Watumishi Housing nyumba zenu ni kwa ajili ya kusaidia au kunyonya Watumishi?

ThaGreatman

JF-Expert Member
Sep 11, 2018
708
1,465
Nimekuwa nikiona matangazo ya mara kwa mara kuhusu nyumba zinazojengwa na watumishi housing company, nilivutiwa (kwa kuwa matangazo yao ni manono)

Nilipowapigia simu wakanielekeza kwenda ofisini kwao, (Jubilee Tower Floor ya nne). Nikaenda mpaka pale na kupewa maelekezo kadhaa....nikaambiwa Bei za nyumba (zipo mkoani) nikaambiwa bei Mil.68 kwa nyumba ya vyumba 3 (kimoja master,sebule, jiko na public toilet).

Nikaamua kuchagua hiyo, yenye 3 bedrooms na kupewa form ya kujaza then niirudishe ikiwa imejazwa vizuri (Nilifanya hivyo)

Kilichonishangaza ni kwamba siku nairudisha hiyo fomu, nikakutana na kitu kipya kabisa kwenye swala la malipo

Nyumba niliyoambiwa ni milioni 68, nikaambiwa nitatakiwa kuwa nailipia sh.laki 8 kila mwezi, kwa miaka 15,(yaani 800,000×12×15= Tsh.144,000,000/= (Najiuliza kwa bei hii kwa nyumba ya vyumba 3, unakuwa umemsaidia mteja au unamkamua kisawa sawa?)

Nilipomuuliza sababu za bei kuwa kubwa tofauti na tangazo la awali la mil.68 akanambia ni kwa sababu ya kulipia kwa mkopo,(yaani unailipia huku ukiwa unaishi ndani ya nyumba yenyewe) lakini najiuliza hii riba ya kutoka mil.68 mpaka mil.144 imekaaje?

Watumishi Housing Company, wapo kwa dhana ya kumsaidia mtumishi au kumnyonya? (watumishi wote ,ie umma na sekta binafsi, wote wanaweza kuzinunua hizo nyumba kwa kadri ya advertisement yao)

Jamani, tujipangeni mdogo mdogo tu tujenge, kama hali yenyewe ndiyo hii unaweza jikuta miaka 50 hii hapa na nyumba hauna....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ThaGreatman,
Hili swala tulisha discuss wakati fulani, wengine wakadai yakifanyika malipo yote unaponunua hizi nyumba ni sawa kama umelipa mkopo wenye mark up ya 2.11 mpaka 2.5! Wadau walibisha sana sana. nashukuru umeshuhudia.
Best option, nunua kiwanja, jenga taratibu kuliko kujiingiza kwenye hilo janga halafu ukaishia kushindwa malipo na kuwarudishia wenyewe.
 
Salamu wakuu,
Mkopo unaweza kuwa asset au liability , hii itategemea umekopa ili ufanyie nini huo mkopo wako. Ukiamua kukopa ili ununue nyumba, hakikisha riba inakuwa ndogo na muda wa kurejesha deni unapungua.

Hii mikopo ya ujenzi wa nyumba Kwa watumishi ilitakiwa iratibiwe na mfuko maalum kwa watumishi na wakopeshwe bila riba. Lengo ni kuwaletea makazi bora watumishi bila kuwaumiza. Mikopo ya bank inawaletea umaskini tu, sasa umekopa nyumba ya thamani ya 68m . Unarejesha 144m kwa miaka 15 huku nikuumizana tu.

Nawashauri jengeni kidogo kidogo, mfano hiyo pesa yako ya marejesho 800,000 kwa mwezi ukiwekeza kwenye ujenzi wako kila mwezi kwa miaka 15 ya urejeshaji wa mkopo wako kwenye hizo nyumba si utakuwa umejenga nyumba mbili bora kabisa.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ukiwa na 35m unajenga nyumba ya kuishi safi kabisa ya vyumba 3

Sent using Jamii Forums mobile app
Haitakua nyumba safi.. wacha kumdanganya mwenzako... milion 35 itakua nyumba ya hovyo hovyo with cheap materials both structurally na finishings... nyumba nzuri ya 3 bedrooms walau from 60m na kuendelea mpaka 100 uko kama unainclude na vitu kama fence, paving etc depending na size ya kiwanja.
 
35M inatosha kwa kuhamia ukiwa unamalizia taratibu
Haitakua nyumba safi.. wacha kumdanganya mwenzako... milion 35 itakua nyumba ya hovyo hovyo with cheap materials both structurally na finishings... nyumba nzuri ya 3 bedrooms walau from 60m na kuendelea mpaka 100 uko kama unainclude na vitu kama fence, paving etc depending na size ya kiwanja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo 76,000,000 ndo faida watakayopata kwa kufanya biashara nawe kwa miaka 15.

Hivyo ndivyo baishara ya "Mortgage" inavyofanya kazi.
Haifanyi kazi hivyo brother riba haiwezi kuwa kubwa hivyo hapo cdhani kama watapata wateja. Kama ni nyumba za serikali inabidi serikali upunguze bei kwani serikali haitakiwi ifanye biashara. Serikali ipo kwa ajili ya watanzania. Serikali inabidi bei ziwe chini hata ikibidi wafanya kazi wa serikali waulize hata kwa 40m na wananchi wa kawaida wauziwe 50m kwa kufuata vigezo. Lengo ni kusaidia wananchi. Tanzania serikali ipo kwa ajili ya viongozi ndio maana wengi wanakimbilia kuongoza
 
Haitakua nyumba safi.. wacha kumdanganya mwenzako... milion 35 itakua nyumba ya hovyo hovyo with cheap materials both structurally na finishings... nyumba nzuri ya 3 bedrooms walau from 60m na kuendelea mpaka 100 uko kama unainclude na vitu kama fence, paving etc depending na size ya kiwanja.
labda kama unawaachia mafundi kila kitu ila milion 35 unajenga nyumba safi sana ,acha kuogopesha watu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom