Watumishi wa umma sasa kwisha

Watumishi wa umma sasa kwisha

Ile kitu inaitwa UGATUAJI WA MADARAKA naona haipo siku hizi.
 
Japo umeandika hovyo lakini nahisi wewe ni muathirika namba moja wa uamuzi wa Mh Rais.!

Hebu fikiri kidogo Kama wewe ni mkazi wa Dar tembelea kimara.! Angalia ujenzi unaofanyika kisha jiulize je wilaya hiyo ina afisa mipango ardhi?
Upimaji wa viwanja na ramani idara hiyo ipo? Kama ipo, ipo tangu lini?
Je wanalipwa mishahara kama ndio je kwa kazi ipi. Ama iliyofanywa ama inayofanywa, sasa.!

Au tembelea Jiji la mbeya hasa maeneo ya uyole juu na uyole kati angalia Zile nyumba zinazojengwa kisha jiuliza afisa Ardhi yupo.?
Je jiji la Mbeya lina idara ya upimaji na ramani.? Kama ipo hiyo idara je ina muda gani? Na je ina watu wanaolipwa na serikali? Kama ndio je kwa kazi ipi wanayofanya?!!

Kisha baada ya hapo usisahau uuzwaji wa viwanja vilivyopimwa ulivyo na mizengwe na rushwa vibali vya ujenzi na nk.

Au amua kutembelea Nchi jirani tu kisha angalia miji ya wenzetu na huo wa kwetu.

Ukisha jijibu maswali hayo utampongeza mh Rais kwa uamuzi huo..
Excellent , binafsi namuunga mkono mkuly
 
negative thinkers!...declare interest...au nawe ndo mmoja wa hao wapimaji wahuni wanaoleta usumbufu huku wilayani? Kama ndivyo subiri panga la Lukuvi utalisikia mu shingo muda mfupi ujao...la sivyo jirekebishe! Hizi ni zama zingine tumechoshwa na ukuritimba na ubwanyenye!
 
No ukiritimba ndio utazidi Kama mkuu wa idara ataratibiwa na wizara badala Ya madiwani mkuu ni hatari kumbuka kuwa halamashauri ziko zaidi Ya 180 zote ziratibiwe na mtu mmoja si jumbo rahis Kama unavyofikiria tofauti na madiwani walioko hapo hapo Siku zoote saaa yooote pia kumbuka kuna watakaoletwa na huyo katibu mkuu Kama Jamaa zake
Nadhani haukumsikiliza vizuri mheshimiwa Rais.
'Pwenti' yake ilikuwa ni kukazia uwajibikaji, hasa mainjinia wa maji waliokuwa chini ya halmashauri, kwamba walikuwa hawadhibitiwi na madiwani, ndiyomaana miradi mingi ya maji, pamoja na fedha za utekelezaji kutolewa ilikuwa haitekelezwi.
Kwa kipindi cha miaka 10 ni karibia %70 ya miradi ilidorola pamoja na kuwa pesa ilitolewa.
Hizo mbinu na maagizo aliyotoa ya kiuwajibikaji, kwangu naona ni madini yanayostahili kuzungushiwa ukuta.
Kamwe hatuwezi kutetea uozo 'kabila' hiyo.
WaTz tulizoea sana kula bila kufuta midomo! Linapokuja suala la kukumbushwa mtu uliyestaarabika unavyotakiwa ule, hapohapo yanaanza makelele na majungu kama hivi!
 
Inasikitisha sana kuona Kwa zaidi ya miaka 57 ya uhuru wa Tanganyika huduma ya Maji imeshindikana kupatikana [emoji848][emoji848][emoji87][emoji87]
Kila mwaka bajeti ya Maji inasomwa lakini tatizo la Maji linazidi kuwa kubwa sana!
Hata Dar imeshindikana kuwa mfano Kwamba ukiwa huku tatizo la Maji ni historia !
Sasa Hivi mshaurini asinunue ndege kwanza hadi wananchi tupate huduma ya Maji jamani!
Mkuu, umeielewa mada lakini ama umesikiliza alichokisema rais juu ya hasara taifa limeingia kwa kipindi kirefu kutokana na utendaji usiowajibika wa wahandisi wa maji wa halmashauri?
 
Mtoa mada pole sana umetumia nguvu kubwa na hisia kuandika either kwa kujua au kutokujua ntaelezea mambo Mawili
1.Rais ni mtumishi na mwajiri mkuu na kama kiongozi wa serikali anapoona kunaudhaifu sehemu lzma achukue hatua.Halmashauri nyingi zimeoza rushwa na urasimu iyo inasababisha miradi mingi kukwama na pesa kupotea pia madiwani wameshindwa kuwawajibisha watendaji ndo maana rais akaamua hvyo

2.Sio kweli Rais anayo falsafa ya kufukuza watu ulivyosisitiza. Hpn wala aonei sbbu ata waliosimamishwa kazi walipewa sbbu na ambao hawakuridhika walikwenda Mahakamani kutafuta haki

Kwakumalizia Rais habadilishi sheria kuzuia wengine kufanya kazi mfno madiwani au RAC wale wanasheria zao. Anafanya mageuzi machache kwa maslahi mapana ya nchi
 
Na wakuu wa mikoa vipi mkuu?

