Acha wapumzike... Hii iwe fundisho kwa wengine kutambua madawa sio mazuri,tuyaepuke.
Kwa hiyo lengo ni kuhaakikisha mateja wote wanakufa kwa kukosa unga?Kwa hiyo ulitaka wapelekewe madawa ili wasife.?
Hoja hapa ni kuwa baadhi ya watumiaji wa mihadarati wamekosa dozi zao, hivyo kupelekea kuwa arosto.Kwahiyo hayo ndio mafanikio?!
Mgonjwa anapokufa ni sifa kwa daktari?.
Wataalamu wa hii Mamlaka wamepata mafunzo kweli?
Ni kweli rehab centers zipo na ndio maana kina Chidi wamepona na wanaendelea vizuri. Nonsense!Wewe hujui kuwa hao ni wagonjwa wanaohitaji matibabu?
Unajua kwanini kuna drug rehab centers?
Acheni kupenda sifa za kijinga!
Mineno mingine inakera ila uvumilivu unahusu hapaAcha kutetea wala unga ili tu uonekane unapingana na serikali.
Mwenyekiti wenu kesho anakamatwa atalala sero siku tatu kama ni mtumiaji lazima atapata arosto kwa hizo siku tatu.
Lama unadhani hii ni nzuri, then hujui ukiombacho. Vita ya kimya kimya si mpya, na halo ndipo vigogo hukwepea. Ushahidi ukikamilika ni muhimu kuwa exposedNafikiri hoja ya Sianga ni kwamba, kama matokeo ya initiative ya Makonda, upatikanaji wa madawa umekuwa mgumu na waliozoea kuishi kwa hizo dawa wanakufa. Yawezekana kufikiria kuwa Sianga amefurahia vifo hivyo lakini mimi nafikiri alichofurahia ni madawa kupungua mitaani.
Serikali ingetafuta namna ya kuwa rehabilitate waathirika ili wapone waachane na madawa. Sianga pia amesema hatataja majina hadharani; hii ni message sent to 'mungu' wa Dar na wote wanaofurahia maumivu ya wengine!
Usirudie kuni quote katika inshu ya ujinga kama hii... Kwahiyo unataka tuwatengenezee sehemu za kufanyia upuuzi wao. Ukishakua mtumwa wa madawa hakuna kitu. Kinga ni bora zaidi katika hili kuliko tiba. Itakuwa ngumu kutokana na mbinu zake ila hatuna budi kufuata hii njia... Uchina ambao sio dunia ya tatu unanyongwa. Kama unanufaika, mwisho umewadia. Tuwaache wa pumzike kwa amani ili iwe fundisho.Wewe ni matazania kama walivyo watanzania wengi majibu yenu yanafanana,wanatanzania wanajibu bila hata ya kufikiri bila hata ya kuangalia "impact" msukumo wa hili tatizo.Vifo vitazidi, familia zitaparaganyika ,nguvu kazi itapungua umasikini utazidi.
Ubora wa Binadamu unapimwa kutokana na maamuzi yake na msimamo wake hasa katika wakati mgumu.....Ni hulka ya waafrika kuwa na udhaifu wa kutoa maamuzi magumu,lakini watanzania wana udhaifu mkubwa kuliko waafrika hasa inapokuja serikali kuwaamulia raia wake, ukifanananisha waafrika wengine IQ yetu iko chini sana
Maendeleo yanaletwa na maamuzi, sisi kama nchi maendeleo yatachukua muda mwingi kutufika,maamuzi yetu yanatokana na hisia zetu sio kwa uhalisi wa jambo, tatizo hili la kuamua kwa hisia bila ya kutafakari ni tatizo la wafrka wote lakini watanzania tumezidi,nchi za wenye akili wanakuwa wanatushangaa utokana na maamuzi yetu
Wenzetu wenye akili ili kuwanausuru raia wao,kama kuna unga mkali mitaani wanatangaza kwenye radio,wametengeneza sehemu maalum kwa wateja kwenda kujidunga,wametengeneza sehemu maalumu kwa wateja kwenda kunywa dawa.
Hawa watu wanaziita nchi kama Tanzania ni nchi ya dunia ya tatu,Nchi kuitwa dunia ya tatu ina maana kuwa nchi ya dunia ya kwanza wametupita kiuchumi,kimawazo,kiakili tuko nyuma yao miaka 500.
Tumetawaliwa na chuki,viasi na uonevu hatufati yale ambayo tumeyapanga wenyewe ili yatuongoze,taifa litazidi kuingia kwenye majanga kama maamuzi yetu yatatawaliwa na chuki na visasi...
