Watumishi wa umma sasa kwisha

Watumishi wa umma sasa kwisha

Madiwani wetu siyo siri elimu "0"haipendezi kuwacontrol ma DEO,DMO,DPO nk...ni wazushi tu acha iwe hivyo.

Kweli kabisa wengi wao wapo tu Kama rubber stamp!
Kazi Yao kupitisha tu kila kitu muda wa kusoma Kwa umakini hawana, uwezo wa kujenga na kuchambua hoja hawana!
Kazi Yao kufukuzia posho na majungu na kufukuzia flani apate tenda ili akumbukwe !
 
Japo umeandika hovyo lakini nahisi wewe ni muathirika namba moja wa uamuzi wa Mh Rais.!

Hebu fikiri kidogo Kama wewe ni mkazi wa Dar tembelea kimara.! Angalia ujenzi unaofanyika kisha jiulize je wilaya hiyo ina afisa mipango ardhi?
Upimaji wa viwanja na ramani idara hiyo ipo? Kama ipo, ipo tangu lini?
Je wanalipwa mishahara kama ndio je kwa kazi ipi. Ama iliyofanywa ama inayofanywa, sasa.!

Au tembelea Jiji la mbeya hasa maeneo ya uyole juu na uyole kati angalia Zile nyumba zinazojengwa kisha jiuliza afisa Ardhi yupo.?
Je jiji la Mbeya lina idara ya upimaji na ramani.? Kama ipo hiyo idara je ina muda gani? Na je ina watu wanaolipwa na serikali? Kama ndio je kwa kazi ipi wanayofanya?!!

Kisha baada ya hapo usisahau uuzwaji wa viwanja vilivyopimwa ulivyo na mizengwe na rushwa vibali vya ujenzi na nk.

Au amua kutembelea Nchi jirani tu kisha angalia miji ya wenzetu na huo wa kwetu.

Ukisha jijibu maswali hayo utampongeza mh Rais kwa uamuzi huo..
Mkuuu wewe ulienda shule? Au unajitoa ufahamu coz Ya vijisenti? Unajua maaana Ya madaraka Ya serikali za mitaaa? Mimi nilikuwa Mwalimu niliacha miaka mingi nashughulika na biashara zangu hivyo ninaongea Kwa mujibu wa sheria na sera unapotaka kurudisha madaraka serikali kuuu wizarani ni kurudi nyuma hatua mia hivi kwenye Maendeleo unapaswa kurudi nyuma?
 
Kama changamoto ilivyo Kwa wabunge hivyo hivyo Hata madiwani wanapaswa kuwa wasomi Walau kuanzia kiwango cha shahada moja!
 
wakuuu huyu baba anataka kila kitu kiwe chini yake na falsafa yake ni fukuza fukuza hili ni janga kubwa Sana tena Sana watumishi sasa wanaenda kufukuzwa Kama njugu
Ukifanya kazi yako kwa nidhamu, uaminifu na uadilifu uliotukuka nani atakufukuza kazi?? Kama wewe ni mwizi, mvivu na mzembe ukiwa kazini lazima utaogopa fukuza fukuza ya Magufuli. Siku zote mwizi huogopa mpaka kivuli chake mwenyewe.
 
Wakuuu natazama taarifa Ya habari hapa naona Aucle magufuli amebadilisha utaratibu wa wakuu wa planing Ardhi majengo na maji wa Halmashaur ya wilaya kuwa sasa watawajibika Kwa wizara moja Kwa moja hiii ni hatari Sana kumbukeni kuwa alipoingia madarakani alibadilisha ule utaratibu wa kuwapata madasi yani makatibu tawala wa wilaya na wakurugenzi akawa anawateua yeye, kinachooonekana ni kuwa anataka watumishi wooote wawe chini yake, ndio maaana anabadilisha utaratibu wa kisheria yani anaposema mtu afukuzwe moja Kwa moja hiii si sawa ni ukandamizaji wa Hari Ya juuu maaaana mtu hataweza kujitetea popote, wakuuu huyu baba anataka kila kitu kiwe chini yake na falsafa yake ni fukuza fukuza hili ni janga kubwa Sana tena Sana watumishi sasa wanaenda kufukuzwa Kama njugu Lakini pia madiwani wamenyang'anywa madaraka sasa maaana wakurugenzi hapo awali walikuwa wanawajibishwa na madiwani sasahivi Diwani hawezi kuthubutu ataaambiwa weeee Mimi nimeletwa hapa na rais na Mwisho had walimu watakuwa chini yake wakuu hili ni janga
Mbona unaeleza na kufafanua hata zaidi ya yale aliyosema Rais? Ameagiza Mawaziri wa Tamisemi, Ardhi na Katibu mkuu kiongozi wakutane ili kuweka utaratibu rasmi wa utekelezaji wa agizo lake, lakini lengo kuu ni kuwadhibiti kinidhamu wataalamu hao wanapokiuka utaratibu bila kusubiri vikao vya madiwani na wala hajawanyang'anya madiwani mandate ya kuwasimamia kiutendaji wataalamu hao.Zingatia kuwa Wizara ndio mamlaka ya uteuzi na sio full council za madiwani ktk halmashauri husika. Hayo mengine ni according to your own opinion.
 
