Mapengo 17
R I P
- Mar 28, 2014
- 1,228
- 618
Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Amani Mwakasege kwa kosa la kuharibu mali kuchana picha ya mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Tukio hilo limetokea Agosti 27, 2015 majira ya saa 14:30 mchana huko Ilomba, kata ya Iyunga, Jijini Mbeya. Inadaiwa kuwa, mtuhumiwa alionekana akiwa amebeba mabango ya picha za mgombea wa urais huku yakiwa yamechanwa vipande vipande na ndipo jitihada za kumkamata zilifanyika na kumfikisha katika Kituo kidogo cha Polisi Ilomba.
Aidha, katika tukio jingine, mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Fadi Mwashimaha anashikiliwa na Jeshi hilo kwa kosa la kuharibu mali kuchana bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 27.08.2015 majira ya saa 12:00 mchana huko Iyunga, Kata na Tarafa ya Iyunga, Jijini humo. Inaelezwa kuwa mtuhumiwa na vijana wengine waliitoa bendera hiyo iliyokuwa juu ya mti na kisha kuichana kwa madai kuwa mti huo uliokuwa umefungwa bendera hiyo ni mali yao.
Watuhumiwa wamefikishwa Mahakamani leo hii kutokana na makosa hayo.
Imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi.