Watumishi wa Mungu mpo?

Watumishi hao wengine ndio walikua wanapitisha kura feki! Wengine wanabariki udhalimu huu wa uchafuzi mkuu kule twitter!
 
Yuko yule baalam wa Lissu mtafute umuulize alipata wasaa wa kuongea na huyu mtu wake akampa ufafafanuzi wa nini alikifuta katika kukutana kwake na rais wa mashoga duniani?
 
Kuna kiongozi mmoja juzi kati alijitangaza kwa jina la Chidy, nimemuona sehemu anakata mauno tu
 
Watumishi walikuwa wanapanda majukwaani kwa wagombea wote. Hawa wamepoteza moral authority ya kuja tena kwa waumini wao na kuwaeleza kitu tofauti
 
Baada ya kugaragazwa vibaya mno mnaanza kukumbuka kuna watumishi wa Mungu. Tulieni dawa iingie vizuri, lazima muone aruweruwe.
Kugaragazwa wagaragazwe kwa halali, si tatizo. Faulu ya wazi wazi ndiyo inanifanya niwatafute watumishi. Umesha jiuliza chanzo cha vikundi vya kigaidi/waasi? Au unaongozwa na tumbo tu?!
 
Nafikiria kuacha kutoa sadaka kanisani na kuanza kutoa sadaka yangu kwa CHADEMA.

Hao wanaojiita watumishi wa Mungu wengi wao wameamua kukaa meza moja na watesi wetu wakinywa mvinyo na raha zote
Duh! Kweli ndugu umegusa mada pana sana.

Hawakujali ugumu wa maisha wa wasio katika SYSTEM, bali walihimiza collection ya sadaka katika nyumba za ibada.

Ni muda wa kupeleleka sadaka kwa masikini zaidi, wajane na yatima. Ukame utawale misikitini na makanisani. Wakalime nao sasa, hadi wapate ufahamu kuwa unahudumiwa kwa kuwa unafanya kazi ya Mungu. Ukiacha unaachwa
 
Nchi imefula

kuna Haja gani kuita uchaguzi ambao huja kutuumiza na kutuachia Chuki, makovu na Matatizo makubwa namna hii.???
 
Baadhi yao Ni Waganga Njaa Tu, Wamejionea Wenyewe
Wanamsifia Mtu, Hawakemei.
 
Hahaha sijui Askofu Rashidi ataendelea kufufua au ndio basi tena?!

Watakaokufa kuanzia sasa msiwe na matumaini, askofu Rashidi atakuwa bungeni.
 
Nchi imefula

kuna Haja gani kuita uchaguzi ambao huja kutuumiza na kutuachia Chuki, makovu na Matatizo makubwa namna hii.???
Hasira Ni Kubwa
Maumivu Tele, Kuna Mambo Yanachoma Moyo Yanaacha Midomo Wazi Unashindwa Kuzuia Machozi.
Vyombo Vya Habari Hoi Sana Vya Ndani Vinasifu
Vinaogopa Kusema Lolote
Kura Fake Tume Imeruka Kimanga
Tulitegemea Uchunguzi Ufanywe, Lakini Oops!!
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom