Wawili matatani kwa utapeli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wawili matatani kwa utapeli

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mbonea, Sep 24, 2009.

 1. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  WATU wawili wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kutapeli shamba huko Kiluvya mkoani pwani.  </SPAN>Watu hao wakiwa na lengo la utapeli waliuza shamba la hekati tatu isivyo halali na kugundulika na kushikiliwa na polisi kwa kosa hilo.

  Watu hao ambao walitambulika kwa majina ya Said Said [45] na mwenzake Sylivesta [42] walimuuzia shamba hilo Bakari Ohumani [40] kwa lengo lda kumtapeli kwa kuwa shamba hilo lilikuwa lilishauzwa kwa mtu mwingine.

  Akielezea kwa umakini mtapeliwa amesema kuwa alikuwa anahitaji shamba na alielekezwa na wakazi wa maeneo hayo kuwa wao huwa wana mashamba na kuonana nao kwa lengo la kuuziwa shamba hilo kutoka kwa watu hao.

  Hivyo walikubaliana bei na kwenda kukagua shamba hilo na kuridhika na kutakiwa kuwaamuru kwenda kuandikishiana kwenye ofisi za serikali za mtaa kwa nia ya kupatiwa hati na saini husika kutoka kwenye ofisi hizo.

  Hivyo mara baada ya kufika katika ofisi hizo Mtendaji wa ofisi hizo aliwauliza kuwa walikuwa wamemuuzia shamba gani mteja huyo na kusita kumwambia mtendaji huyo.

  Ndipo mtendaji huyo kumwambia mteja huyo shamba ambalo alikuwa anataka kuuziwa lilikwisha uzwa kwa mtu mwingine na hivyo watu hao waliuza isivyo halali kwa lengo la utapeli.

  Ndipo mtendaji huyo akishirikiana na mteja huyo walipotoa taarifa katika kituo cha polisi na watu hao kuwa chini ya ulinzi na kushikiliwa kusubiria hatua ili waweze kufikishwa mahakamani kwa utapeli.
  </SPAN>
   
Loading...