Wawekezaji toka china | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wawekezaji toka china

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Researcher, Jun 27, 2011.

 1. Researcher

  Researcher Senior Member

  #1
  Jun 27, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kuna vita nzito ya kipropaganda inayoendelea baina ya hawa Jamaa wa mashariki ya mbali na wale wa magharibi. Ni ukweli usiofichika kwamba uchumi wao unakuwa kwa kasi ya ajabu na hivyo kuwa tishio kwa ulaya na marekani.. Si kusudii kujadili hilo.

  Ila nimeguswa na uhusiano kati ya nchi yetu na hawa watu. Natambua kwamba nchi yetu inaheshimu haki za binadamu na vilevile ni mwanachama wa jumuiya za kibiashara za kimataifa kama WTO. Zaidi ya hivyo nchi yetu imekuwa na mahusiano ya muda mrefu kiitikadi na kiuchumi. Sote tunafahamu kwamba mwezi januari wachina waliamrishwa kufunga virago na kurudi kwao. Sijaweza kufuatilia hatma ya sakata hilo. Hata hivyo pamoja na kwamba amri ile ilikuwa na mapungufu yake, ni ishara kwamba serikali imeanza kuona kuna tatizo.

  Tayari mambo kadhaa yameshajidhihirisha;
  1. Kwamba kuna uwepo wa wachina wanaofanya kazi nchini bila vibali au kupitia njia zisizo halali
  2. Kwamba kuna wachina wanaofanya kazi ambazo watanzania wanaweza kuzifanya na hivyo kukuza tatizo la ajira nchini
  3. Kwamba kasi ya kuongezeka wachina ni kubwa na swala hili lisipowekewa mkakati itakuwa tishio kwa uchumi wa nchi yetu

  Nimegundua kwamba kuna mengine ambayo yamekuwepo kama tetesi na yanahitaji utafiti kupata ushahidi;
  1. Kuna idadi kubwa ya makahaba wa kichina waliosajiliwa kwa huduma za massage n.k jijini dar es salaam
  2. Kampuni za kichina zimekuwa zikitumia udhaifu wa mfumo wetu wa manunuzi na tamaa ya baadhi yetu kujinyakulia zabuni kwa kukiuka taratibu
  3. Nguvu ya wachina nchini inazidi kuimarika na wakati mwingine wanakuwa wababe kwa wazawa
  4. Kuna viwanda vya wachina visivyotambulika na serikali nchini. havilipi kodi na ambavyo vinachochea kasi ya kuongezeka bidhaa feki

  Lakini vilevile nimegundua mambo kadhaa ya mazuri kuhusiana na wachina;
  1. Wachina ni watu hodari wa kufanya kazi na tunaweza kujifunza mengi katika utendaji wao. Mfano vijana waliofanya kazi kwenye gereji za wachina wakiwezeshwa wanaweza kuwa wajasiriamali wazuri sana.
  2. Mazingira ya awali ya uchina ni sawa na ya kwetu ya sasa na hivyo tuna mengi ya kuiga kuhusiana na maendeleo ya viwanda toka kwao
  3. Misaada ya wchina haina longolongo kama ya ulaya na ajenda kubwa kwao ni ajira kwa watu wao kwenye miradi yao.

  Hata hivyo bado tunahitaji kujipanga zaidi katika swala hili;
  Tunaweza kuhamisha teknolojia toka kwao kuja kwetu, mfano viwanda
  Tunaweza kujifunza mbinu na namna wanavyofanya kazi kuimarisha uwezo wa ndani
  Tuanze kuuhakiki mfumo wa vibali vya kazi, na mianya yake ili kulinda ajira zetu
  Ikibidi tuimarishe mwenendo wa uzalendo katika manunuzi binafsi ili pesa yetu izunguke ndani isiishie nje ya nchi.

  Kama kuna mengine wadau nitafurahi kupata michango yenu.


  Angalizo:
  Ikumbukwe kwamba nchini kwao pia kuna weusi wengi wakiwemo watanzania
  Bado wachina hawajajikita (mfano madini na nishati) kwenye mikataba yenye kutuletea hasara kubwa kama wasauzi na nataifa mengine.
  Binafsi siwachukii wachina ila najaribu kuona na sisi tunanufaika na uwepo wao nchini.
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mada nzuri, cha msingi watanzania tumezoea vijiweni badala ya kukaza buti katika utendaji. Mwingiliano wa mataifa mbalimbali ndio njia bora ya kukuza uchumi, kwani tuna mengi ya kujifunza toka kwao, na nchini kwako makampuni yatavutwa kuja wekeza kwa vile kuna watu wao na pia wazawa kupata nafasi za ajira.

  Tukiangalia mataifa yaliyopaa sana kwa teknolojia na uchumi wa kutegemea viwanda ni mataifa ambayo yalikuwa na mwingiliano wa kimataifa hasa yaliyokuwa na makoloni au kuwa na wahamiaji wengi kutoka nje. Mabadiliko hayo yanasaidia sana na kama tunafunguka akili tutajifunza mengi kutoka kwao. Afrika kusini imeendelea sababu ya wahamiaji toka mataifa ya ulaya. China yenyewe iliruhusu mfumo wa biashara ndani ya taifa la ujamaa kama miongo michache tu iliyopita na leo ni taifa la pili tajiri duniani baada ya Marekani, japani imeshapigwa kikumbo na China.

  Kasoro haziwezi kukosekana, lakini tuwe wapembuzi wa kuangalia manufaa ya kiuchumi. Kuwafukuza wachina sioni kama suluhisho vinginevyo kama wanafanya mambo yasiyoweza kuvumilika kama uvunjaji wa amani. Watanzania wengi wako mataifa ya nje na wanaishi kinyume cha sheria ingawa kuna wanaoishi kihalali, lakini jambo hilo linaangaliwa kwa misingi ya kibinadamu zaidi,
   
 3. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #3
  Jun 27, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mawazo yako ni mazuri lakini swali la kujiuliza ni hi: Wazawa watafaidikaje na teknolojia ya hawa wazee wa mafeki ktk miradi yao wakati kuanzia engineeers hadi wabeba zege wanatoka China, na wabongo wanabaki kuwa mamessengers na wafungua mageti au watazamaji? Huu ndio uwekezaji makini?
   
 4. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #4
  Jun 27, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kama ni wawekezaji kwa wachina hawa wa sasa walioko Tanzania ni hasi [Fake]. Ni kweli tuanitaji kupata technolojia,Ila uamishaji wa nama hii ya uwekezaji ni kilio,wanaamisha pesa nyingi sana kwa mfumo wa dola.

  Nilipenda tutumie njiaa ya kuamisha teknolojia kwa mbinu ya miradi mikubwa [Projects] kama vile Mwalimu alitumia ujenzi wa reli,migodi ya makaa ya mawe kiwila Mbeya. Na Rais Mkapa yeye aliwatumia kwenye miladi kama uwanja wa Mpira na ujenzi wa mabarabara.

  Uendeshaji wao kwa haraka ukiangalia utafikili kuwa hauna madhara ukizingatia wanaonekana kuwa karibu na watanzania wakiishi mitaani tofauti na ndugu zetu wa kihindi na kiarabu.Lakini wameingia katika biashara za uchuuzi na hivyo kualibu mfumo wa wananchi wetu wa kufanya biashara kwa kushindwa kushindana na wachina ambao wao bei zao ni za chini.

  Wameua gereji za wazawa na kwa kuwa Mtanzania haswa rika la wau wenye kipato bado tuna ulibukeni wa kuthamini mgeni kuwa anachokifanya ni bora kuliko mwenyeji.Walipo anza walijitahidi kuwa wanyooshaji wazuri wa magari siku hizi wanaletewa gari garage kwao kisha wanapelekwa kwa mswahili wanayeamini ni mzuri kwenye kunyoosha ama kupiga rangi.

  Hivyo napingana sana na uwepo wa hawa jamaa kwa sasa Nchini wameenza kuwa kero huku mitaani,usanii na kama tunavyojua teknolojia yao pia wanaichakachua,hatuitaji kuadapt teknolojia ya kujifunza kuchakachua.Tunaitaji teknolojia ya kutondolea kero ya matatizo yetu sio kutuongezea kero.

  Kama ni kufaidika na teknolojia yao tupeleke vijana wetu kwao wakasome kama tunavywapeleka kila baada ya miaka kadhaa.Tuongezee idadi ya vijana kwenda kusoma heavy technology na sio domestic technology ya toi za kichina.

  Serikali ifanye mpango wa kuwaondoa kabla awajaanza kuunda mifumo yao ya umafia wa kichina,wameanza na dada zao kujiuza hapa nchini na hilo liko wazi halina kificho magazeti ya Global Publishers ya Erick Shigongo kila siku yanatuonyesha wanavyojiuza na wapi.Je serikali inajua kuwa mfumo wa wanawake hao haswa wa kigeni unaambatan na biashara haramu za kibabe [umafia ingawa sio jina sahihi kwa kuwa limezoeleka kwa kutegemea na genge lenyewe ni la aina gani,kuna Yakuza n.k].Je mpaka sasa hawa Malaya wa kichina mmilki wake ni kundi gani la kichina,bado nimapema sana.Tuwai kabla hawajajiimarisha itakuwa taabu hata kwa watawala wenyewe siku za mbele.

  Mfano wa ubabe ambao si umafia ila ni silka ya kichina ulifanya na hawa jamaa dhidi ya watawala wetu wa jeshi la polisi walipo pigwa na kundi la wachina, wasingekuwa wananchi kuingilia kati kwa kuona viongozi wa polisi wanapigwa sijui hatima yao ingekuwaje.Kupitia tukio hili pata picha wawe na magenge ya kiuni na ubabe mitaani kitakachofuata.

  Kibongo bongo unaweza mkopa dada yetu pale mitaa ya Kinondoni,Obey Maisha au Bills,Je ukimkopa dada yao kitakachofuata nini?.Amini ukweli wachina huwa hawapendi waswahili muwadandie dada zao, kwa waliosomo China wanakwambia wakikunasa unawaduu dada zao watakufanyia kitu mbaya si kinoma.

  Ukitaka kujua ukali wa hawa jamaa watizame pale wanapovamiwa na chombo cha habari, wengi wetu uwa tunaona kwenye luninga mtafauruku,hata kama ni dola imeenda pale bado mchina atawapa makashikashi pamoja na kuwa anamakosa.

  Serikali iwaaondoe iwaludishe kupitia miladi [Project] kitu ambacho itakua rahisi kuwathibiti na pia wanakua wanaishi nchini chini ya mpango wa mladi.Uwepo wao huu wakimagutugutu wataanzisha mitandao yao kuwadhibiti kwenye matendo yao kialifu itakua kazi,ukizingatia wanavyofanana na ujuzi wao ambao kwetu itakuwa ni utamaduni mpya.
   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  Jun 27, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Uchumi wa China unakua kwa haraka sana kwa sababu ya Marekani kuwatunza kama Most Favored Nation (MFN), hali iliyoanza tangu mwaka 1994 ikiasisiwa na Rais Clinton. Wakiamua kuwawekea ngumu kwa mwezi mmoja tu, utaona uchumi wa china unapungua kasi kwa haraka sana na hata kukwama.
   
 6. zaratustra

  zaratustra JF-Expert Member

  #6
  Jun 27, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 849
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Mkuu hapo kwenye red, nina wasiwasi napo!
   
 7. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #7
  Jun 27, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Haya Mataifa mawili Marekani na China wanachezeana foul kubwa sana kama kawaida ya Marekani,Manake hofu kubwa ya Mmrekani ni population ya China.na kama isingekuwa ni hiyo idadi ya watu, China ingekuwa iko kwenye list ya Marekani kama Russia kuondolea makali ya kuwa strong Nation.

  Lakini muda utasema makali ya Marekani juu ya China yatachomoka na uenda wakawapatia wapi pa kuwadumaza.Uzuri wa china wanahakikisha Marekani hapenyi katika Serikali yao.Na hili uwe kiongozi China lazima kweli uwe ubongo wako unachemka kwa kwenda mbele.Na kama ukimess up wanakupoteza chini ya msemo wao kwa faida ya kuhujumu umma wao.
   
 8. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #8
  Jun 28, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Una wasiwasi lakini huenda huna uhakika sawasawa. MFN status ya China ilikuwapo siku nyingi sana tangu miaka 1930, ila ilifutwa mwaka 1951 kutokana na kitendo chake kuivamia Tibet. Ilirudishwa tena conditionally mwaka 1980, na baadaye ikapunguzwa makali (karibia kufutwa tena) mwaka 1989 kutokana na mauaji ya Tiananmen square. Mwaka 1994 ndipo China ilipoleta ujumbe wa nguvu sana kwa rais Clinton kuja kuomba MFN statsus iimarishwe, ingawa Congress iliweka sharti kuwa statsu hiyop iwe inakuwa revised kila mwaka, lakini iliimiarishwa sana.

  Ni kutokana na kuimarishwa huko ndipo China ilipojipatia soko kubwa sana la marekani huku makampuni mengi ya Kimarekani yakihamisha opersheni zao kwende china kwenye cheap labour. Mzunguko huo wa China kuuza sana Marekani na makampuni ya marekani kuhamia china kulichangia sana kuua manufacturing sector ya marekani, na ndiyo maana hadi leo huko Ohio bado watu wanalia na kusaga meno kwa kukosa kazi kwa viwanda walivyokuwa wakifanyia kazi generatina na generation vilihamia China.
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wachina kuingia bongo ni tofauti kama mataifa mengine ya kiafrika au ya nchi za magharibi. Wachina wanaishi isolated, hawako social kama watu wa mataifa mengine. Kati ya watu wa asili ya Mongolian wachine wana tabia ya peke yao tofauti na wakorea, wavietnam nk. Na kama mtu ameingilia himaya yao hawa ni chui hawana huruma. Hali hii inatokana hali ya siasa za kukandamizwa sana nchimi mwao.

  Na wachina wengi wanaobahatika kutoka nchini mwao kwenda nchi nyingine wanajiona kama wamefunguliwa minyonyoro ya utumwa nchini mwao. Wamezagaa nchi nyingi, na nitaifa linaloongoza duniani kwa umachinga. Nimewashuhudia katika miji mikubwa duniani wamachinga wa kichina hasa wanawake wakifanya umachinga bila woga wakati wenyeji hawafanyi hivyo, ama kwa kweli wingi wao umewapa risk ya kujituma isivyofikirika.

  Wachina wakianzisha makampuni yao au biashara zao huwa ni wabinafsi, hawapendi kuwaajiri wazawa, ila huajiriana wao kwa wao, na kama wanahitaji watu zaidi huagiza wengine toka kwao waje kufanya kazi kwenye makampuni au biashara zao. Ila khofu tuongoe maana hakuna binadamu mkamilifu. Biashara zao zinafungua milango zaidi ya kiuchumi nchini mwetu na yamkini watalipa kodi pamoja na kuvusha pesa wanazofuna hapa. Uchumi mzuri pia hutegemea na mzunguko wa pesa, hivyo mahusiano ya biashara hii yanapanua wigo wa mzunguko wa pesa.
   
Loading...