Watumishi hewa: Kompyuta yenye rekodi yaibwa, wakopa benki kwa majina hewa

Naomba kujuzwa jamani kwa wataalamu, mimi nilikuwa mwajiriwa wa serekali miaka 15 iliyopita baada ya kuamua kurudi shule nikaacha kazi na kulipwa stahiki zangu ila miaka ya 2003 nilisikia mshahara bado unaingia nilipofatilia pale nikaambiwa ukiibgia ubarudishwa sasa sijui labda na jina labgu bado liko huko au vipi, kwa nini tusiwekewe majina ili tujue na tukatoe ushahidi ili hao watu wafungwe???@zambez dr. Mifugo zamani....Arusha town
 
Server pia imeibwa. Hakuna kurudi nyuma. Tunaunga mkono juhudi za Mr President JPM. Juhudi zenu za kunkatisha tamaa hazitasaidia kitu

Hicho ndo nilichokuwa nawaza, server na backups zingine ziko wapi? By the way system ipo connected na hazina (sina uhakika sana), haitakiwa kuwa tatizo kama TEHAMA wapo
 
Nasikia kalipoanza kazi huko ukerewe kalikuwa kembamba kama mimi. Ila nasikia kwa sasa hata T-shirt mpya za CWT inaweza kukabana namna kalivyonenepa
Daaah nimecheka sana, ni kweli nampata huyo Dogo, alikuwa anaendesha pikipiki flan hivi ki 110.
Kumbe alikaimishwa udt? Namuona fb na picha zake akila bata Mwanza town.
Alitakiwa amtafute mtaalamu mtasiwa amfudishe jinsi ya kupiga.
 
Server pia imeibwa. Hakuna kurudi nyuma. Tunaunga mkono juhudi za Mr President JPM. Juhudi zenu za kunkatisha tamaa hazitasaidia kitu
Siku hizi ni standard practice ku backup data kwenye server (cloud) . Mkuu wa mkoa pamoja na kusisitiza computer ipatikane la muhimu ni kupatikana data- je halmashauri ilibackdata ndio swala muhimu.
 
Pia huko chuoni kuna majipu. Unakuta mwanafuzi analipiwa na bodi ya mikopo anapoacha chuo mkopo wake unaendelea kuja.sasa sijui ni nani anaipokea iyo pesa...??
 
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella ametoa saa 24 kwa kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Ukerewe, Ally Mkaripa, kuhakikisha wanaitafuta hadi kuipata komputa iliyoibwa usiku wa kuamkia April 22, 2016 kwenye chumba kinachotumika na mifumo ya ukusanyaji mapato na uandaaji wa malipo ya Halmashauri (EPICOR)

Mhe. Mongella ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye kikao cha kujitambulisha kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ambapo taarifa za awali zilionesha kutokea kwa wizi wa komputa moja iliyofungwa kwenye chumba cha mifumo ya komputa ambayo ndio hutumika kuandaa malipo mbali mbali ya halmashauri.

“OCD kesho nitakwenda kanisani asubuhi, ikifika saa 8.00 mchana nataka taarifa niikute mezani kwangu, vinginevyo hatutaelewana", amesema Mongella na kuongeza sisi tunajua nini chakufanya kama kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa lakini na wewe tumia mbinu zako kuweza kubaini wapi ilipo kompyuta hiyo.

Akizungumza kando ya Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri, Kaimu Mhazini wa Halmashauri hiyo, Baraka Munuo alidai kupokea taarifa za kupotea kwa Komputa hiyo kutoka kwa afisa TEHAMA wa halmashauri ya Ukerewe.

Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa Mwanza, amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe kupitia mafaili na kubaini watumishi waliofanya kazi katika kituo hicho kwa muda mrefu, jambo ambalo Mkuu wa Mkoa amedai linachangia watumishi kufanyakazi kwa mazoea.

”Mkurugenzi nakuagiza pitia mafaili ya watumishi ili kubaini wote waliokaa katika kituo hiki kwa muda mrefu. Haiwezekani mtu amekaa hapa miaka ishirini na moja halafu uniambie kwamba atakuwa na maarifa mapya, hapana" alisema Mongella na kuongeza, Sasa nakuagiza pitia mafaili yao na kama kuna mtumishi aliye kaa kwa zaidi ya miaka kumi atafutiwe kituo kingine.

