Wawakilishi wataka uwiano katika Muungano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wawakilishi wataka uwiano katika Muungano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Jun 19, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Posted on June 18, 2012 by zanzibaryetu
  [​IMG]
  Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud akibadilishana mawazo na Muakilishi wa Mji Mkongwe Ismail Jussa Ladhu ndani ya Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi huko Bweni Nje ya Mji wa Zanzibar.

  WAJUMBE wa baraza la wawakilishi wametaka uwiano sawa katika nafasi za juu za Muungano izingatiwe uteuzi wa wazanzibari ili kutoa haki sawa kwa pande zote mbili. Baadhi ya wajumbe wa baraza la wawakilishi wametoa kauli hiyo katika kipindi cha masuali na majibu ambapo walihoji kwa nini nafasi za majeshi na polisi zinashikiliwa na watu kutoka upande mmoja wa muungano peke yake.

  Mwakilishi wa Jimbo la Wawi (CUF) Salim Nassor Juma alisema kutokuwepo na uwiano katiak kushika nafasi za uongozi na nafasi nyeti katika utumishi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ni kero na inahitaji kushughulikiwa.

  Aidha Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni (CCM) Jaku Hashim Ayoub na Mwakilishi wa Jimbo la Mtambwe (CUF) Salim Abdallah Hamad walitaka nafasi ya mkuu wa jeshi la polisi na nafasi ya mkuu wa majeshi ya ul;inzi na usalama ishikwe na wazanzibari.

  Akijibu hoja hizo za wajumbe Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa pili wa rais, Mohammed Aboud Mohammed alisema kwa mujibu wa katiba rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ndio mwenye mamlaka ya uteuzi huo na halazimiki kufuata ushauri wa mtu yeyote.

  "Hata hivyo marekabisho ya sasa ya katiba ambayo yataanza hivi karibuni ni pahala pazuri pa kuwasilisha malalamiko na kutoa mapendekezo juu ya mamlaka ya rais, toweni malalamiko yenu kwa tume na ninakunasihini mfanye hivyo" alisema Aboud.

  Aboud alisema katika uteuzi wa nafasi zote za juu katiba haikuweka vigezo, uwiano wala fomula maalumu katika uteuzi na ni mamlaka aliyonayo mheshimiwa rais ambaye ni pia jemedari mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama.

  Kutokana na kuwepo na hali hiyo Aboud alisema ni wakati mwafaka kwa wananchi pamoja na wajumbe wa baraza la wawakilishi kutoa maoni yao kwa tume ya kuratibu maoni ya katiba mpya inayoanza kazi yake hivi karibuni.

  Viongozi wagoma kuhama nyumba za serikali
  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema inakabiliwa na upungufu wa nyumba za kuishi viongozi wa kitaifa kutokana na tabia ya baadhi ya viongozi hao kutotaka kuhama wanapomaliza muda wao wa uongozi.

  Naibu Waziri wa wizara ya maji Ardhi, Makaazi na Nishati, Muhidin Makame alisema kuwa kwa miaka mingi serikali ilikuwa na nyumba zake za kuishi kiwemo viongozi wa kitaifa lakini matatizo yaliojitokeza ni baadhi ya viongozi hao kuwa na tabia ya kutohama katika nyumba za serikali baada ya muda wao wa uongozi kumalizika.

  Hayo ameyaeleza Naibu waziri huyo wakati akijibu suali la msingi la Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni (CCM) Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua mipango ya serikali katika kuwapatia viongozi nyumba za kuishi na kuepuka gharama za kukodi.

  Alisema jambo jengine ambalo limesababisha serikali kuwa na nyumba pungufu ni uchakavu wa nyumba hizo kutokana na kutokuzifanyia matengenezo kwa muda mrefu.

  "Hivi sasa serikali inaandaa mpango maalumu wa kuzifanyia matengenezo nyumba zote za viongozi ambazo zipo katika hali nzuri na pia kuzivunja kwa zile amabzo zipo katika hali mbaya ili kutoa nafasi kwa ujenzi wa nyumba mpya" aliahidi naibu huyo.

  Aidha naibu waziri huyo aliwataka viongozi wanaomaliza muda wao kuzihama nyumba za serikali ili kuwapisha wengine ili kuondokana na upungufu wa nyumba na kutoa nafasi kwa viongozi wengine wanaoteuliwa nafasi hizo.

