Wauzaji wa pikipiki/boda boda hii ni kwaajili yenu

Kaliro X

JF-Expert Member
Apr 18, 2013
749
438
Habari zenu wana Jamiiforums, it has been a while..
Leo nmekuja na hili wazo.

Kipindi cha karibuni bodaboda zimekuja kurahisisha sana upatikanaji wa usafiri hasa hapa Jijini Dar,

Wauzaji wa pikipiki hizi nao walisoma wakazileta kwa wingi ili waweze kukeep up with the demand

Matokeo ya hili kimekuwepo na utitiri mkubwa wa bodaboda kiasi cha kuleta karaha na usumbufu badala ya kuwa suluhu ya adha ya usafiri

Kule Mbeya lilitolewa tamko la kusitisha usajili wa hivyo vyombo kwa muda kwasbb ya kero iliyopo kwa wasafiri na wateja

Mfano ukishuka tu kwenye mwendokasi pale Gerezani Kariakoo unajikuta umezungukwa na bodaboda kama watano wamekuzibia njia wote wanataka uwe mteja wao na kuna wakati utakuta wanagombana wao kwa wao kwa maneno makali kugombea wateja.

Cha ajabu suppliers wa hizi bodaboda nao wanazidi kuziagiza na kwasasa utashuhudia nyingi zipo tu madukani zinapgwa vumbi hazina wanunuzi na huenda kwa jinsi teknolojia inavyokwenda kasi ikaja teknolojia mpya anytime soon ikawalamba hasara..

Ok ok, nina USHAURI:
Mnaonaje kama mkianza kuwaza kuagiza sasa bodaboda zinazotumia umeme EV-bikes ili kuendana na kasi hii, kama una stock ya bodaboda 100, toa zote agiza hata 50 tuu ambazo una uhakika hata zikikaa showroom kwa next 5-10yrs bado utaweza kuuza..

Anyways..
KAMA KUNA MUUZAJI YEYOTE WA BODABODA kwa ajili ya kuendea kazini TVS AU BOXER X125 NAHITAJI KUNUNUA KWA MKOPO, NIMLIPE 1M CASH THEN INAYOBAKI NITAMLIPA KWA INSTALLMENTS KWA MIEZI 3

Napatikana Kariakoo
TUWASILIANE DM au KWA 0715168802, kwa details zaidi..
 
MKUU NAHISI MWENGE KUNA MAKAMPUNI YANATOA PIKIPIKI KWA MKOPO UNAOHITAJI JARIBU KUULIZIA WADAU WANAOJUA ZAIDI
Shukran mkuu, ngoja waje hapa kama wengine wapo humu.. au wenye connection wanipe
 
Sisi ni kama Kenge, mpaka tutokwe na damu sikioni....jamii yetu yote akili zinachaji kidogo sana tofauti na jamii zingine.
Fikiria mpaka lini hizo boda za Umeme zitaanza kuingizwa hapa nchini, juzi kwenye bajeti ya Mh. MWIGULU alisema msamaha wa kodi kwa vyombo vya usafirisaji inayotumia umeme vitakazoingizwa hapa nchini.

Cha kushangaza, hapakuwa na any project ya kuanza ujenzi wa charging points hapa nchini.
Japo mimi Sina mtaji wa jamani...wenye mitaji changamkieni fursa.
 
Sisi ni kama Kenge, mpaka tutokwe na damu sikioni....jamii yetu yote akili zinachaji kidogo sana tofauti na jamii zingine.
Fikiria mpaka lini hizo boda za Umeme zitaanza kuingizwa hapa nchini, juzi kwenye bajeti ya Mh. MWIGULU alisema msamaha wa kodi kwa vyombo vya usafirisaji inayotumia umeme vitakazoingizwa hapa nchini.

Cha kushangaza, hapakuwa na any project ya kuanza ujenzi wa charging points hapa nchini.
Japo mimi Sina mtaji wa jamani...wenye mitaji changamkieni fursa.
Hahah. Mkuu una hasira nao sana hawa jamaa..
Na nmesikia tuna mgodi wa maji ya betry tupo kwenye negotiations na Elon Musk alete EV za Tesla huku
 
Nenda mwenge mpakani kachukue boda boda hata 5 kwahyo milioni yako. Panaitwa WATU
Hawa WATU Ukikaribia kumaliza mkopo wanakutengenezea mazingira ya kuiba hiyo bodaboda. Wanazi track. Hapo Kenya wanafahamika vizuri tu kwa uhuni wao
 
Back
Top Bottom