Wakati huo huo, MSAKO ulioanzishwa na Rais John Magufuli wa kutokomeza tatizo la wafanyakazi hewa katika utumishi wa umma, umeendelea kuibua mazito, ambapo mkoani Kilimanjaro, Benki ya CRDB imejikuta ikitoa mkopo kwa waliokuwa wafanyakazi hewa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Helga Mchomvu aliyasema hayo akidai kuwa, yamegundulika baada ya Serikali kuunda kamati za uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya Sh milioni 500 katika halmashauri hiyo.

Kabla ya kuibuka kwa kisa hicho kinachoonesha namna wafanyakazi hewa alivyokuwa wakiibia nchi, hivi karibuni mkoani Singida, Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Imani Nyamangaro, alipandishwa kizimbani akidaiwa kujilipa mishahara ya wastaafu 57, yenye thamani ya Sh milioni 29.4.

Mbali na mhasibu huyo, Rais Magufuli alipokuwa mapumziko kijijini kwake Mlimani, katika Wilaya ya Chato mkoani Geita, alieleza kisa kingine kilichoshitua jamii kuwa katika Mamlaka ya Mapato (TRA), kulikuwa na mtumishi mmoja ambaye alikuwa akilipwa mishahara ya watu 17.

Akizungumza jana, Mchomvu alidai kuwa watumishi watatu wa halmashauri hiyo; wawili wa Idara ya Utumishi na mmoja Mchumi, walikopa katika Benki ya CRDB Sh milioni 35.2, kwa kutumia majina ya wafanyakazi hewa.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Mkuu Idara ya Utumishi na Utawala, Gudila Mashele, Ofisa Utumishi Daraja la Kwanza, Faraja Ndatu na Mchumi Daraja la Pili, Isaiah Bayege. Kutokana na tuhuma hiyo iliyoibuliwa na kamati hizo za uchunguzi, Mchomvu alisema Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Hai, limewafukuza kazi watumishi hao.
CHANZO: Habarileo
 
Ni upuuzi na chuki kudhani kuwa wafanyakazi hewa wameanza awamu ya nne, labda kama una lako jambo


Mnyonge mnyonge ila haki yake apewe....Hao watumishi hewa hawakuanza AWAMU YA NNE jamani...walianza muda mrefu tuu...chekini taarifa zao za kuanza malipo
 
Mwigulu alithubutu ila siasa ilimzibiti!!


Tatizo anayekula ktk hili sio mmoja...Kila mmoja ana sehemu yake ya kula. Uovu ni mwingi. Hata hawa wanaochonga chonga wangepewa nafasi hizi wangekula....Tatizo watanzania wengi ni maskini, mishahara ni midogo sana kuliko mahitaji. Muda mwingi unamalizia kazini, hatufanyi kazi kwa masaa, tungekuwa tunalipwa kwa masaa ingekuwa nafuu, lkn mtu unamaliza masaa nane yote kazi moja halafu mshahara mwisho wa mwezi mdogooo una watoto wanakusubiri, ukitoka kazini na foleni nyumbani unafika saa moja usiku au kumi na mbili, hapo huwezi fanya kazi part time kwingine.

Pia tatizo ni mfumo wa elimu yetu. Sasa hivi janga kubwa ni kuwa watu hawasomi kwa kuwa anachokisoma anakipenda anasoma basi tuu kwasababu hii kazi ina hela..hivyo lazima akifika kazini apige dili ile mbaya.

Pia TCU imekuwa jipu, inachagulia wanafunzi wa vyuo course za kusoma wakati mwanafunzi huyo hakuwa anapenda course hiyo. Je unategemea huyu mwanafunzi akimaliza hiyo kazi aliyosomea atapenda kuifanya kwa ari au atafanya basi tuu ili apate hela? Hawa nao wanakera kweli ni jipu kubwa.

Sasa hivi ni wakati wa kumruhusu kijana akifika chuo achukue course anayoipenda yeye ili aje atumikie alichokisoma vizuri.
 
Pana ombwe la uelewa hapa. Kompyuta ya EPICOR ni maalum kwa kufanyia malipo ya halmashauri au Wizara. Hii inakuwa chini ya wahasibu wakuu wa maeneo hayo.

Kazi ya mtandao wa EPICOR hauingiliani na mtandao wa LAWSON ambao upo chini ya Afisa Utumishi Mkuu wa Halmashauri au wa Wizara.

Mifumo yote hii miwili server zake zipo maeneo tofauti. Kwa ndani, Server ya LAWSON ipo Utumishi Dar. Ukiiba hiyo kompyuta utakuwa hujaiba chichote kuhusu kumbukumbu. Watafunga nyingine na zitakuwepo vilevile.

