Wazanzibar ni kama popo: Si ndege si mnyama

Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,559
1,452
Wazanzibar ni Kama Popo si ndege si Wanyama

1 Serikali Tatu

Haili suala alilizungumzia Lissu (Mtanganyika) lakini Chama Cha Jussa (CUF) Kwa Kushirikiana na Chama cha Sitta(CCM) wakamsulubisha Lissu hata kufikia Kuitaka SMZ irudishe Michnago ya CDM kwa Wahanga wa Meli ya MV Spice Highlanders.

2. Muungano

Lissu katika Hotuba yake ya kambi Rasmi ya Upinzania alipendekeza Kwamba Ni bora Watanzania (Tanganyika na Zanzibar) waulizwe kama wanauhitaji Muungano na kama wanauhitaji Muungano ni wa aina Gani. Wabunge wa Chama Cha Jussa (CUF) wakapendekeza yafanyike Maandamano Zanzibar ya Kumlaani Lissu na CDM. Nilitegemea kwamba Wataitisha Maandamano ya Kumpongeza Mtanganyika Lissu kwa kwa Kuunga Mkono matakwa yao lakini wapi.

3. Katika Mpya

Muswada wa kuundwa kwa tume ya Katiba mpya umesema kwamba "Ni Marufuku Kujadili Muungano katika kipindi cha kutoa Mapendekezo ya Katika Mpya" Wabunge wa Chama cha Jussa (CUF) wakishirikiana na CCM wakajadili Mpiasho halafu wakapitisha Muswada ule kwa Mbwembwe na Baada ya Wiki Moja eti wakaenda Ikulu Kumuona JK kujadilia Mapungufu ya Muswada.

Kama si Upopo ni nini huu?
 
Mmmmmh, siasa zetu za Tanzania zimeshanichosha, wanasiasa wetu wanafikiri kimakundi badala yakutafakari mmoja mmoja ndio wafikie muafaka hakuna hilo ndio maana leo wanafikilia hivi kesho yake wanabadili mawazo.
 
Matatizo ya wazanzibari yanasababishwa na wawakilishi wao, wanaganga njaa bara, wanawadanganya wazanzibari kuwa wanafanya walicho watuma, sioni kwanini wazanzibari hawayaoni haya.
Mimi napendekeza wanasiasa wote wa zanzibar waitwe Popo.
 
hahahahaha! albedo, dah!
binafsi hawa watu siwaelewi, sijui ni kwasababu wana asili ya ubishi?
wakitoa hoja ikikubaliwa wao hawataki ili waendeleze ubishi. wakisema Yesu si Mungu ukiwakubalia wao wanaona umewatukana, sasa tuwaeleweje ndugu zetu hawa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom