Way forward 2018-2020


Mkuu mti haupukutiki kwa kiboko kimoja. Muda utasema.
 
Seriously anataka kuilinganisha ccm ya 1995 na ya sasa kwa hoja kwamba Mchonga aliisimanga? Zimwi likujualo halikuli likakwisha Mchonga asingekubali ccm ife
Nakuambia kwa hii staili ya uongozi wa mwenyekiti wao watamalizana tu wenyewe
 
Hapana kwasasa ccm ni majeruhi kuliko wakati mwingine wowote na hii inatokana na utemi wa mkulu wao kiburi na dharau
Mkuu TANU /CCM ni ile ile ya jana na juzi,alitoka katibu mkuu wa Tanu Oscar Kambona haikuanguka
Wakafukuzwa wabunge machachali zaidi ya 10 kwa mpigo akina Choga,Kaneno na wenzao haikuanguka.
Akatimuliwa Makamu wa Kwanza wa Raisi Aboud Jumbe na wenzake haikuanguka
Alijiondoa waziri Mrema akidai CCM sio baba wala mama haikuanguka
Horice Kolimba aliipaka paka matope kuwa CCM imekosa mwelekeo alikufa yeye kwenye mkutano,CCM ikazidi kudunda.
Kaondoka Edward Lowassa kwenye CCM na watu wake baada ya kukatwa jina CCM haikuanguka.
Kaondoka mmoja wenye hati miliki ya CCM Kingunge Ngombale Mwiru,CCM haikuanguka.
Na kuondoka light weight Mh.Nyalandu CCM ipo pale pale.
Siri ya CCM isianguke alizikwa nayo Mwl.Nyerere.
 
Wakati ni hakimu mzuri na hakuna kidumucho milele.... Wahenga walisema kamba hukatikia pembamba let's wait n see by the way karibu balimi.... Nimeamua kujinunulia zangu zile za noa
 
Mmmmmh!! Dalili za uchochezi na kufuatwa na Nissan nyeupe zinaendelea kuonekana.

Haya yanayojitokeza mfano wake ni mtu aliyekanyaga mwiba anapokaa chini autoe anakalia kibao chenye misumari... najaribu kuyafikiri mayowe yanayofuatia!!

Hongera muasisi wa viwanda Tanzania, hakika sasa nchi yetu inasonga mbele kutoka tulipokwamishwa na watawala waliopita.

Sitoshangaa viwanda vikiyeyuka kama zilivyoyeyuka zile 50m. zetu na Noah
 
Ulemavu uliopatikana Zenji mpaka leo hujapatiwa dawa, haina haja ya kuandika kinachoendelea Zanzibar maana nao ni uchochezi usiopendeza, acheni maneno tujenge nchi yetu.
 
Zilipopigwa 2015 ushindi wa JK wa 70% ulishuka mpaka 58% kwa Magu plus wizi wa kura sasa zinapigwa tena tukitoa tena 12% hope you know what I mean
 
Wakati ni hakimu mzuri na hakuna kidumucho milele.... Wahenga walisema kamba hukatikia pembamba let's wait n see by the way karibu balimi.... Nimeamua kujinunulia zangu zile za noa
Unajua CCM wao wanadai kutawala miaka elfu,nimeshuhudia siasa za CCM at across road 1995,tukiamini wanakwenda na maji,wapi wakajikongoja hao tena wakarudi magogoni.
2015 ilikuwa near miss bado wakadaka penalti wamechukua tena nchi.
Ukishafanya kosa la kujiondoa CCM nyota yako inafutika
Mkuu labda ndani ya CCM kuna Aliens toka sayari nyingine.
Sina jibu
 
Kma mko imara mnaogopa nni ssa kuruhusu mikutano ya kutafuta wanachama wapya na kwanni hamuweki tume huru ili mshinde kweupe!

Eti zaidi ya chama mnaweza jilinganisha na RPF?? NRM je??

Haya wwe niambie hapa mna mafanikio gani kuzidi KANU ila leo hii ikwapi??
 
Wakati utaamua hata mbuyu hauangushwi kwa shoka Moja kinachoifanya ccm iendelee kupumua ni mbinu chafu na michezo ya hila na sivinginevyo
 
Mimi naona umekurupuka. Kila mkoa ndani Tanzania una manufaa kwa Taifa zima. Tunachozungumzia hapa na kuhoji kwa nini wengine Watanzania hawahawa wavunjiwe nyumba mbali na zuio la mahakamani na mkulu anadiriki kusimama na kusema Mwanza wasibomolewe kwa vile walimpigia kura. Huu ni upuuzi kuligawa Taifa kiasi hiki. Basi asubiri 2020 Mwanza mumpigie kura tena na mikoa iliyobakia wampigie mpinzani wake halafu tuone. Yeye ni rais wa Tanzania sio wa Mwanza tu suck it in your brain!
 
Usipate shida best wengine wanaandikiwa kisha wapost
 
mtu aliekua au niseme anaependwa sana kati ya wanasiasa wa tanzania alihama CCM 2015 chama kiliyumba lakini hakikuanguka . impact ya nyalandu sio kubwa sana hili ni vuguvugu hasa kwenye mitandao kuna wanakijiji huku tandahimba wananiuzia korosho hawajui hata nyalandu ni nani . CCM ni zaidi ya tuijuavyo na kuiangusha yahutaji mageuzi makubwa ya kimkakati ndani ya upinzani .
 
Wakati utaamua hata mbuyu hauangushwi kwa shoka Moja kinachoifanya ccm iendelee kupumua ni mbinu chafu na michezo ya hila na sivinginevyo
But if you can not defeat them,you join them!!
 
Kamba hukatikia pembamba... Misri ya Hosni Mubarak ilitikiswa na wanasiasa nguli tena machachari sana lakini ikaja kuangushwa na kijana hohehahe asiyejulikana hata
 
Mtumishi yeyote asie na tija baada ya kulewa kazi anapaswa apewe redundancy, kuna mtu atakuja kuisoma namba 2020,
 
Kamba hukatikia pembamba... Misri ya Hosni Mubarak ilitikiswa na wanasiasa nguli tena machachari sana lakini ikaja kuangushwa na kijana hohehahe asiyejulikana hata
je watanzania tunayo hio spirit ya kina kibanga? ccm inashinda kwa michezo michafu unafikiri michezo misafi inaweza kusaidia upinzani kushinda ?
 
je watanzania tunayo hio spirit ya kina kibanga? ccm inashinda kwa michezo michafu unafikiri michezo misafi inaweza kusaidia upinzani kushinda ?
Muda ukifika itawezekana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…