  Baadhi ya nyumba za serikali ambazo zinakabiliwa na uchakavu mkubwa ni nyengine kuwa katika hatari ya kuanguka zipo katika maeneo ya mazizini, migombani na chakechake kisiwani Pemba.

  Zanzibar kutengeneza bendera nyingi zaidi
  WAZIRI wa Katiba na Sheria Zanzibar, Abubakar Khamis Bakari amesema jana kuwa serikali inakusudia kutengeneza bendera za kutosha za Zanzibar ili kuondoa upungufu na kuwawezesha wananchi kuzitumia.

  Akijibu suali la Mwakilishi wa Jimbo la Mpendae (CCM) Mohammed Said Mohammed ambaye alitaka kujua kama matumizi ya bendera ni kosa kisheria.

  Naye Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu alihoji upungufu wa bendera za Zanzibar katika visiwa vya Unguja na Pemba ikilinganisha na bendera za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Akijibu masuali hayo Bakari alisema sio kosa kisheria kwa wananchi kutumia bendera ya nchi yao katika shughuli mbali mbali ikiwemo kupachika katika baiskeli au gari au kutumia kwa matumizi ya sheria za nchi na sherehe nyenginezo.

  "Serikali haimzuwiii mwananchi kutembea na bendera ndogo ya Tanzania wala ya Zanzibar kama ataiweka ndani ya gari yake au vyombo vya maringi mawili, hii ni fakhari kuona wananchi wanaipenda nchi yao" alisema Waziri huyo.

  Waziri Bakari alisema matumizi ya bendera yanafanana katika mahala mingi duniani hasa pale ambapo wananchi wanasherehekea kitu Fulani kama vile mpira, siku ya kitaifa na kadhalika kwa sababu hakuna tatizo lolote la kisheria.

  "Kama kuna upungufu wa bendera nitashirikiana na taasisi inayohusika tuweze kutengeneza bendera za kutosha ili wananchi waweze kuzipata na kuzitumia" alisema.

  Hata hivyo katika majibu ya ziada Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Issa Haji Gavu alisema kwa hivi sasa zipo bendera za kutosha na kuwataka wananchi wende wakazinunue ambapo bendera moja inauzwa kwa bei ya shilingi 40,000.

  Zanzibar ilipitisha sheria ya kuwa na bendera yake mwaka 2005 ikiwa sehemu ya kielelezo cha utaifa baada ya bendera hiyo kutokuwepo kufuatia Zanzibar kujiunga na Tanganyika mwaka 1964.

  Chalezo kipya kujengwa Zanzibar
  ZANZIBAR inakusudia kujenga chelezo ambapo meli na boti za kijeshi zitatengenezwa ili kuondoa mchanganyiko wa vifaa vya kijeshi na sehemu za raia.

  Hayo yameelezwa katika kikao cha baraza la wawkailishi kianchoendelea na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Dk Mwinyihaji Makame Mwadini wakati akijibu suali la msingi la Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani (CCM) Ali Salum Haji aliyetaka kujua kwa nini kikosi cha KMKM kimeshindwa kufufua chelezo chake hapa Zanzibar.

  Waziri alisema hivi sasa serikali imo katika mipango ya kuangalia gharama za kufufua chelezo cha KMKM ambacho ni kikosi maalumu cha maji ya Zanzibar.

  "Chelezo cha KMKM kilichindwa kufanya kazi tangu miaka ya 1970 lakini hivi sasa kwa msaada wa jamhuri ya kidemokrasia ya ujerumani tuna mpango wa kufufua chekelezo hicho" alisema waziri Makame.

  Alisema kampuni ya Damen Shipyard kutoka Uholanzi imo katika kufanya upembuzi yakinifu na kuangalia gharama halisi ili kazi iweze kufanyika na kwamba jeshi kuwa na chelezo chake ni muhimu.

  Waziri huyo aliwaambia wajumbe wa baraza hilo kwamba kikosi cha KMKM kutumia chelezo chake kwa ajili ya matengenezo ya boti zake na hasa ikizingatia kanuni za kiusalama.

  Kikosi cha kuzuwia magendo (KMKM) ni miongoni mwa vikosi vitano vya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ambavyo vina majukumu mbali mbali ikiwemo ulinzi na usalama nchini.

