Hivi EWURA wana mamlaka ya kufuatilia haya TANESCO kama wanavofatilia uhaba wa mafuta?

ozark

JF-Expert Member
Dec 31, 2021
629
1,581
EWURA ni "regulator" wa nishati ya aina yoyote hapa nchini,umeme,maji,gesi,mafuta n.k. Na ndio wapangaji bei,na kuna muda huwa wanaigomea hata TANESCO kupandisha bei.

Sasa najiuliza kwa kipindi hiki ambacho umeme unakatika katika ovyo nchi nzima,kwa maana kuna uhaba wa umeme,ningetegemea EWURA wangejitokeza na kuwataarifu wanachi shida ni nini,na ikiwezekana iwakemee TANESCO na idara za maji kama walivofanya kwa vituo vya mafuta,ikiwezekana kuwapiga faini,kama REGULATOR.

Au kwa umeme na maji ni upangaji bei tu?
 
Wataanzaje wakati na wao ni Serikali

Serikali haiwezi kujiratibu kamwe ila kuwaratibu wengineo
 
Back
Top Bottom