Watumishi wa Umma njooni tukubaliane

Watumishi wa Umma njooni tukubaliane

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
59,220
Reaction score
138,651
Watumishi wenzangu wa umma bila kujali cheo wala ngazi ya mshahara,bila kujali ni permanent and pensionable ama ni mkataba,nawaalika hapa ili tujadili na kukubaliana kuhusu hatma yetu Octoba 25.

Katika mjadala wetu tujadili juu ya mazingira ya kazi kwa ujumla ikiwa pamoja na stahiki zetu.Kwa kuanzia tu niseme mimi kama afisa mwandamizi wa serikali naona watumishi tuna changamoto nyingi sana ambazo zimekosa majibu na utatuzi.Mojawapo ikiwa ni gap kati ya maslahi yetu na wanasiasa.

Wanasiasa wanakula nchi mpaka mbegu.Mfano ni ukata uliokumba ofisi zetu mwaka huu,lakini unaweza kusikia mamilioni na mabiliöi kuhonga wanasiasa.Mnasemaje kuhusu PAYE kwenye mishahara ukilinganisha na misamaha ya kodi kwa makambuni makubwa ya kibiashara. Watumishi wenzangu mnasemaje kuhusu wanasiasa kuwa ndio kila kitu nchi kiasi cha taaluma zetu kuwa dumped.

Mfano mzuri ni jinsi bajeti ilivyovurugwa mwaka wa fedha uliopita na unaoendelea.Watumishi bunge la katiba halikuwa kwenye bajeti na pesa zimetafunwa.Mambo ya maabara yamekwapua Grants zote na Mapato ya Ndani.

Unajua hujalipwa stahili zako ngapi kutokana na lack of budget displine?Sasa ndugu watumishi tunafanyaje Oct 25?Ni kweli CCM bado inatosha?

Tujadili hapa.
 
tatizo Magufuli Sera zake ni kiwajibisha ss, wanapaswa atuahidi, wakorofi aseme ndio atawaadhibu sio sisi sisimizi
 
Mwaka huu lazima mabadiliko yafanyike kwa kweli.. mie nimechoka hiyo PAYE kwa kweli...
Bila kuiondoa CCM PAYE itabikia gumzo kubwa kwa watumishi wa UMMA.. Kwangu kwa kweli CCM bado haitoshi!!
 
Dawa ya Haya yote ni kupigia kura magufuri
Watumishi wenzetu wa Kigamboni wanaweza kusema kitu,wanaijua habari ya kupiga mbizi.Halafu hapa tunazungumza kitaalam.Report ya CAG inasema ukweli.Halafu mimi mtumishi nikipangiwa Tanga nakuta nyumba ya umma imeuzwa,kodi room laki moja
 
watumishi wenzangu wa umma bila kujali cheo wala ngazi ya mshahara,bila kujali ni permanent and pensionable ama ni mkataba,nawaalika hapa ili tujadili na kukubaliana kuhusu hatma yetu octoba 25.katika mjadala wetu tujadili juu ya mazingira ya kazi kwa ujumla ikiwa pamoja na stahiki zetu.kwa kuanzia tu niseme mimi kama afisa mwandamizi wa serikali naona watumishi tuna changamoto nyingi sana ambazo zimekosa majibu na utatuzi.mojawapo ikiwa ni gap kati ya maslahi yetu na wanasiasa.wanasiasa wanakula nchi mpaka mbegu.mfano ni ukata uliokumba ofisi zetu mwaka huu,lakini unaweza kusikia mamilioni na mabiliöi kuhonga wanasiasa.mnasemaje kuhusu kodi zetu kwenye mishahara ukilinganisha na misamaha ya kodi kwa makambuni makubwa ya kibiashara. Watumishi wenzangu mnasemaje kuhusu wanasiasa kuwa ndio kila kitu nchi kiasi cha taaluma zetu kuwa dumped.mfano mzuri ni jinsi bajeti ilivyovurugwa mwaka wa fedha uliopita na unaoendelea.watumishi bunge la katiba halikuwa kwenye bajeti na pesa zimetafunwa.mambo ya maabara yamekwapua grants zote na mapato ya ndani.unajua hujalipwa stahili zako ngapi kutokana na lack of budget displine?sasa ndugu watumishi tunafanyaje oct 25?ni kweli ccm bado inatosha?tujadili hapa

kama umeshindwa kazi basi ondoka.hatuwezi kuacha kuwapa pesa watu kama dr silaa na professpr lipumba kutufanyia kazi ya kumudhibiti lowasa halafu tukufikilie wewe.ccm hatuko tayari kuachia dola kiraisi hivyo.unajua kabisa watu kama dr silaa na lipumba si watu wakuwapa billion moja au mbili lazima tutumie pesa nyingi ili kuhakikisha lowasa tunamdhibiti.hatutaki mtu wa kaskazini kushika uraisi
 
Ukawa Mwaka Huu Ikulu Ccm Tupa Mbali Imeshindwa Kila Kitu
 
kama umeshindwa kazi basi ondoka.hatuwezi kuacha kuwapa pesa watu kama dr silaa na professpr lipumba kutufanyia kazi ya kumudhibiti lowasa halafu tukufikilie wewe.ccm hatuko tayari kuachia dola kiraisi hivyo.unajua kabisa watu kama dr silaa na lipumba si watu wakuwapa billion moja au mbili lazima tutumie pesa nyingi ili kuhakikisha lowasa tunamdhibiti.hatutaki mtu wa kaskazini kushika uraisi

point nzur sana,
 
kama umeshindwa kazi basi ondoka.hatuwezi kuacha kuwapa pesa watu kama dr silaa na professpr lipumba kutufanyia kazi ya kumudhibiti lowasa halafu tukufikilie wewe.ccm hatuko tayari kuachia dola kiraisi hivyo.unajua kabisa watu kama dr silaa na lipumba si watu wakuwapa billion moja au mbili lazima tutumie pesa nyingi ili kuhakikisha lowasa tunamdhibiti.hatutaki mtu wa kaskazini kushika uraisi
hatuna tatizo basi tuambieni zinatoka kifungu gani cha bajeti na afisa gani kapewa masufuru hayo ili tufuatilie retirement zake
 
CCM kwa heri siwapi kura yangu.namchagua LOWASA basi.nyie sio mafisadi sawa mmetudhulumu madeni yetu hatutawasamehe kamwe.
 
Tuna imani na Magufuli atashughulikia maswala hayo yote usijali mtumishi we mpe kura tuu yule mtendaji
 
Lowassa mabadiliko!hakuna tumaini ndani ya ccm tenaaa!nchi zilizopiga hatua kimaendeleo na watumishi kulipwa mishahara mizuri ni pale tu walipo badili mfumo wa vyama kama hapa kwetu na kuweka chama kipya.ni wakati wa watanzania kufurahia matunda ya mfumo wa vyama vingi tukifanya makosa kuitumia chance hii tutajuta chonde chonde mabadiliko lazima.
 
Hivi inakuwaje na naanzaje ja nafikiriaje na naona haja gani kupigia uduni wa maisha badala ya mabadiliko
 
Back
Top Bottom