Watz ovyo kabisa!!!!!

oba

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
310
65
Hivi inakuwaje serikali inafukuza madaktari wanaowatibia pneumonia na malaria zenu pale mhimbili na ninyi mmenyamanza kimya? watawala wakiugua wanapanda pipa, ninyi mkiugua mnakimbilia mhmbli ambapo mama nyoni(katibu wizara ya afya) amefukuza madaktari, nani atawatibu huko? kilichofanywa na wizara ya afya ni kama kumwaga uji wa mgonjwa mahututi, kipi kitatokea?si watz, si wanaojiita wanaharakati, si profesionals; wote waoga!!!kwa nini wananchi msiwape kampani hao madokta wanaonyanyaswa na kuingia barabarani kuandamana hadi wizara ya afya? mbona nchi nyingine kama nigeria, kenya n,k wanaungana na kuandamana linapokuwa swala la kuhatarisha maslahi yao? kwani nani amewaloga watanzania hata kuwa kama mbwa aliyemwona chatu?tunaliwa huku tukiwa macho na akili zetu, ama kweli lakuvunda halina ubani!!!!!!!!!
 
Shida yetu sisi hatuangaliagi tulipojikwaa bali kulaumu tulipoangukia. Serikali haiwapi wataalam wetu stahiki zao, TUPO KIMYA. Wataalam wakigoma kututibia kuhara kwetu na magonjwa ya zinaa, tupo wepesi kuwalaumu HAWANA UZALENDO. Hivi ni nani aliyesababisha. serikali inayowanyima haki zao au wao ambao wanajitetea?

Huu ndio mzigo wa kukosa elimu. Naunga mkono hoja
 
Hivi inakuwaje serikali inafukuza madaktari wanaowatibia pneumonia na malaria zenu pale mhimbili na ninyi mmenyamanza kimya? watawala wakiugua wanapanda pipa, ninyi mkiugua mnakimbilia mhmbli ambapo mama nyoni(katibu wizara ya afya) amefukuza madaktari, nani atawatibu huko? kilichofanywa na wizara ya afya ni kama kumwaga uji wa mgonjwa mahututi, kipi kitatokea?si watz, si wanaojiita wanaharakati, si profesionals; wote waoga!!!kwa nini wananchi msiwape kampani hao madokta wanaonyanyaswa na kuingia barabarani kuandamana hadi wizara ya afya? mbona nchi nyingine kama nigeria, kenya n,k wanaungana na kuandamana linapokuwa swala la kuhatarisha maslahi yao? kwani nani amewaloga watanzania hata kuwa kama mbwa aliyemwona chatu?tunaliwa huku tukiwa macho na akili zetu, ama kweli lakuvunda halina ubani!!!!!!!!!
Na nyinyi madaktari walimu wakigoma nanyi kimya wakati vigogo wakiwasomesha watoto wao abroad
 
Oba naomba kujua wewe hapo umefanya nini? Umeenda mtaani uka mobilise watu kua you have to take action? Kuna la zaidi umefanya zaidi ya kulalamika kijiweni na kuipost hapa JF? Samahani kama nitakua nimekukwaza, ila napenda nijue... Then nina mchango zaidi....
 
Nadhan itabid wagonjwa tugome nasisi kutibiwa na madaktari wasio lipya stahiki zao. halaaaa
 
..Chadema wakiandamana kudai hayo ulioyasemea, wewe utakuwa mmoja wa wanaosema Chadema wanataka kuchukua Nchi kwa kumwaga damu, kwa sababu kila Mtanzania sasa hivi analalamika, si Viongozi si Wananchi, kila mtu analalamika, Nchi haisongi mbele tunapiga mark time.
 
oba achana na hao wanafiki, Tanzania bado sana katika safari ya mabadiliko mfano mzuri ni dr mwakyembe hataki hata kusema kinacho msibu, mfano mzuri ni wanafunzi wa vyuo hugomea maslah yao tu miaka yote, mfano mzuri madaktari hawawezi kugoma gharama za matibabu ziko juu mwananchi wa kawaida hawezi lipa, mfano mzuri wabunge wanapandisha posho zao sio mishahara, mfano mzuri ni walimu wanagoma kwa malimbikizo yao sio malipo ya dowans. Mwisho kila mtu atajiju kivyake. Ina discourage sana, bt will do something big pretty soon! I love my country and my people better dying trying than never!
 
@Oba, statement yako iko too general. Pia inawezekana watanzania wengi hawajaingia mtaani kuwaunga mkono hawa madaktari waliofukuzwa kwa sababu hakuna 'coordinator' wa hayo maandamano. Unaonaje ukachukuwa hilo jukumu?
 
Wananchi legelege huchagua viongozi legelege wanaounda serikali legelege inayoendesha mambo ya msingi kilegelege na kusababisha huduma za msingi kuwa legelege
 
watanzania legelege waliichagua ccm na haijawafanyia lolote la maana,kuna jamaa mtaani kwetu hataki kusikia unaisema ccm vibaya,lakini maisha yao ya ufukura mkubwa
watanzania wanataka uhuru wa bure bila kumwaga damu
 
kwani wewe umefanya nini so far! au wewe si mtz!! Hivi umewahi kuwajoin wanasiasa hasa wa upinzani wanapodai haki?
 
Siku wakiumwa wataona ukweli na siku ukweli ukiwauma wataona wanapoumwa na kuchukua maamuzi magumu. Hao watanzania si hovyo bali ni zaidi ya hapo. Ukondoo na ukuku vinawasumbua.
 
Wa tz wengi hawawezi kuunganisha chains za tukio kwamba limetokea hili litasababisha lile na lile, wanashindwa hata kuriakti kwa yale yanayo wagusa direct sembuse hilo? Amini amini nakwambia baada ya kuondoa kodi ya kichwa watnzania wengi wanajua kuwa ntanzania halipi kodi!
 
Tuanze kwa kuwapa chadema nguv kwanza..maana ndo point yetu ya kuanzia
 
kwani nani amewaloga watanzania hata kuwa kama mbwa aliyemwona chatu?
Tumelogwa na muasi-si wa tanganyika huru kwa kuwaaminisha wa tz wazee wa magamba ndio mzazi wao naye leo hayupo!
 
Tatizo watu wa Dar ni waoga wa mtutu wa bunduki na mabomu ya machozi sijapata kuona.
Tunaomba Muhimbili hosp. ihamishiwe Arusha muone moto wa machalii wa Arusha!
 
Back
Top Bottom