Wauza mafuta wachekelea viwango vya faini za Ewura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wauza mafuta wachekelea viwango vya faini za Ewura

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Feb 12, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,572
  Likes Received: 5,760
  Trophy Points: 280
  Wauza mafuta wachekelea viwango vya faini za Ewura
  Na Jackson Odoyo

  MIEZI miwili baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Madini nchini (Ewura), kupewa meno kwa ajili ya kuwadhibiti wafanyabiashara wa mafuta wanaovunja sheria, imegundulika kuwa adhabu zinazotolewa kwa wafanyabiashara hao ni ‘ kama cha mtoto’


  Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi tangu Ewura ilipoanza kutekeleza sheria hiyo mapema mwaka huu, umegundua kwamba wafanyabiashara wa mafuta wanaokiuka sheria wanao uwezo mkubwa wa kulipa faini mara moja na kuendelea na kazi kama kawaida.


  Kwa kipindi cha Januari hadi sasa Ewura imevinasa vituo sita vikikiuka sheria za biashara ya mafuta, lakini wamiliki wa kampuni hizo walilipa faini bila wasiwasi wowote ndani ya siku moja na wengine kuonekana wakiwa na furaha tele.


  Kwa mujibu wa sheria na kanuni za adhabu, wafanyabiashara wa mafuta wanaokiuka sheria wanatakiwa kutozwa faini ya Sh3 milioni kwa mara ya kwanza na endapo kampuni itakamatwa kwa mara ya pili itatozwa faini ya Sh 5milioni pamoja na kufungia kituo kwa miezi 12.


  Kipengele cha tatu cha kanuni za sheria hiyo kinasema endapo wafanyabiashara hao watakamatwa kwa mara ya tatu watanyang’anywa leseni ya biashara na kufungiwa wasifanye biashara hiyo tena nchini, adhabu hiyo pia inawahusu wenye magari ya kusafirisha mafuta.


  Kwa upande wa waagizaji wa mafuta watakaobainika kuvunja sheria watatozwa Sh5milioni kwa kosa la kwanza na akirudia tena kosa lilelile atatozwa Sh10milioni pamoja na kufungiwa kwa miezi 12, lakini akikamatwa kwa mara ya tatu kwa kosa lilelile atapokonywa leseni yake ya biashara na kufungiwa milele.


  Adhabu hizo zinaonekana kuwa kiduchu kwa wafanyabiashara za mafuta ambao wengi wanasemekana ndio matajiri wa ‘dunia’.


  Godwin Samwel ,ambaye ni Meneja masoko wa Ewura, alipoulizwa kuhusiana na udogo wa faini hizo alikiri na kufafanua kwamba adhabu hizo zinaonekana wazi hazina ubavu kwa wafanyabiashara hao.


  “Ni kweli kwamba faini hiyo ni ndogo sana ikilinganishwa na uzito wa kosa ingawa kabla hatujapokea fedha za faini , tunahakikisha kwamba mafuta yote yaliyokuwa ndani ya matenki yanaondolewa na kuwekwa mengine baada ya siku kadhaa tunarudi kupima mafuta hayo na tunafanya ukaguzi huo kwa siri kubwa lakini bado wanaweza kurudia tabia hiyo”alisema Samwel.


  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madani, William Shellukindo alipoulizwa juu ya kugundulika kwa udogo wa faini wanaotozwa wanaokiuka sheria ya biashara ya mafuta alisema upo uwezekano mkubwa kwamba kipengele cha adhabu kwa watu hao ni ndogo ikilinganishwa na uwezo wao na aina ya makosa wanayoyafanya.


  “Ninakushuku kwa kuniuliza swali hilo kwani ni swali zuri na linapaswa kufanyiwa kazi kwa maslahi ya wananchi”alisema Shellukindo na kuongeza,.


  “Kwa kuwa na sisi Kamati na Wabunge wengine tumeshaliona hilo, hatua ya kwanza tuliochukuwa ni kumweleza Waziri wa Nishati na Madini ili aandaye mapendekezo kuhusu marekebisho ya kanuni hizo”.


  Alisema Kamati yake inapendekeza adhabu hiyo ianzie Sh10milioni kwa kosa la kwanza.
   
Loading...