Ukifanya kazi yako kwa nidhamu, uaminifu na uadilifu uliotukuka nani atakufukuza kazi?? Kama wewe ni mwizi, mvivu na mzembe ukiwa kazini lazima utaogopa fukuza fukuza ya Magufuli. Siku zote mwizi huogopa mpaka kivuli chake mwenyewe.
Mkuuu madaraka yanaenda Kwa wananchi unapoyarudisha Kwa mtu mmoja unarudi nyuma ngoja nikupe mfano hapo nyuma wakurugezi walikuwa wanaomba nafasi wanashindanishwa tena wanafanya mtihani anaefaulu ndio aliekuwa anateuliwa kuwa Mkurugenzi wa halamshauri Ya wilaya Fulani ndio maaana wakurugenzi wengi hapo mwanzo walikuwa ni maaafisa Utumishi au maaafisa mipango Lakini Kwa sasa wanateuliwa inamaaana wanaweza kuteuliwa Toka kabila moja tu au Kwa kigezo cha uchama au undugu au Rafiki matokeo yake ni kuondoa ufanisi na kuondoa haki na kuondoa ushindani na kuondoa usawa ndio maaana kuna kitu kinaitwa ushindani hivyo tunataka kurudi nyuma Sana
 
Najiuliza Kwa nini anatanguliza saaana hoja Ya kufukuza?
Kuondoa utendaji wa mazoea..mi pia nafanya kazi kampuni binafsi kinachonifanya niheshimu sheria na kanuni ni sababu naogopa kufukuzwa..maana jamaa slogan yao ni zero tolerance.
 
Mkuuu Kama kweli una uelewa vizuri hueezi kubaliana na jambo hili hata kidogo mabadiliko haya yakujiribikishia madaraka tulishahama huko tukapeleka madaraka mikoani na wilayani hatua iliyokuwa inafuata ni kupeleka madaraka kwenye Kata sasa tunarudi tuliko toka labda wewe ujitoe ufaham
Sawa lakini kumbuka Rais ni head of State.
 
Tushamuuzia msukuma nchi tunataka nini tena???deal done wazee...
 
Sababu mabilioni ya miradi na hasa ya maji yameliwa karibu nchi nzima na kwa sehemu kubwa wahusika ni wao." Ukicheka na nyani utavuna mabua ".

Inasikitisha sana kuona Kwa zaidi ya miaka 57 ya uhuru wa Tanganyika huduma ya Maji imeshindikana kupatikana [emoji848][emoji848][emoji87][emoji87]
Kila mwaka bajeti ya Maji inasomwa lakini tatizo la Maji linazidi kuwa kubwa sana!
Hata Dar imeshindikana kuwa mfano Kwamba ukiwa huku tatizo la Maji ni historia !
Sasa Hivi mshaurini asinunue ndege kwanza hadi wananchi tupate huduma ya Maji jamani!
 
Maji hakuna kila mahali , majumbani hakuna, Hospitali hakuna, mashuleni hakuna, wanafunzi wakijisaidia haja kubwa inabidi watumie majani au makaratasi ambayo yanaumiza na kuchana nyeti !
 
