleti fyongo tena baada ya kupewa hisani na CCM
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. F

  FJM JF-Expert Member

  #15
  Oct 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Katika vitu ambavyo vinaniacha hoi ni jinsi wanavyongelea as if Tanganyika will go along with whatever demand from Zanzibar! Yaani uniite mkoloni, udai nikulipie bill zako mpaka umeme, uje na marakatasi ya kunisanisha (for another 'ATM season?).

  Ni kwanini Bwana Ahmed anafikiri Tanganyika wanakata mkataba mwingine na Zanzibar? What for? Na kwanini mtu utake mkataba na mtesi/mnyonyaji? This doesn't make sense kabisa!
   
 16. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #16
  Oct 28, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Nilitarajia Wazanzibar ''wamoja'' waungane kuwazuia wabunge wao wasije Dodoma. Hilo halitatokea hata siku moja.

  Napenda sana kauli ya Mkandara 'Kadhi kaingia mjini wanandoa hawataki kuomba talaka''. Ndio kama Elizabeth Dominic asemavyo'' mke hataki talaka amebaki kuita matarumbeta''.

  Mkuu Pasco, kauli za mwisho Chumbe ni zao. Wao walisema azimio la Arusha mwisho chumbe. Nami nasema chochote wafanyacho kwa masilahi yao mwisho chumbe. Nafuata tu kauli zao. Si Karume alisema?

  Tena wakasema koti likikubana unalivua na ndivyo ulivyo muungano. Sasa koti limewabana wanataka kulivua halafu wampe Mtanganyika alibebe. Sisi tunasema koti limewabana wanachopaswa ni kulivua na kulibeba au kulitupa.

  Mkuu Pasco kama issue za muungano ni sensitive mbona Ahmed Rajab haachi kuzua uongo na kubambikizia Tanganyika matatizo yao ya mwaka 1957. Inakuwaje anasema Wazanzibar waungane dhdi ya 'adui' yao Tanganyika, sio umoja wa nchi bali umoja wa kukabiliana na Tanganyika. Hii ni nini kama si ukosefu wa fikra, uchochezi usio na uhalali na unafiki uliobobea.

  Niweke kumbu kumbu sawa.
  Ahmed Rajab alianza na hoja ya kuvunja muungano ili ZNZ iwe kama Malaysia! Hoja imekufa
  Akaja na serikali 3 ili nchi za jirani zijiunge, hoja ikakosa mashiko, akashindwa kuitetea na kuonekana upuuzi tu
  Akaja na Muungano wa Uswiss akisadiwa na mwanasheria wa Unguja, hoja ikakosa miguu
  Akaja na mkataba, akaulizwa wa nini, akashindwa kutetea
  Sasa ameibuka na mashirikiano mapya, tunamuuliza yapi hayo? kama ya EAC, SADC, FIFA au CHANEZA. Hana jibu.

  Muhimu ni kuwa kwanini WZNZ wasiotaka muungano, wanaotaka ukoloni ufike mwisho na wanaotaka mamlaka kamili hao hao wanataka uhusiano na Tanganyika wala si Kenya, Comoro au Mauritius.

  Mwisho wa kutishia nyau umefika, sasa ni ima wasikilize tunasema nini au waondoke.
  Hakuna hata mmoja miongoni mwao mwenye nguvu ya kusema VUNJA MUUNGANO. wameufyata wote!

  Tanganyika tembeeni kifua mbele kwa kujidai maana hamna cha kupoteza na wala humuihitaji ZNZ.
  Watanganyika hatupo tayari Mzanzibar mmoja au kikundi cha WZN kuamua tushirikiane vipi. Ikibidi tutaamua na si kuendeshwa na wafuasi wa Sulatan.

  Mwisho wa ubabaishaji Chumbe! baada ya bahari kuu nidhamu na adabu mbele.
   
 17. N

  Nonda JF-Expert Member

  #17
  Oct 29, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
 18. takashi

  takashi JF-Expert Member

  #18
  Oct 29, 2012
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 909
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Naona umekutana na waabudu Nyerere wenzio ,mnajifurahisha ....
   
 19. J

  JokaKuu Platinum Member

  #19
  Oct 29, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,137
  Trophy Points: 280
  Nguruvi3, takashi,

  ..naona Rajab hazungumzii tena muungano wa mkataba.

  ..nadhani hata Rajab amegundua kwamba hoja hiyo ilikuwa ya kipuuzi.

  ..hakuna ulazima wa mkataba, kila upande uwe kivyake tu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #20
  Oct 29, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Mkuu, Warioba aliuliza mkataba ni upi huo? Hakuna jibu, Ahmed amebadili dira kama kawaida yake.

  Kinachokera sana, ni kwanini Zanzibar inayotaka mahusiano na Tanganyika idhani kuwa ina haki saaana ya kuchagua aina ya mashirikiano. Kwanini wao waone wana haki na si Tanganyika. Haki hiyo wanaipata wapi na kwasababu zipi.
   
Loading...