Watumishi wa umma, sasa RUSHWA ruksa, toa huduma baada ya kupewa rushwa

ntamaholo

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
12,906
6,909
Samahani sana wana jamvi.

Nimeamua kuanzisha kampeni ya kuchukua RUSHWA kwa watoa huduma wote kuanzia wale wa umma na wale wa sekta binafsi. Sababu za kuhamasisha kudai rushwa ni:-

(i) Kupambana na gharama za maisha zinazopaa kila siku. Mchele leo 1700/- sukari 2500/- khanga ya urafiki 8000/- mafuta ya taa 2300/- na mengine kibao. Kupokea rushwa, kutasaidia kupambana na hali ya maisha iliyopo.
(ii) Kuendana na fikra za wawakilishi wetu, walijipandishia posho kwa asilimianahamsininanne=154%
(iii) Kudai rushwa kwa kiwango sawa na ongezeko la posho ya wabunge, kutawafanya wananchi mbumbumbu waichukie moja kwa moja serikali na hivyo kujitosa moja kwa moja katika kuikomboa nchi yao.

WALIMU, ASKARI WA MAJESHI YOTE, MADAKTARI, WATUMISHI WA HALIMASHAURI, MANSPAA NA MAJIJI, WATUMISHI WA MAMLAKA ZOTE NCHI, CHUKUA RUSHWA ILI KUSAIDIA KUIKOMBOA TANGANYIKA YETU.

Ni mawazo yangu tu jamani
 
haswa trafiki rushwa toka sh 5000 mpaka sh 10000

hii kidogo, haendani na mfumuko wa bei za vitu AU KWA KUWA HAKUSANYI KWA MMOJA? BASI NAUNGA MKONO HOJA, KWANI AKIKUSANYA KWA WATU 20, TAYARI NGOMA DROO NA MBUNGE WAKE
 
ni mawazo mazuri kabisa. kwasababu mara nyingi anayemwaga msosi jalalani hawezi kujua kama kuna wengine hawali hata mara moja kwa kutwa. nilikuwa sina mpango wa kufanya kazi serikalini kwa kuhofia kupokea rushwa "automatically", sasa nitajitahidi ili niingie na mimi nikawe mla rushwa mkubwa
 
Support- kula rushwa kwa kwenda mbele. Kila mtu ale kwa nafasi yake. Rushwa ruksa sasa. Maana na wabunge kujiongezea posho ni rushwa iliyohalalishwa. Sisis wengine hakuna wa kutuhalalishia, hivyo tujihalalishie!!
 
tena napendekeza rushwa iwe kubwa lakini huduma za kijamii ziwe mbovu. hali hii itawafanya wapigakura wajiulize wamejikwaa wapi na hatimaye wataovacome
 
Support- kula rushwa kwa kwenda mbele. Kila mtu ale kwa nafasi yake. Rushwa ruksa sasa. Maana na wabunge kujiongezea posho ni rushwa iliyohalalishwa. Sisis wengine hakuna wa kutuhalalishia, hivyo tujihalalishie!!

ule msemo wa kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake, iwe ajenda ya kila siku, tunyonyane, halafu atakaye athirika zaidi na unyonyaji atachukua hatua tu, kwani ni wengi watakaoumia kwa kujilipa posho siye wenyewe katika ofisi zetu
 
mimi barabarani sitembei bila msimbazi,trafiki tukikutana wala msisumbue muda wenu kupatana na mimi mkinikuta tu semeni lete hela.
 
hayo sio mawazo yako pekee bali ndo mawazo ya watanzania wengi sababu life ipo juu sana

basi mkuu mood, tuhame kutoka kwenye mwazo, na tusipende kusikia oooh walimu wameuza mitihani, oohho polisi wanaongoza kwa rushwa, ohoo hospitalini bila chochote hupati huduma, oooh mahakani rushwa imezidi, tusiongoee habari hizi kabisa, ili mbinyo wa maisha kwa watatnznia utufanye tubadilike kifkra, tushiriki sawasawa katika mambo yanayotuhusu tena kwa nguvu ya ajabu yaani umma uamue
 
mimi nakula ruswa hata mia tano tu! Kazini naingia saa nne za asubuhi,kuondoka saa saba mchana japo sina kiosk bora nikaanzishe kibustani cha mboga na kufuga sungura na kuku wa kienyeji!
 
mimi nakula ruswa hata mia tano tu! Kazini naingia saa nne za asubuhi,kuondoka saa saba mchana japo sina kiosk bora nikaanzishe kibustani cha mboga na kufuga sungura na kuku wa kienyeji!

bora kila mtu awe fisadi halafu tuone nani atamfunga mwenzie kengele, kila mtu mwizi
 
hilo nalo nineno
wengine hata namna ya kuomba hilyo rushwa inakuwa ngumu.
 
...rushwa dhambi.

POSHO JE ZISIZO LAZIMA SIYO DHMABI? ETI MBUNGE anabaki na laki saba? kutoka mil. 12? huu si uwongo wa kutaka kuhalalisha posho. fuatilia maneno ya makinda utaona dhambi aliyoifanya, ya kudanganya watatnzania
 
hilo nalo nineno
wengine hata namna ya kuomba hilyo rushwa inakuwa ngumu.

utakuwa unaleta visingizio tu, mara hiki hakipo, mara kile hakuna, mpiga kura atajiongeza na kukupa ya chai, pokea halafu mpe huduma asepe
 
wanatoa rushwa ni wale wenye uwezo
je maskini asie kuwa na senti anapoumwa akatibiwe wapi
rushwa ikishakolea kuitoa ni ngumu sana wengi wataumia
bora tuingie mtaani tukiwa wazima kumtoa gamba kichwa kuliko kuruhusu rushwa
 
Back
Top Bottom