Watz Tulimwelewa Mzee Ruksa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watz Tulimwelewa Mzee Ruksa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sumba-Wanga, May 18, 2012.

 1. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Sina hakika kama Kweli watanzania tulimwelewa Rais wa Awamu ya pili alipokuwa anasema RUKSA!

  Mzee mwinyi alichukua nchi ambayo uchumi wake ulikuwa karibu ku collapse.
  Mishahara kiduchu, hakuna sabuni, mafuta ya kupikia, sukari, dawa za mswaki, e.t.c.
  Watanzania walikuwa wanatamani kuwa na rubber mtoni, jeans (wrangler) na mengine mengi.
  Wakati ule ilikuwa ni kawaida upanga foleni ya mahitaji muhimu kwa kuweka jiwe..
  Kila kitu kilikuwa hakipatikani, Tanzania was almost a living hell!
  By that time, Kenya ilikuwa kama London.

  Ujio wa Mwinyi ulikuja na mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kijamii.
  Biashara za cross border zilishamiri, maduka yalijaa bidhaa ambazo hapo mwanzo hazikuwepo.
  Most of the people wakaona kwamba kufanya bishara ndio deal.
  Huu ndio muda ambao wafanya biashara wakubwa kama Dewji, Gulamali na wengine walijitokeza kwa wingi.
  Nakumbuka Bwana Joe Mzuwanda aliwahi kununua picha ya Rais kwa 1,000,000 (mwaka 1989/90) kwenye hafla ya chakula cha kuchangia ambacho mzee RUKSA alikuwa mgeni rasmi.

  Wafanyakazi wa serikali wenye vipato vidogo waliendelea kutamani vitu vilivyojaa madukani....
  ndipo Mzee mwinyi aliporuhusu (RUKSA) "informal activities" za kufuga kuku, ngombe, bustani ili kujiongezee kipato.

  Vile vile, kipindi hicho, watu walizidisha matumizi mabaya ya ofisi za serikali na mashirika kwa kujilimbikizia mali kwa wingi.

  Wizi kwenye ofisi za Uma ukawa ni jambo la kawaida kwa kupewa jina la RUKSA.
  Ni kama alianzisha mbio za marathon kwa watu kupora mali za uma.
  Hali hii inaendelea kwa kasi hadi leo.
  Mtu asiyepora mali za uma anaonekana ni mshamba aliyeshindwa kutumia ofisi yake.
  Ufisadi umekuwa jambo la kawaida na sifa,.

  Nikiangalia hali ya sasa na kasi ya ufisadi, Nimekuwa najiuliza, hivi Watanzania tulimwelewa Mzee Mwinyi aliposema RUKSA?
   
Loading...