  Vikosi vyengine ni Valantia, Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU), Magereza, Kokosi cha Uokozi na Zima moto (KUZ) ambavyo voye vinatambulika kisheria.

  Utafiti wa madini joto ni muhimu
  WIZARA ya Afya Zanzibar imesema itaendelea kusimamia na kufanya uchunguzi wa viwango vya madili joto katika chumvi inayozalishwa na kutumika zanzibar ili kuepuka madhara ya kukosekana kwa madini hayo mwilini.

  Hayo yameelezwa na Naibu Waziri hiyo, Dk Sira Ubwa Mamboya wakati akijibu suali la msingi lililoulizwa na Mwakilishi wa Wawi (CUF) Saleh Nassor Juma aliyetaka kujua nafasi ya wataalamu wa afya katika kushauri matumizi ya madini joto katika chumvi hasa kwa uzalishaji unaoendelea kisiwani Pemba.

  Waziri alisema wataalamu wa wizara yake kitengo cha lishe kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la Unicef wametoa mafunzo kwa vikundi vya uzalishaji chumvi ili kuzingatia uchanganyaji wa chumvi na madini joto.

  Alisema wizara yake imetoa mafunzo kwa maafisa wa afya kusimamia viwango vya madini katika chumvi inayouzwa kwa ajili ya matumizi ya wananchi.

  "wizara ya afya kupitia bodi ya chakula, dawa na vipodozi itaendelea kusimamia na kufanya uchunguzi wa viwango vya chumvi ili wananchi watumie chumvi inayotakiwa" alisema Dk Sira.

  Aidha Naibu waziri huyo amesema wameshirikiana na jumuiya ya wazalishaji chumvi kisiwani Pemba (Association of Zanzibar Salt Prcessing Organisation – AZASPO) ili kuwanunulia madini joto na kuwakabidhi wao kama ni wadhamini na wasimamizi wa vikundi vyote vya uzalishaji chumvi.

  "Lengo la kufanya hivyo wao AZASPO walitakiwa wawauzie wazalishaji na pesa wanazokusanya waziendeleze kwa kununulia madini joto ikiwa ni fedha za kimzunguko (revolving fund)" alisema naibu huyo.

  Kwa mujibu wa wizara ya afya, ukosefu wa madini joto unasababisha matatizo mbali mbali ya kiafya ikiwemo kutoimarika kwa mifupa mwilini na maradhi ya uvimbe shingoni (goiter).

  Zaidi ya bilioni 1.5 zatolewa kwa vikundi
  ZAIDI ya shilingi bilioni 1.5 zimetolewa kwa vikundi vya ujasiriamali Zanzibar hadi kufikia mwezi Aprili mwaka huu kupitia mfuko wa rais Kikwete na Rais Karume.

  Hayo yameelezwa na Waziri wa Kazi, Uwezeshaji Kiuchumi na Ushirika, Haroun Ali Suleiman wakati akijibu suali la msingi la Mwakilishi wa nafasi za wanawake, Mwanaidi Kassim Mussa ambaye alitaka kujua ni wananchi wangapi walinufaika na mfuko huo kwa upande wa Zanzibar.

  Waziri alisema jumla ya mikopo 750 ilitolewa ikiwemo watu binafsi, vikundi vya wajasiriamali, saccos na vikundi vya kiuchumi ambapo sehemu ya fedha hizo tayari zimesharejeshwa.

  "Fedha zilizorejeshwa ni zaidi ya milioni 765,000 hadi kufikia Aprili mwaka huu ambapo ni sawa na asilimia 50. Jumla ya wanawake 170 katika mkoa wa mjini magharibi wamepata mkopo huo kati ya wanawake 276 waliopewa mkopo kwa Zanzibar nzima" alisema waziri huyo.

  Waziri Suleiman aliwaeleza wajumbe wa baraza hilo kwamba waazilishi wa mfuko huo ambao ni marais wa Tanzania na Zanzibar, maarufu mfuko wa JK na AK wanadhamira ya kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuwaendeleza wananchi wenye kipato cha chini ili kupunguza umasikini nchini.

  Mfuko wa JK na AK ambao umeanzishwa mwaka 2005 kwa lengo la kupunguza umasikini na ukosefu wa ajira nchini unaowanufaisha zaidi ni makundi ya akina mama kupitia miradi yao mbali mbali.
   
