Wazanzibar wanataka Muungano tulionao uendelee | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazanzibar wanataka Muungano tulionao uendelee

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Kimox Kimokole, Jul 9, 2012.

 1. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #1
  Jul 9, 2012
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  TUME YA KUKUSANYA MAONI JUU YA KATIBA MPYA- DUNGA 9/7/2012

  Dunga maoni leo:
  Walosema mfumo wa sasa wa Muungano uendelee ni 59, walotaka mfumo wa Serikali mbili huru zenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa na kisha kuwa na mashirikiano kupitia Muungano wa Mkataba ni 108, walotaka Tuachiwe tupumuwe ni 2, walowasilisha barua (mchanganyiko) ni 49

  MAONI JUU CHA MCHAKATO WA KATIBA HUKO MAKUNDUCHI

  Maoni Jana:
  Kijini (Makunduchi) walosema Tuachiwe tupumuwe ni 2, waliotoka nje ya mada ni 2, barua ni 3, walotaka Serikali mbili huru zenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa (Zanzibar na Tanganyika) na kisha kuwa na Muungano wa Mkataba ni 39, walotaka mfumo uliopo uendelee ni 78. Jumla ni 124.

  MAONI JUU YA KATIBA MPYA HUKO PAJE.

  Jana Paje na Bwejuu,
  Waliosema tuachiwe tupumuwe ni 8, waliotaka Serikali mbili huru (Zanzibar na Tanganyika) zenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa na kisha kufuatiwa na Muungano wa Mkataba wa Mashirikiano baina yao ni 46, waliotaka Muungano uendelee kama ulivyo sasa ni 25 na waliotoa maoni kwa barua ni 26 (ambao ni mchanganyiko baina ya wanaotaka muundo wa sasa na wale wanaotaka Mkataba).

  Kajengwa (Makunduchi):
  Waliotaka Tuachiwe tupumuwe ni 2, waliotaka Mkataba ni 48, waliotaka mfumo uliopo uendelee ni 69, waliokuwa hawakufahamika ni 2, barua 26.

  Mawazo yangu:
  Kwa matokea haya ni wazi Wazanzibar wanataka Muungano uendelee wa Serikali mbili ya sasa, msitarajie mabadiliko na msije mkawasumbua tena Watanganyika. Wako wapi waliosema Wazanzibar hawataki Muungano?

  Updates today:

  TUME YA KUKUSANYA MAONI JUU YA KATIBA MPYA.
  Leo Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba imemaliza kazi Mkoa wa Kusini Unguja,
  na mukhtasari wa maoni unaonesha kuwa waliotaka muundo wa sasa wa Muungano ubaki kama ulivyo ni 1503,
  na waliotaka Serikali mbili (Zanzibar na Tanganyika) zenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa na kisha kuwa na mashirikiano kupitia Muungano wa Mkataba ni 1411
   
 2. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #2
  Jul 9, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Source?
   
 3. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #3
  Jul 9, 2012
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mimi Mwenyewe na Tume ya Katiba
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Jul 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  WaZanzibar Hawataki Muungano Uvunjike Wanachotaka Wao, Wa Zanzibar wapate haki zao wasiingiliwe mambo yao ya ndani kwenye Serikali yao na hata suala la Mafuta ni yao ni la kwao. Lakini ikiwa Serikali ya Muungano ikiwa inaingilia Suala ya Serikali ya Zanzibar hapo ndipo Wa Zanzibar hawata utaka tena huo Muungano Uwepo. Hayo ni Mawazo yangu mimi sio mawazo ya Wa Zanzibar .@Kimox Kimokole
   
 5. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #5
  Jul 9, 2012
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  MziziMkavu kuna watu wa Zanzibar wanasema Wazanzibar wanataka "KUPUMUA" na hawataki Muungano. Lakini kwa maoni mengi yanayotolewa wanataka muundo wa sasa uendelee wa serikali mbili, na wengine wanataka Muungano wa mkataba, hapo ndipo nina wasiwasi...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Jul 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kimox Kimokole Kwa Ufupi

  WaZanzibar Wameshachoka na huo Muungano wetu Wanacho taka hawa Wa Zanzibar kuwa huru hawaoni Faida ya huo

  Muungano, Tangu Uanzishwe huo Muungano yafika sasa ni Miaka 48 hakuna faida yoyote ile kwa hao Wa Zanzibar .

  Kwa hiyo Wa Zanzibar Wamesha choka na Kero la Muungano hata kama wewe ulikuwa na Mke umemuowa miaka 48

  Mukaishi muda wote itafiki wakati iedha atakuchoka wewe huyo mke wako au wewe utamchoka mke wako kila kitu kina

  Mwanzo wake na Mwisho wake Mkuu nionavyo mimi hata kama kukiwa na kura ya Maoni Wa Zanzibar wote karibu asilimia

  99 hawautaki huo Muungano Mkuu nionavyo mimi mkuu na kwa mawazo yangu hayo.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #7
  Jul 9, 2012
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Wako huko huko Zanzibar, kwani hujui Uamsho wanapatikana wapi?
   
 8. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #8
  Jul 9, 2012
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mbona hatuoni juhudi zao za "Tunataka Kupumua" zikiungwa mkono?
   