Wawili wapoteza maisha kwa kukosa dawa za kulevya
Sunday , 19th Feb , 2017
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga amesema watu wawili wameripotiwa kupoteza maisha mkoani Mwanza kwa sababu ya kukosa dawa za kulevya mtaani kama walivyozoea.
Rogers Sianga, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya
Kamishna Sianga amesema taarifa hiyo ameipata kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, hali inayomaanisha mafanikio ya mapambano ya dawa hizo, ambapo kwa sasa usambaaji wake umepungua mtaani kwa kiasi kikubwa.
"Nimeongea na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, ameniambia kwamba kuna watu wwili wamefariki sababu walikuwa drug addict na sasa dawa hizo hazipo mtaani" Amesema Sianga
Sianga amesema mara baada ya kupokea kijiti cha mapambano kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Mamlaka hiyo imeendelea na moto huo huo, na kwamba kwa hivi sasa timu yake hailali, ikiendelea na mapambano kila siku na kwamba hata leo, kuna mtuhumiwa mkubwa wa dawa za kulevya amekamatwa.
"Leo asubuhi tumemkamata mtuhumiwa mmoja mkubwa wa dawa kulevya, tupo naye tunaendelea kumuhoji, mengi yataibuka" amesema Kamishna Sianga
Kuhusu kuendelea kutumia mbinu iliyokuwa ikitumiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam paul Makonda ya kutaja majina hadharani,, Kamishna Sianga amesema hatatumia njia hiyo kwa kuwa kutaja majina ya watu hadharani kunaweza kuiingiza serikali katika matatizo maana kuna watu wengine wanaweza kutoa majina ya watu kwa sababu ya chuki binafsi.
Amesema njia anayoitumia ni kuwakamata na kuwahoji kimyakimnya na wakishajiridhisha hatua nyingine za kisheria zinafuata.
Katika hatua nyingine, Sianga amesema Tanzania iko makini katika kuwashughulikia wahusika wakubwa wa dawa za kulevya duaniani tangu miaka mingi iliyopita, akitolea mfano mtuhumiwa mmoja wa kike ambaye ni gwiji katika biashara hiyo au 'King Pin', ambaye hivi sasa amefungwa katika magereza ya Tanzania tangu mwaka 2010
"Tulimkamata mmoja kati ya watu waliokuwa wametajwa kama king pin wa dawa hizo nchini Marekani, alikuwa ameshindikana, na huko Marekani alikuwa na kesi zaidi ya 40, lakini alikamatwa hapa na amefungwa tangu mwaka 2010, yuko gerezani nafikiri kama siyo Keko, ni Segerea". Amesema Sianga.
Usirudie kuni quote katika inshu ya ujinga kama hii... Kwahiyo unataka tuwatengenezee sehemu za kufanyia upuuzi wao. Ukishakua mtumwa wa madawa hakuna kitu. Kinga ni bora zaidi katika hili kuliko tiba. Itakuwa ngumu kutokana na mbinu zake ila hatuna budi kufuata hii njia... Uchina ambao sio dunia ya tatu unanyongwa. Kama unanufaika, mwisho umewadia. Tuwaache wa pumzike kwa amani ili iwe fundisho.
Of course, sianga anauma na kupuliza. Vita ya kimya kimya ndo iliyoshindwa zamani!Lama unadhani hii ni nzuri, then hujui ukiombacho. Vita ya kimya kimya si mpya, na halo ndipo vigogo hukwepea. Ushahidi ukikamilika ni muhimu kuwa exposed
Uki kamatwa ukatoe maelezo unga umepanda bei wap? ume tambua vip? na ni kigogo gan anae piga pesa utaweza kujibu haya mkuu?... Hapo ndo utakaa usome rangi zoteDah. Sasa hii serkali nimeichoka kwa maigizo. Khaa.
Wanataka kuwaaminisha kuwa watz vita ya madawa imefanikiwa wakati bei za unga zimepanda. Vigogo wakubwa wa unga ndyo wanapiga pesa vizur sasa.
Ndiyo. Hawa ni wagonjwa, wanatakiwa kupata matibabu. Wakipona wanaweza kuwa msaada katika vita ya madawa ya kulevya.Kwa hiyo ulitaka wapelekewe madawa ili wasife.?
Nasema, kwa kujiamini, hii vita ikiendeshwa kimya kimya au kwa usiri, hakika haitafanikiwa, maana inatoa mwanya kwa nguvu ya pesa ya mapapa wa hiyo biashara, kuvuruga mikakati ya hiyo vita.Hii vita inatakiwa iende hivi, sio kukurupuka tu na kutaja taja majina. Viva kamshina.