 2. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=1]‘Kiini Macho' Cha Kuandika Katiba Mpya TZ[/h]Written by administrator // 16/06/2012 // Makala/Tahariri // 3 Comments


  Abdi Salum,
  Unajua kama utafuatilia sana suala zima la Muungano (ukiachilia ule mkataba halisi wa 1964), mazonge yamekuwa mengi, udanganyifu, ujanja na hadaa zinazofanywa na Tanganyika zinachupa viwango – yaani Tanganyika wameilalia sana Zanzibar – wameidhulumu kwa kila hali.
  Mtakumbuka kuwa mwaka 1992/93 ulipoanzishwa mfumo wa vyama vingi TZ, ilipitishwa sheria maarufu Bungeni inaitwa ‘Mabadiliko ya 11 ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa TZ", mabadiliko haya – Ibara ya 11, ndio yalimuondeshea Rais wa Zanzibar kuwa Makamo wa Rais TZ (na kuvunja mkataba wa Muungano wa 1964). Dhulma na ujanja huo.
  Hii haikuletwa BLW wala BLM wala popote pale Zanzibar – Zanzibar kuweza kuijadili na kuipta riadhaa, na hata Wabunge wa Zanzibar wakati ule pia hawakuipigia kura maana walitoka nje na kususa kikao. Spika wa siku zile, Msekwa alisema kwa dharau kuwa ‘ni kweli wabunge wa Zanzibar hawakuipa ridhaa mabadiliko ya ibara hii ya 11 kwa sababu walikwenda kusali'. Mnaona dharau hiyo?
  Hii ya jana na juzi, Mabadiliko ya 8 -2012 ya Katiba eti inaletwa BLW kama ‘taarifa' – hii kali na inaonyesha kini macho cha hali ya juu kwa Tanganyika v.s Zanzibar. Mimi hii sijawahi kuisikia popote duniani kuwa bill /au sheria inaletwa Bungeni/BLW kama ‘taraifa' – dharau ya mwisho!
  Kama nilivyosema ‘bad start or wrong approach haiwezi kuleta good results'.
  Msimamo wa Tanganyika ni kuwa Zanzibar si chochote si lolote; lakini wao wanaitumilia sana Zanzibar kwa kupata tija halisi hasa kipato.
  Mfano, ilipovunjika Jumuiya ya Afrika Mashariki 1977, Edwin Mtei alikuwa Ganava wa Benki Kuu ya TZ; siku zile EAC ilitoa mgao wa pesa kwa Zanzibar tu, ambazo ndizo zilizoanzisha BoT. Msekwa aliandika barua kwa EAC na kudai pesa za ziada na sehemu ya barua yake ilisomeka hivi (roughly) kuwa "….sisi ni nchi mbili tofauti, na mgao mliotupa ni kidogo sana kwa nchi mbili kwa hivyo tunaomba sehemu mgao wa Tanganyika kama nchi…..". Naam, EAC walitoa kasma nyengine kwa ajili yao. Haya leo ni nchi ‘moja'; yakiwepo maslahi – zinakuwa nchi mbili? Kiini macho hicho.
  [naomba mtembelee archive ya Nairobi, Kenya mtaziona na hata katika report ya tume ya Amina Salim Ali ameziweka kama appendix/annex]. Hii report SMZ wameificha maana imefuchua mambo mengi mazito juu ya Muungano hasa kuhusu pesa.
  Msekwa yupo hai, na Edwin Mtei yupo hai – waulizwe kama ni kweli au uwongo, record za barua zipo na record za malipo zipo (unless wazichakachue leo na kesho). JK upo?
  Sasa, tunapodai haki zetu za msingi – iwe UAMSHO au Jumbe, au Maalim Seif na timu yake (enzi zile, sio leo tena), au Kamandoo Salmin au yeyote yule – inakuwa NOMA. WHY?
  Tanganyika wajue kuwa tuna madai mengi kwao, na wajue kuwa hizi ni haki zetu za msingi na sio ‘kiini mamco au lele mama'.
  BLW limepokea mabadiliko ya katiba kama ‘taarifa' huo ndio upumbavu wa mwisho kwao na Wazanzibari.
  Wallah ingalikuwa tuko serious hawa wote wawakilishi wangalipaswa kujiuzulu na BLW kuvunjwa kama kitu ‘constitutional crisis' .
  Kwa nini basi ile ibara ya 11 iliyomuondoshea rais wa Zanzibar kuwa makamo haikuletwa BLW, kwa nini sheria ya kuanzisha TRA 1998/99 haikuletwa BLW na zinafanya kazi hapa Zanzibar kwa mabavu??
  Hata hivyo, haya yote ni makosa yetu – tumezubaa mno; vipi BLW ikubali upuzi huu, vipi Katibu wa BLW, Mh.Yahya Khamis Hamad - tunayemjua sisi akubali comedy kama hii?
  Suluhisho
  Kama kweli JK na serikali yake wana dhati ya nchi ya TZ na hasa Zanzibar – basi bill ile aliyoitia saini irejeshwe AG office DAR ifanyie a small review au mapitio, na iende tena bungeni as an emregency document, bunge waijadili tena – (kidogo tu) na halafu irejeshwe BLW kwa kupata idhini, then aitie saini kama sheria – plus aivunje tume ile fake ya kukusanya maoni, aunde nyengine (kwa sababu hii iliyopo sio halali kabisa, as sheria yenyewe kama ilivyokuwa sio halali).
  Wazanzibari wengi wana shaka na uundwaji wa katiba mpya maana haukufuata utaratibu – lakini jana Maalim seif, VP1 amewatoa ‘shaka' wananchi na kusema kuwa eti ‘tume itafuata kile kitachosemwa na wananchi'. I doubt Maalim Seif – wewe unawajua vizuri wajomba zako akina Kikwete, Pinda, Msekwa, Mwinyi, Mkapa n.k – hawa kukubali HAKI kwao ni mwisho – ndio wameumbwa hivyo na wameumbika hivyo.
  Mimi nitaona ajabu sana kama watachosema Wazanzibari ndicho kitachosikilizwa na kukubalika. I bet! Kwa sbabu watanganyika wameondosha uaminifu kwetu tokea 1964, wao wamechukua nafasi kama ndio wafalme, watawala, mabosi na wakoloni badala ya Mngereza; and not otherwise.
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ah sasa wanataka uwiano na sio "Zanzibar huru"?

  Na wanataka uwiano kwa vyeo au na gharama zake? Kama ni 50/50 tuanze na wizara zooote za muungano kila upande utoea kiasi sawa kuendesha mambo ya ndani, mambo ya nje, ulinzi, science & technology, Makamu wa rais etc. Kwa miaka 48 Tanganyika wamekuwa wanalipa bill zote hizo. Sasa kila mtu alete hela.

  Na pia bill ya umeme ilipwe tafadhali.
   
 4. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 330
  Trophy Points: 180
  Nadhani uwiano katika taasisi mbalimbali za muungano uzingatie pia uwiano wa idadi ya wananchi wa pande hizi.
  Kwa mfano sioni mantiki ya wingi wa wabunge toka baraza la wawakilishi wanao ingia kwenye bunge la muungano,huku watanganyika wakiwa hawana kauli yoyote barazani pa wawakilishi.
   
 5. s

  swrc JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 442
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mbaguzi:llama:
   
 6. J

  JokaKuu Platinum Member

  #6
  Jun 19, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,958
  Trophy Points: 280
  ..wawakilishi wako out of touch na matatizo ya wa-Zanzibari.

  ..badala ya kuzungumzia njia za kutatua matatizo ya ukosefu wa ajira kwa wa-Zanzibari na Tanzania nzima, wao wanazungumzia kugawana nafasi za uongozi.

  ..according to Mashekhe wa Uamsho, wabunge wa Zanzibar walioko ktk bunge la muungano wanalipwa milioni 12 kwa mwezi. hicho ni kipato kikubwa sana ukizingatia udogo wa maeneo wanayowakilisha. pamoja na ukweli huo, wabunge hao hawafanyi jambo lolote lile la maana au msaada kwa wananchi wao.

  ..halafu kuna mwingine eti anazungumzia masuala ya bendera. what about text books kwa wanafunzi? how about madawa mahospitalini? je, kuna mbolea, pembejeo za kilimo, vifaa vya uvuvi?
   
 7. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #7
  Jun 19, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  haka kawilaya ka zanzibar kananikera sana
   
 8. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #8
  Jun 19, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha ha nilidhani wanataka uhuru wa kisiwa chao sasa wanakuja na single ya mgawanyo wa madaraka.
   
 9. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  inakera sana aisee
   
Loading...