Mkuuu wewe ulienda shule? Au unajitoa ufahamu coz Ya vijisenti? Unajua maaana Ya madaraka Ya serikali za mitaaa? Mimi nilikuwa Mwalimu niliacha miaka mingi nashughulika na biashara zangu hivyo ninaongea Kwa mujibu wa sheria na sera unapotaka kurudisha madaraka serikali kuuu wizarani ni kurudi nyuma hatua mia hivi kwenye Maendeleo unapaswa kurudi nyuma?
Waweza kuwa mwalimu.lakini huoni uchafu na uozo unaofanyika kwa kupeleka madaraka huko yalikokuwa yamepelekwa.!
Nimeuliza maswali yale ambayo kwangu nimeyaona ni msingi pale Juu soma kisha uyajibu.

Tusiangalie madaraka tu na kulalamika nadhani ingelikuwa busara pia tufanye tathmini kwa kipindi chote ambacho madaraka yalikuwa huku yaliko ondolewa je kulikuwa na tija?

Kama hakuna tija je hatupaswi kuchukua hatua zitakazo tengeneza uwajibikaji?

Au ndio siasa kwenye kila hatua as usually
The president is not right but opposition ndio wako right.
 
Wakuu huyu baba anataka kila kitu kiwe chini yake na falsafa yake ni fukuza fukuza hili ni janga kubwa Sana tena Sana watumishi sasa wanaenda kufukuzwa Kama njugu.
Atakufukuzaje kama ujavunja sheria na utaratibu wa kazi? Wewe kama ulikuwa unanufaika na mfumo huo pole. Kwanza, wafanyakazi hawa walikuwa wananyanyaswa na vikao vya madiwani sana ! Mimi naunga mkono uamzi huu wa serikali.
 
Mkuu mbona kama umeangalia kitu kimoja tu?
1. Ina maana ukiritimba huuoni kama sasa utapotea sababu ya yale mambo ya usumbufu na urasimu katika maofisi ya serikali?
Hata yeye mwenyew ni mkiritimba..mbona kaleta ukiritimba kuwapa watumishi wa umma annual increment zao...kaleta ukiritimba kupandisha madaraja na vyeo vya watumishi wa umma...lile povu analowatolea watumishi wa umma kuchelewa kufanya majukumu yao kwa wakati ilitakiwa ajitolee yeye kwanza kwa kutowapa haki zao kwa wakati...nyani haoni kundulee
 
Kwa hili tuko pamoja @ Anko Magu, twende kazi [emoji124][emoji124][emoji125]
 
Mbona unaeleza na kufafanua hata zaidi ya yale aliyosema Rais? Ameagiza Mawaziri wa Tamisemi, Ardhi na Katibu mkuu kiongozi wakutane ili kuweka utaratibu rasmi wa utekelezaji wa agizo lake, lakini lengo kuu ni kuwadhibiti kinidhamu wataalamu hao wanapokiuka utaratibu bila kusubiri vikao vya madiwani na wala hajawanyang'anya madiwani mandate ya kuwasimamia kiutendaji wataalamu hao.Zingatia kuwa Wizara ndio mamlaka ya uteuzi na sio full council za madiwani ktk halmashauri husika. Hayo mengine ni according to your own opinion.
sasa na nani alikuambia unawadhibiti watu kinidhamu kwa kugatua madaraka na kuyapeleka serikali kuu,halafu kwa akili yako unategemea huyo waziri wa TAMISEMI,Ktibu mkuu wataenda tofauti na anavyo hitaji magufuli?. pia hao madiwani watawezaje kusimamia watu ambao wata report moja kwa moja kwa WAZIRI?
anacho kifanya magufuli anarudisha mambo nyuma mara 100 na yalivyo kuwa
 
Atakufukuzaje kama ujavunja sheria na utaratibu wa kazi? Wewe kama ulikuwa unanufaika na mfumo huo pole. Kwanza, wafanyakazi hawa walikuwa wananyanyaswa na vikao vya madiwani sana ! Mimi naunga mkono uamzi huu wa serikali.
una unga mkono sababu hujui ni kwa nini serikali za mitaa zilianzishwa,kila idaa inayounda halmashaui ni muhimu ktk maisha ya watu huwezi sema unaitoa huko eti kwa kuwa inasumbuliwa na madiwani.
 
Back
Top Bottom