Wavutaji sigara kuchunguzwa mapafu madukani UK

Wavutaji sigara kuchunguzwa mapafu madukani UK

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,267
150928121839_smoker_tobacco_addiction_640x360_thinkstock.jpg

Wenye maduka wanapatiwa mashine za scan Kaskazini ,mwa Manchester nchini Uingereza ili kuzuia ugonjwa wa mapafu miongoni mwa wavutaji sigara.

Kwa mara ya kwanza ,mashine hizo zitawekwa katika maduka ,maeneo ya kuegesha magari katika mradi wa jaribio la kwanza unaosimamiwa na shirika la hisani la Macmillan na NSH England.

Wavutaji sigara na waliokuwa wakivuta sigara watapata huduma ya bure ya kuangalia mapafu yao kupitia uchunguzi wa mashine hiyo ya scan.

Eneo la Kaskazini mwa Manchester lina visa vingi vya saratani ya mapafu nchini Uingereza na watu wanaokufa kutokana na ugonjwa huo wameongezeka ukilinganisha na viwango vya ugonjwa huo.

Wagonjwa walio na kati ya umri wa miaka 55 na 74 wana historia ya kuvuta sigara wamesajiliwa katka maeneo tofauti ambapo huduma ya bure ya kuchunguza mapafu yao hufanywa.

Dkt Phil Barber anasema kuwa mradi huo unatoa fursa nzuri ya kutambua saratani pamoja na magonjwa mengine ya mapafu mapema ili kutoa matibabu.


BBC SWAHILI
 
Waingereza wamefika stage ambayo shida za kijamii ni vituko.
 
Back
Top Bottom