Wanabodi,
Hii ni makala yangu kwenye gazeti la Nipashe la Leo.
View attachment 3302753
Paskali.
Mbona unapotosha maana ya maneno. Kwa faida ya nani? Unataka kuwashawishi wananchi waamini kwamba huyo jamaa kabambikizwa kesi? Halafu situnaambiawagwa kwamba kesi ikiwa mahakamani haturuhusiwi kuijadili?
Sedition ni neno la kiingereza ambalo kiswahili chake ni uchochezi. Katika lugha yo yote ni kawaida Kitu au tendo moja linaweza kuwa na majina au maneno zaidi ya moja yanayoelezea kitu kile kile. Kwa mfano beautiful, cute na gorgeous yote yana maana moja.
Maneno usaliti, uasi, uchochezi, ukhulukutabu na uhaini yote yanaelezea kitu au tendo hilo hilo moja kama yalivyo maneno ya kiingereza ya betrayal, treachery, disloyalty, sedition and treason. Maneno hayo hutumika kumaanisha ukosefu wa kiwango cha juu wa utii (allegiance) wa mahusiano kati ya mtu na mtu, mtu na taasisi yake, kikundi chake cha kijamii, ndoa yake, wazazi wake waliomzaa au nchi yake aliyozaliwa.
Matokeo au adhabu ya makosa ya utiifu huwa ni kubwa. Kama ni ndoa ukiisaliti (kwa kutembea na mwanamke au mwanaume mwingine) ndoa hiyo huvunjwa (divorced). Kama utafanya hivyo kwa taasisi iliyokuajili utafukuzwa kazi. Kama ni chama chako cha hiari hususani cha siasa , utafutwa uanachama kama ilivyowatokea akina Kitila Mkumbo, Zitto Kabwe na wengine wengi waliokuwa chadema.
Makosa kama hayo ukiyafanya kwa wazazi wako waliokuleta hapa duniani kupitia kwa Mwenyezi Mungu, utaadhibiwa vikali Mwenyezi Mungu kwa kuvunja amri ya ya nne kwa wakristo, kwa waislamu sikumbuki ni amri ya ngapi lakini ipo kwenye maandiko ya Quran. Ni Mwenyezi Mungu ndiye hukuchagulia wazazi watakaokuleta hapa duniani hivyo unalazimika kuwatii. You owe them allegiance.
Vivyo hivyo Mwenyezi Mungu ndiye huchagua nchi utakayozaliwa. Hivyo makosa hayo ukiyafanya kwa nchi yako ambayo Mungu alikuleta, utaadhibiwa vikali kwa mjibu wa sheria na katiba ya nchi husika ambayo kwa nchi nyingi huwa ni kunyongwa hadi kufa au kifungo cha maisha ikithibitika mahakamani bila kuacha shaka ya mtu wa kawaida. Every citizen owes allegiance to the country in which he was born.
Tatizo la wengi ni kudhani serikali ndiyo nchi. Nchi sovereign ni kipande ardhi hapa duniani ambacho kina mipaka yake na raia wake. Raia wote ndiyo wamiliki wa hiyo nchi. Wameweka mifumo yao ya kujitawala hususani katiba ya nchi, serikali, mahakama, bunge la kutunga sheria wanazotaka wananchi,, majeshi na kadhalika. Kuna mkuu wa nchi ambaye hapa kwetu huchaguliwa na raia wote isipokuwa wenye umri wusiozidi miaka 5 na wale wenye dosari ya akili. Nchi kama Uingereza mkuu wa nchi amri jeshi mkuu huchaguliwa na familia ya kifalume (loyal family). Huko Marekani huchaguliwa na kikundi cha mabilionea wapatao 500 tu wanaojiita Electrol Conference. Sisi tukishamchagua mkuu wa nchi tunampa pia mamlaka ya kuwa mkuu wa serikali na amiri mkuu wa majeshi yetu.
Hivyo allegiance inayozungumziwa hapa ni kwa mkuu wa nchi na hiyo mifumo ya nchi iliyowekwa na katiba ya nchi. Sheria zinatungwa na wananchi kupitia bunge lao. Hazitungwi na wanasheria. Wanasheria kazi yao ni kusoma hizo sheria na kusaidia bunge katika uandishi wake. Ni wasomi na waandishi wa sheria zetu. Tatizo lao badala ya kujiita Wasomi na waandishi wa sheria wanaishiaga kwenye Wasomi.
Kila mtu anapaswa kujua sheria za nchi yake. Kuna msemo unaosema kutojua sheria is not a defense in a court of law. Sheria yetu kwa makosa hayo ya uhaini inasema: Any attempt to overthrow the government other than through election or any attempt toimpair the well being of the state to which one owes allegiance is treason by our country's constitution. Huyu mtu kwa muda mrefu amekuwa amkimtukana mkuu wa nchi na mtoto wake Abdul, amekuwa akitukana all the state apparatus zikiwemo mahakama, bunge na majeshi yetu.
As is for any criminal case all that the prosecution has to do is to convince the jury or the judge, leaving no reasonable doubt that the accused had the intent to commit treason and that his subsequent overt (visible) actions were directed to implement his intent.. Overt evidence typically occurs through verbal statements of the accused or through written advertisements or materials published by the accused. DCI ushahidi huo kwa asilimia 90% ambao DPP karidhika nao na hivyo kuamuru kukamatwa kwake ili kumpa fursa DCI kupeleleza the accused covert (hidden) actions evidence kwa kupekuwa mitandao ya mawalisiano ya kikomputa ya mtuhumiwa. Tuiache sheria ichukue mkondo wake. Ngoma itakuwa nzito na hatimaye bila shaka tunaweza kupata tutapata mpya ya kisheria ya uhaini kwa nchi yetu. Kitu pekee kinachoweza kukatisha mjadala huo mzito wa kimahakama ni huruma au parole ya mkuu wa nchi ambayo haitegemewi itatokea kwa mtu kama huyu.