Watumishi wengi wa Umma tumeachwa Kimaisha na Wajasiriamali wadogo

Yaani mtumishi aniboost mimi wakati wao ndio wananikopa vitu wakisubiri mshahara ndio walipe! naamua kuwasaidia kwakuwa pesa yangu inakaa kwao mda mrefu bila mzunguko.

Mishahara yenyewe ya nchi hii ya take home laki 8 au 7 ndio mtegemewe na jamii ok may be wewe!lakini mimi kwetu watu wamesoma wengi lakini kwenye mambo ya kifamilia yakitokea wanategemewa nduguzetu wafanyabiashara.

Mimi nilisoma nilipomaliza nikapata ajira nikafanya miaka 8 nikapata kianzio nikaacha kazi nafanya biashara! mimi sina DND ya kuajiriwa akili yangu iligoma kabisa ajira zenyewe za nchi masikini kutoboa ukiwa kazini labda uibe lakini sio mshahara.
 
DND =DNA
 
Sio wote waliojariwa wanapenda wengine ni family background ndio inafanya hvyo kama ww kwenu mmesoma wote ni jambo la kher watu wamevaa namba 9 mgongoni tangia primary school ila hawana back up biashara kuna rise and fall ila ajira ni uniform usidharau walioajiriwa maana kuna wengine wengine wanaona ni bora laki 5 ya uhakika kuliko million 1 ya kukimbizana na biashara kwasababu we differ in many ways according to responsibility and family background so respect others life is like a box of chocolate.
 
Huyo Kimaro unamwamini mtu wa Kuongeza chumvi sana! Motivational speaker!
 
Watu wanapenda sana kubisha, wanaona mambo hayawezekanai ila wapo watu wanaingiza pesa ndefu sana kwa biashara ambazo ni za kawaida. Nina mfano wa dada mmoja anauza juisi fresh.

Kwa siku analaza za kawaida analaza wastani 350k, kuanzia ijumaa na weekends analaza wastani wa 600k.

Ubishi bila kuwa na ushahidi ni UJINGA na MZIGO.
 
Yaani wewe Mbumbumbu kweli yaani ukiwa bizzy na mavitabu kuangalia uhalisia kweli huwezi ona ukweli Kundi kubwa la Watumishi wa umma ndiyo wajasiliamali wenyewe. Wao ndiyo wakulima,wao ndiyo wamiliki wa vyombo vya usafiri wao ndiyo wafanyabiashara tatizo kubwa ya hao wafanyakazi huwa wanaficha uhalisia ili kukwepa taarifa za kuharibiwa kazi.Madaktari wengi wanamiliki hospital na pharmacy,Walimu wengi ndiyo Wamiliki wa Bookshop na stationary ,Maofisa wengi wa majeshi ndiyo wamiliki wa makampuni za Ulinzi na vyombo vya Usafiri,Maofisa wengi ndiyo wafanyabiashara wa Kariakoo,Waandisi wengi ni wamiliki wa nyumba za kupangisha town maofisa Ardhi wengi ndiyo wafanyabiashara wa Kuuza viwanja ,Kilimo ndiyo karibu wafanyakazi wengi ni wakulima hata ukienda mashambani utasikia tu hili shamba kubwa ni la Teacher,Mjeshi,Doctor,Bwana mifugo au vyovyote mradi tu wafanyakazi. Kwenye Makazi ukifika kila mitaa utakuta nyumba kali za hayo maeneo ni wafanyakazi wa umma tupo mitaani huku tunaona kuanzia Masaki,Oysterbay,Mbweni Bunju kijichi utasikia tu hii ya mejor General fulani ,hii ya kamishina fulani,hii ya Professor fulani,hii ya Waziri fulani ,hii ya Mbunge fulani na majina ya hiyo mitaa wanapewa hao viongozi wanaoishi huko.Tuache kujidanganya ili uwe mfanyabiashara Mzuri kwa jamii zilizotokea kaya maskini wengi wanapatia pesa kwenye Utumishi wa Umma na kisha wanafanya Uwekezaji. Kule Gongola mboto Mashamba mengi ya kuku wa Mayai na nyama yanamilikiwa na Askari na Walimu, Bajaji na Bodaboda kwa DSM nyingi kupita maelezo zinamilikiwa na hao wafanyakazi .
Hivyo acha kujifariji ikitokea fursa za ajira tuzidandie fasta tupate mitaji ya kueleweka.
 
Kwaiyo kwa mwaka anapata faida ya million 60 afu bado anauza nyama na ugali ebu acha mashala
Lizika na ajira yako usiumizwe na maneno ya watu
 
Achana nao hao watu!ajira zenyewe za nchi masikini hizi mishahara kiduchu kutoboa hadi uibe.Ukikutana na Kiongozi kama Chuma Magufuli anaziba mianya mnabaki kulialia kwa sababu mshahara hautoshi.

Mimi niliajiriwa miaka 8 nikapiga chini nafanya mishe zangu! maisha pote yanachangamoto lakini wasidhani kuwa wao ndio wanapiga pesa kuliko wasio watumishi kuna watu mtaani wanachukua pesa nzuri kwa siku kwenye kazi zao.

Mfano mimi nilifungua kibanda cha TIGO PESA nikamuweka binti yupo pale hadi leo! kupitia miamala ya Lipa kwa simu kwa siku naingiza sio chini ya 30,000/= bado malipo ya mwisho wa mwezi kutoka makampuni ya sim.

Binti namlipa 150,000/= kwa mwezi halafu nalipa 15,000 ya sehem nilipoweka banda! na mimi ninashughuli zangu zingine.Kuna watu wengi tu nawajua waingiza zaidi ya laki 1 faida kwa siku haya mambo sio hadithi yapo nduguzangu msiwaone watu mtaani hawajavaa tai na suti makadhani wate wamechoka.
 
Kwani wewe kuchoma chipsi unashindwa, kuchoma nyama na kuuza ugali unashindwa ???.....🤔🤔🤔

Kuna tatizo pahala juu yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…