Watumishi Mbozi tunaaibishwa

mAgaziJuTO.

Senior Member
Feb 22, 2014
119
37
Kuna mwalimu mwenzangu kaniita nikamdhamini achukue mkopo wa pesa kwenye kampuni inayoitwa MGOSI SHOPPING CENTRE hapa wa riba ni 40% ya kiasi unachochukua.

Kilichonistua ni utaratibu wa kuacha ATM card na namba ya siri kwao, mshahara ukiingia wanatoa pesa yote, wanakata wanayodai na kinachobaki wanakurushia kupitia m-pesa.

Pembeni kulikuwa na kadi za bank zilizoachwa na wateja zisizopungua 500 nimesononeshwa sana na kitendo cha wao kuhodhi kadi na namba za siri za kadi ya mteja.

Kweli shida haina adabu.
 
Walimu wengi huko a toka makampuni mbalimbali ya Tokyo mikopo. Kwa bahati mbaya hawastukii riba kubwa insyotozwa na kampuni hizi. Makato yanapoanza wanajutia uamuzi wao wa kuchukua mikopo hiyo. Nawashauri walimu kusoma kwanza masharti ya mikopo kabla ya kukopa.
 
Kama Bank wanakopesha kwa 18% halafu wewe ukaenda kukopa kampuni kwa riba ya 40% lazima tuhoji uwezo wako wa kufikiri.
 
nchi hii kuna vitu tunailaumu serikali.. wakati ni ujinga wa raia wenyewe..

mwalimu mzima unaenda kopa na kuacha kadi yako ya bank kwa mtu..

ndio maana magufuli na majaliwa waliamua kusepa ualimu after only one year teaching.. sababu ya kukerwa na ujinga wa wenzao
 
Kama Bank wanakopesha kwa 18% halafu wewe ukaenda kukopa kampuni kwa riba ya 40% lazima tuhoji uwezo wako wa kufikiri.

Mkuu
Hapo Pia Utashangaa Hao Ndiyo Wanatakiwa Kuwafundisha Watoto Ama Taifa Liyaepuke Hayo
Lakini Wenyewe Wanayatenda Kwa Haraka
Hata Sasa Kama Kusoma Hujui Hata Tofauti Ya Riba Hawaioni?

Halafu Unaacha ATM Na Password
Hii Nchi Ina Majipu Mengi Sana!
 
Hao jamaa huwa wanafanya kazi na wafanyakazi wasiowaaminifu wa benki.

Ukienda kuchukua hela ndani, hupewi.
 
Hvi bado mnatumiaga ATM yaani mmi ningewakabidhi na ATM na password na vitambulisho wangeisoma namba mambo yote ni NMB mobile iyo salary wasingeiona hats dk 10 kwenye account yangu.
 
kwani ile benk ya walimu bado haijafunguliwa? /tatizo nn

benk ya walimu ingewasaidia, kuliko kulipa riba ya 40% au 18%.
 
Mkuu
Hapo Pia Utashangaa Hao Ndiyo Wanatakiwa Kuwafundisha Watoto Ama Taifa Liyaepuke Hayo
Lakini Wenyewe Wanayatenda Kwa Haraka
Hata Sasa Kama Kusoma Hujui Hata Tofauti Ya Riba Hawaioni?

Halafu Unaacha ATM Na Password
Hii Nchi Ina Majipu Mengi Sana!

Hii nchi bure kabisa!!,na hapo bado Elimu haijawa bure sasa ikiwa bure kuna hatari ya mambo kuwa mabaya zaidi.
 
Je wanaochukua mkop wana utindio wa ubongo? Nashauri hao jamaa wachuke zaidi ya 200% ya mkopo., na hiyo kadi ya benki wachukue milele. Ikiwa kama huyo mwalimu anamwadhibu mwanafunzi kwa kufeli mtihani, naye anastahili adhabu kali kwa ujinga huu. Yaani baadhi ya watumishi, hasa waalimu wanadhalilisha kada zao. CWT iweke faini kwa ujinga huu kwa wanachama wake.
 
Kama Bank wanakopesha kwa 18% halafu wewe ukaenda kukopa kampuni kwa riba ya 40% lazima tuhoji uwezo wako wa kufikiri.

Nikwambie rafiki yangu, sio kwamba hawaoni na sio kwamba uwezo was kufikiri no mdogo. Mwalimu anaajiriwa mshahara laki NNE sina hakika lakini no around hapo. Katika kufikiria kuwa anatakiwa kujipanga na kuanza maisha wengi hukimbilia mikopo ya benki.Sasa matumizi ya hiyo fedha ndio huwa shida. Ule mkopo hupunguza kiasi anachopokea ..take home. Kutoka hapo akipata tatizo kidogo atakopa tena. Mwisho wa Siku kiasi anachochukua ni kidogo had I aibu. Walimu wanakopa sana jamani. Inafika muda hata mwajiri anamzuia kukopa Benki kwa kuwa take home iliyopo ni ngumu kuweza kuishi kwa kiasi pungufu ya hapo. Hapo sasa ndio huwa wanaingia kwenye mikopo ya ajabu mitaani... Hali si nzuri kwa kweli no aibu. Hill lipo kwa walimu wengi mno nchini.
 
Back
Top Bottom