Wawili wapoteza maisha kwa kukosa dawa za kulevya

nimesikitika kupima mafanikio kwa kuwa tu watu wamekufa kwa kukosa dawa za kulevya!.
Sheria namba tano ya 2015 ya kupambana na kusimamia dawa za kulevya iliyomuweka kamishna huyo, inaagiza kuwatibu waathrika wa dawa hizo...........kwa hiyo kitendo cha kusubiri watu wale wafe ni kuvunja sheria.
Lakini nimwambie kamishna, dawa hizo kutopatikana mtaani haimaanishi hazipo...........kwa sababu hatujasikia kama wamezikamata. kiinachoonekana ni kwamba wauzaji wanasubiri mhemko uliopo upoe watoe dawa zao chimbo maisha yaendelee.
Dawa ziko bado mtaani.
 
Kwahiyo hayo ndio mafanikio?!

Mgonjwa anapokufa ni sifa kwa daktari?.

Wataalamu wa hii Mamlaka wamepata mafunzo kweli?
Kwanini hao mateja wasingeenda sober house??

Unataka kumlaumu nani sasa.
Hao mateja ni wapuuzi wangeenda sober house

Bora wataalamu wa mamlaka haya huko ufilipino Duterte kaamua mateja wasipojisalimisha wauliwa

Kama mtu upo arosto,dawa hakuna ameshindwa vipi kusurrender sober house

Sijaona mantiki ya kuwalaumu wataalamu wa mamlaka

Lengo la mamlaka ni kukomesha uteja either die or surrender sober House
 
Kwanini hao mateja wasingeenda sober house??

Unataka kumlaumu nani sasa.
Hao mateja ni wapuuzi wangeenda sober house

Bora wataalamu wa mamlaka haya huko ufilipino Duterte kaamua mateja wasipojisalimisha wauliwa

Kama mtu upo arosto,dawa hakuna ameshindwa vipi kusurrender sober house

Sijaona mantiki ya kuwalaumu wataalamu wa mamlaka
Waliopewa dhamana ya nchi hii ndio walipaswa kuadhibiwa maana uzembe wao ndio umesababisha yote haya.
 
Nasema, kwa kujiamini, hii vita ikiendeshwa kimya kimya au kwa usiri, hakika haitafanikiwa, maana inatoa mwanya kwa nguvu ya pesa ya mapapa wa hiyo biashara, kuvuruga mikakati ya hiyo vita.

Kwa nini tusiamini kuwa wanaohusika na hiyo vita ndo wahusika wakuu wa biashara ya madawa ya kulevya. Ushahidi ni jinsi ukamataji wa washiriki wa biashara ya madawa ya kulevya, hasa watumiaji, ulivyopamba moto baada ya mkakati wa Makonda kuwataja baadhi tu ya wahusika hadharani.
Mkuu hayo ni maoni yangu, na wewe unayako, Ila wazia wale ambao wametajwa halafu ikaonekana ni wamechafuliwa majina, you think what will happen? Mnapesa ya kuwasafisha?
 
Kuna haja ya kufanya kampeni kubwa ya kuwaita mateja wote kwa amani tu ili wapatiwe matibabu
 
Nadhani Kamishina pale ukumbi wa Mwl Nyerere uliongelea suala la Harm Reduction (Upunguzaji madhara) kwa watumiaji wa drugs.

Ndiyo wakati muafaka wa kuwapata wale addicts ili waingie ktk program ya methadone kama alternative therapy ya heroin ili kupunguza madhara kwa kukosa 'unga' kuliko kuripoti vifo.
 
Ni matumaini yangu hii kimya kimya haita zima moto wa kupambana na madawa ya kulevya na baadae kumkumbuka Makonda!

Mambo ya kimya kimya ndio inashawishi wafanyakazi kujeuza kitega uchumi.
 
Hii vita inatakiwa iende hivi, sio kukurupuka tu na kutaja taja majina. Viva kamshina.
Tatizo wakikamata kimya kimya wanaweza kuelewana kimya kimya na kuachiana kimya kimya! Hofu yetu ni hiyo tu!
Wana jukumu la kutushawishi kuwa mbinu ya kimya kimya INA tija! Hii mbinu ya kimya kimya wahusika wameifurahia mno mpaka inatia shaka!
 
Kwahiyo hayo ndio mafanikio?!

Mgonjwa anapokufa ni sifa kwa daktari?.

Wataalamu wa hii Mamlaka wamepata mafunzo kweli?
Tume hii chini ya kamishna Sianga kazi yake ni kupambana na kuzuia biashara na matumizi ya dawa za kulevya WEL-BEING ya mtumiaji baada ya kuzuiwa hiyo ni kazi ya sober and other rehabilitation centers haya ni majukumu mawili tofauti.
 
Mkuu hayo ni maoni yangu, na wewe unayako, Ila wazia wale ambao wametajwa halafu ikaonekana ni wamechafuliwa majina, you think what will happen? Mnapesa ya kuwasafisha?
Suala si kuwa na pesa za kuwasafisha waliotajwa kw fitina au la. Lakini, bora kupoteza hiyo pesa ya kuwasafisha kuliko kuendelea na balaa la madawa ya kulevya.

Upande mwingine, ukinisingizia kuhusika na ikabainika si kweli, jina langu na hadhi yangu katika jamii itakuwa imeimarika.

Kuna ushahidi wa wazi, kwamba kuna watu maarufu wametajwa na wanaendelea kutajwatajwa hadharani, kuwa ni mafisadi papa, je, umaarufu wao umepungua!
 
Kwahiyo hayo ndio mafanikio?!

Mgonjwa anapokufa ni sifa kwa daktari?.

Wataalamu wa hii Mamlaka wamepata mafunzo kweli?
Unamuuliza nani sasa kamanda. Mafunzo gani hasa unataka wapewe zaidi ya waliokwisha pitia. Hivi unajua wamepitia mafunzo gani
 
Tatizo wakikamata kimya kimya wanaweza kuelewana kimya kimya na kuachiana kimya kimya! Hofu yetu ni hiyo tu!
Wana jukumu la kutushawishi kuwa mbinu ya kimya kimya INA tija! Hii mbinu ya kimya kimya wahusika wameifurahia mno mpaka inatia shaka!
Sawa Mkuu nimekuelewa, ila hii nchi hata kama ingekua wanapokamatwa inarushwa live ktk luninga bado wakitaka kuzunguka mbuyu unazungukwa tu.
 
Kwa nini pombe hizi zisiingizwe kundi la madawa ya kulevya ?
82c4d8668ebd5287092668360103707d.jpg

cc0b15f8fe7e29ccd9342427a86d4c48.jpg

5536249669bf89902bcb132a49b7dbfc.jpg

dd95fa57f7832c5149c10395a8edb878.jpg
 
Packaging imekaa poa brother.
Halafu kingine ni kwamba bei yake iko juu. Kundi la wanywa viroba hawafikii level hizo.
 
Back
Top Bottom