[emoji14][emoji14][emoji14] hao sijui hatima Yao itakuwaje!
Unajua ukiangalia sana muundo wa Serikali kuu na Tamisemi utagundua kuna multi allocation of human resources !
Hali hii imepelekea Serikali kuingia gharama kubwa ktk kuwalipa watumishi wa umma ambao mpangilio wao wa kazi haueleweki!
Hivi Kwa mfano Afisa Ardhi aliyeko halmashauri ya Wilaya pale mfano Kinondoni kazi Yake ni nini?, Afisa Ardhi aliyepo pale Halmashauri ya Jiji la Dsm ni nini?, Je Afisa Ardhi aliyepo wizara ya Ardhi naye kazi Yake ni nini?
N.k Yani ni mlolongo wa urasimu wa kikoloni!
Haya ukija tena ktk kila mkoa kuna Mkuu wa mkoa, kuna wakuu wa Wilaya , kuna mkurugenzi wa kila halmashauri , kuna meya/wenyeviti, ma RAS, ma DAS hawa wote wanapaswa kuondolewa abaki mmoja Kama tuko siriasi!
 
sio lazima ufanye madudu wewe. kumkuu wa idara ya fedha mafia amefukuzwa kazi kwa kumlatalia mkurugenzi ndugu erick mapunda aliyeteuliwa na MAGUFULI kufuata taratibu za pesa. umekaa hapo ulipo unabwabwaja tu kama kasuku
Nini Hiki??
 
Mkuuu wewe ulienda shule? Au unajitoa ufahamu coz Ya vijisenti? Unajua maaana Ya madaraka Ya serikali za mitaaa? Mimi nilikuwa Mwalimu niliacha miaka mingi nashughulika na biashara zangu hivyo ninaongea Kwa mujibu wa sheria na sera unapotaka kurudisha madaraka serikali kuuu wizarani ni kurudi nyuma hatua mia hivi kwenye Maendeleo unapaswa kurudi nyuma?
Sawa, lakini mbona kuna mizengwe huko? Ngoja wanyooshwe then badae watarudishiwa baada ya kunyooshwa?
 
Hata yeye mwenyew ni mkiritimba..mbona kaleta ukiritimba kuwapa watumishi wa umma annual increment zao...kaleta ukiritimba kupandisha madaraja na vyeo vya watumishi wa umma...lile povu analowatolea watumishi wa umma kuchelewa kufanya majukumu yao kwa wakati ilitakiwa ajitolee yeye kwanza kwa kutowapa haki zao kwa wakati...nyani haoni kundulee
Ndo head of the state ;so kelele za chura hazimzuii ndama kunywa maji
 
sasa na nani alikuambia unawadhibiti watu kinidhamu kwa kugatua madaraka na kuyapeleka serikali kuu,halafu kwa akili yako unategemea huyo waziri wa TAMISEMI,Ktibu mkuu wataenda tofauti na anavyo hitaji magufuli?. pia hao madiwani watawezaje kusimamia watu ambao wata report moja kwa moja kwa WAZIRI?
anacho kifanya magufuli anarudisha mambo nyuma mara 100 na yalivyo kuwa
Acha mnyooshwe
 
una unga mkono sababu hujui ni kwa nini serikali za mitaa zilianzishwa,kila idaa inayounda halmashaui ni muhimu ktk maisha ya watu huwezi sema unaitoa huko eti kwa kuwa inasumbuliwa na madiwani.
Kazi za miradi zitaonekana kwa uamuz huu! Sio kula mishahara tu na posho
 
Huu Uzi nimesoma nikaishia katikati, inawezekana kabisa Ujumbe ukawa mzuri ila tatizo uandishi. Daaaaah mkuu mkato na nukta zilikupitia kushoto? Hata ladha ya kuendelea kusoma inakata mkuu, rekebisha huu uzi bwana unyooshe maelezo
Mkuu sema kiswahili kimekupiga chenga,mimi mswahili nimesoma na kufahamu alichoandika,makosa yapo katika kuchanganya baina ya "L" na "R",mfano "Hali" ameandika "Hari",haya makosa sisi waswahili kwa sasa tumeanza kuyazoea,tukiona hivyo moja kwa moja tunajua muandishi katokea wapi😀
 
No ukiritimba ndio utazidi Kama mkuu wa idara ataratibiwa na wizara badala Ya madiwani mkuu ni hatari kumbuka kuwa halamashauri ziko zaidi Ya 180 zote ziratibiwe na mtu mmoja si jumbo rahis Kama unavyofikiria


Hao wadudu ni pasua kichwa, sehemu nyingi hawana elimu, wanachofuata ni kugawana viwanja na fedha toka kwenye miradi inayotekelezwa chini yao
 
Raisi wa awamu ya 6 atapata tabu sana kurudisha mfumo sahihi wa uendeshaji serikali.
 
Back
Top Bottom