 9. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #9
  Jul 10, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Hivi faida za Muungano ni nini; kwangu kama raia nitapimaje kuwa ninapata faida kwenye huu muungano. Nadhani zanzibar wanafaidi zaidi kwa vile wana uwanja mkubwa sana wa kupatia madaraka ya kitaifa kuliko mimi mitanganyika ambaye ama nitapata madaraka kwenye serikali ya muungano ama sipati madaraka kabisa.

  Wao wanaweza kupata madaraka ama kwenye serikali ya Muungano au kwenye serikali ya mapinduzi. wanaweza kuwa wabunge wa muungano wakiwa na sauti kama mbunge wa kutoka Tanganyika, wakati watanganyika hawawezi kuwa wajumbe wa baraza la wawakilishi.

  Niliupenda Muungano kwa sababu za kihistoria tu kuwa tumekulia ndani ya muungano lakini siyo kuwa ninapata faida yoyote na muungano huo ambayo ninaweza kuonyesha kwa majivuno.
   
 10. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #10
  Jul 10, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  MziziMkavu, umesema huwasemei Wazanzibari, mara umeanza kuwasemea, vipi tena??
  Maoni kutoka maeneo matatu yanaonesha hawana problem na Muungano....sasa usiloelewa ni kitu gani?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #11
  Jul 10, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Inasemekana umuhimu wa muungano upo katika suala la usalama/security.Zanzibar ikijitenga itakuwa rahisi sana kutumiwa kama ngome ya ugaidi na kutusababishia tukose amani.
   
 12. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #12
  Jul 10, 2012
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  yaani huko zanzibar ndo uswahilini kwelikweli! Wanataka "kupumua" = kupumzika kidogo kutoka kwenye kibano cha "ndoa" na tanganyika! Je, baada ya kupumua watarudi tena kwenye "ndoa" au wanataka "kupumua" kimoja? Mi naona hata misamiati mingine haina maana kutumika kwenye mambo mazito kama haya. Au mi ndo sijui kiswahili!?
   
 13. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #13
  Jul 10, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,812
  Likes Received: 2,584
  Trophy Points: 280
  Kwa twakimu hizi ni dhahiri Zanzibar wanataka muungano wa mkataba na siyo wa kikatiba. Hoja siyo kuwepo au kutokuwepo muungano bali ni aina ya muungano. Muungano wa mkataba ni msamiati mpya umejipenyeza katika mijadala karibuni labda wataalam wangetujuza zaidi juu ya muungano wa mkataba vis a vis muungano wa katiba.
   
 14. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #14
  Jul 10, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,398
  Likes Received: 6,585
  Trophy Points: 280
  Faida unazozizungumzia wewe ni zipi hasa ziweke wazi, maana tumekua tukisikia hizi kelele wengine hatujui mnazungumzia faida zipi..kama mnataka kuvunja mahusiano sababu ya mafuta..

  Who gave you 100% guarantee kuwa mtanufaika na hayo mafuta?? hamuoni kua ni kamtego ka wachache..Oneni kinachoendelea Nigeria..Wana mafuta lakini mafuta yote yanamilikiwa na makampuni ya nje..hapo Zanzibar kuna mzawa hata mmoja mwenye uwezo wa kuchimba hayo mafuta??

  Kama sio wageni ni nani mwingine zaidi..Jueni kua Bara pia kumegundulika Gesi asilia..na Kuna uwezekano mkubwa pia wa mafuta kufuata..Ok tuwaachie mafuta halafu?? mtakuja lia bure huko mbeleni...
   
 15. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #15
  Jul 10, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  Mie nafikiri hawa watu ni wa kupigwa chini tu.Tuna vijana wengi sana hawana kazi huku bara na wao wanatuzibia.Unajua watu wenye tamaa utawajua tu,akipewa kidogo,anatataka tena,na tena,natena, mpaka ataona kila kitu ni haki yake.Lakini kuna kitu hapa lazima tukijue,kwanini hawa watu wanasikilizwa sana?na huu Muungano uanatetewa kwa maslahi ya nani?Mie sipendi kabisa hizi kelele zao kwa kweli.Tupige serikali tatu, au vinginevyo kila mtu akae kwake.I don't like these noise Neighbours.
   
 16. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #16
  Jul 10, 2012
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Swali langu linaloniumiza kichwa ni Huo Muungano wa mkataba ukoje ukoje hasa?
   
 17. I

  Ibnu Mussa Member

  #17
  Jul 26, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  We kimox na wenzako msiichukulie zanzibar kama kijiji tu,ngoja maoni yakusanywe ktk mikoa yote ya zanzibar na sio kuchukua maoni ya shehia tatu tu. We vipi! Hebu kuwa mkomavu kisiasa. Acha kukurupuka dogo. Kumbe hata hujui nini muungano wa mkataba!
   
 18. b

  bin rasshid Member

  #18
  Aug 6, 2012
  Joined: Aug 6, 2012
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nashukur kujiunga katika jf ilinami nichangie kwani ww uamsho wanakuhusu nini
   
 19. b

  bin rasshid Member

  #19
  Aug 6, 2012
  Joined: Aug 6, 2012
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  waswahili wanasema uji mmoto hupembwa kwa ncha ya ulimi
   
 20. b

  bin rasshid Member

  #20
  Aug 6, 2012
  Joined: Aug 6, 2012
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ahsante kwakumjibu vizur pengine huenda akaelewa ikiwa ataacha mawazo yake na kuchanganyana wenzake
   
Loading...