Hali kadhalika kompyuta za EPICOR server ipo Hazina Dar na TAMISEMI Dodoma.

Panahitajika maelezo zaidi ili tujue wameathirikaje kwa data. Naweza kuwaelewa kama watasema walikuwa wamehifadhi data hizo kwenye hiyo kompyuta nje ya mfumo.

Swali la kujiuliza, hawakuwa na backup kama flash disk? Kuna mengi ya kutaka kujua kuhusu kadhia hiyo.
Kwanza nikushukuru kutupa mwanga zaidi wa matumizi ya hizi computer na sehemu ziliko server zake kama hazina na tamisemi.Jambo la kujiuliza ni kweli hapo Ukerewa zinapofanyia kazi hizi computer hizo hawana hata backup flash disk au hawajui umuhimu wake?Mbona hata sisi wenye computer majumbani tunakuwa na data flash kwa kuelewa computer inaweza chezewa data,kuungua au kuibiwa ila data zake zinakuwepo ukiwa na flash disk? Yawezekana kweli kwa kuelewa wakiingiza kwenye hizo computer uovu wao wote watakuja umbuka na wakawa wanaziingiza nje ya mfumo.Yote haya yatabainishwa na ukweli toka ziliko server (utumishi).Wizi na ufisadi nchini ni mkubwa sana.Sasa kama huko walikokopa mamillion toka benki kwa kutumia hayo majina hewa ukipita uchunguzi wa kina utakuta ni karibu mikoa yote.Mabenki yanakua na bima kubwa ila sidhani wakishagundua mikopo ilitolewa kwa watumishi h ewa watalipia uzembe huo.Hofu nyingine ipo kwa baadhi ya wanasheria wa serikali na waendesha mashtaka wao kuweza kushinda kesi mahakamani.Pia uaminifu kwa baadhi ya watekelezaji wa sheria huko mahakamani rushwa zimetawala mno.Bunge liongeze ukali wa sheria katika hukumu (ingawa nina wasiwasi kwa wabunge walio wengi huko) itamkwe na kufilisiwa mali sio kusema tu akimaliza adhabu alipe upotevu.Iwepo sheria mpya ya kuajiri itakayomtaka anayeajiriwa ngazi yoyote serikalini na halimashauri kuwa na wadhamini wasiopungua wanne au zaidi kutegemea na ngazi(position) anayoajiriwa wenye mali za kudumu zisizohamishika kama mashamba makubwa yenye hati na majumba makubwa ya thamani na yenye hati ili yauzwe endapo mtumishi atakwapua hela za umma.Utaratibu huu ulitumika miaka ya nyuma kwenye vyama vya ushirika kwa mafanikio makubwa na vyama vilistawi bila kuibiwa. Nyanza,Kncu na Bcu/Kcu kuvitaja vichache.Jambo jingine la kurejesha uzalendo kwa watumishi ni kulirejesha azimio letu la Arusha na kuwapa wananchi katiba kadri ya mapendekezo yao waliyomkabidhi judge Warioba.Usumbufu kwa raisi kuhangaika na majipu utamalizwa na azimio la Arusha wala sio la Zanzibar walikoenda wajanja na kujipa mamlaka ya kuwa na mabiashara makubwa kuanzia hisa kwenye makampuni,kumiliki maduka makubwa meli hadi migodi ilihali wao ni waajiriwa wa wananchi.Raisi haya yapo kwenye uwezo wako haswa ukishakabidhiwa kofia yauenyekiti chama taifa mwezi June mwaka huu.Pamoja na kwamba tunaendelea kuridhishwa na utendaji wako na kuzidi kukuombea ulinzi wa MWENYEZI MUNGU ukitekeleza hili utaongoza raha mstarehe na kujihakikishia kipindi chako cha pili kwa kampeni kidogo sana.
 
Huyo jamaa anaitwa baraka abanwe vizuri asema komputer zimeenda wapi alikuwa alikuwa anakaimu DT hapo UKEREWE sasa kwa muda mfupi tu miaka miwili amenunua xtrail mpya ameshaajinga mwanza ,na viwanja kibao kule buhongwa ,
Kijamaa flani kina nyodo sana waseme komputer za EPICOR zimeenda wapi
Jamani hakuna Computer inaitwa EPICOR, bali kuna computer inayotumia mfumo au software ya EPICOR. So kilichoibiwa ni computer au ni software ya EPICOR???????
 
Back
Top Bottom