WaTZ 80,000 kufikishwa mahakamani

Shine

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
11,481
1,364
WaTZ 80,000 watafikishwa mahakamani kwa kutolipa mikopo ya elimu ya juu

Source BBC
 
WaTZ 80,000 watafikishwa mahakamani kwa kutolipa mikopo ya elimu ya juu

Source BBC
Serikali imechemsha. Tunatoa mikopo tupate wasomi wataalam wamalizapo ajira hakuna kwa vile serikali inaruhusu wageni kushika nafasi zote za kazi. Hata wale wachache wanaopata ajira mishahara inasikitisha na haimfikishi robo ya mwezi! Katika mazingira ya namna hizi nani atalipa mkopo wa Bodi? Kama ni kushitaki watashitaki mamia ya maelfu ya waTz. Serikali inatakiwa ijenge na kutumia wataalam wake kikamilifu kwa kuweka mfumo wa fedha za mikopo ya elimu sambamba na kusimamia ajira za wahitimu pamoja na viwango vyao vya mishahara ya chini kulingana na taaluma na madaraja yao. Hali ilivyo hivi sasa msomi wa chuo kikuu usishangae akalipwa mshahara mdogo kuliko mtoto wa bosi mmiliki wa kampuni hata kama hakusoma kabisaaa.
 
WaTZ 80,000 watafikishwa mahakamani kwa kutolipa mikopo ya elimu ya juu

Source BBC


Kurejesha mikopo ni jambo jema kama hujawekewa vikwazo/mizengwe katika shughuli unayoifanya.

Kinachonikera mimi ni kwa nini baadhi ya watanzania waliofaidika na kusomeshwa bure tangu tupate uhuru hawakushirikishwa katika kutunisha mfuko wa bodi ya mikopo ya elimu ya juu, wakati wengi wao ndio walioifilisi serikali mpaka ikashidwa kutoa huduma muhimu ya elimu bure kwa wananchi wake.
 
Na mafisadi je?

Mimi nadhani serikali inapaswa kuilea bodi ya mikopo kwa kiasi kikubwa kwanza kabla haijaweza kusimama yenyewe. Ninachoona hapa ni kwamba huenda imefika sehemu ikaachiwa mzigo kama ilivyo kwa TEMESA na vivuko vya Kigamboni n.k. Wanabaki kutapatapa sasa wapate wapi hela.

Kwa ufupi, la kuwashitaki watanzania halitakuwa na tija. Waanza na kuiomba serikali ifanye mabadiliko ya ki-sera kwanza kuhakikisha kila mnufaika mkopo ana nafasi kubwa ya kupata ajira mara tu ahitimupo masomo yake. Soko la ajira lilindwe kikamilifu na pawepo mazingira bora ya kazi.

Nawasilisha wakuu.
 
Hakimu atakayesikiliza kesi zao sina hakika kama yeye mwenyewe atakuwa amerudisha mkopo.

Ze semu tu mawakili na makarani.
 
Serikali haina priorities kabisa.Nadhani wanajaribu ku-divert attention na kunyamazisha wasomi,kwa kuwa wao ndio wanaoipigia serikali kelele kuhusu udhaifu wake.Frankly logic ya kufanya kitu kama hiki siioni.Serikali yenyewe ina ubavu gani wa kumnyoshea anybody kidole kwamba ana kosa.Ingejisafisha kwanza uovu wake ndio iweze kuwajibisha wengine,otherwise huu ni uonevu mtupu.Hivi hata lini watanzania tutaendelea kudhalilishwa na hawa watu huku tukiangalia?Wao wameiba ngapi?Sisi hatujaiba,ni mkopo ambao tumeshindwa kulipa kwakuwa hatuna ajira,which is a very valid reason,na wao ndio wameharibu uchumi wa nchi tena makusudi, kiasi cha ajira kukosekana.
WaTZ 80,000 watafikishwa mahakamani kwa kutolipa mikopo ya elimu ya juu

Source BBC
 
Duh,,mh mh naomba tuanze na watu waliopata tangu 1961,,kuna special tribunal kwa ajiri ya hili au tutatumi hizihizi mahakam zetu ambazo wengi wa waajiliwa wao ni wadeni sugu????waanzae na mawaziri, usalama wa taifa, na wote waliosomeshwa nje ya nchi,,hii operation iwaexclude wasio na ajira au wapewe ajira then ndo muwadai....
 
Back
Top Bottom